Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sera ya jumuiya

Jinsi ya kusaidia kukomesha biashara haramu ya kusafirisha binadamu

Kama Mwenyeji au mgeni, unaweza kuchukua hatua kuhusu jinsi ya kutambua na kuitikia hali inayoweza kutokea ya biashara haramu ya kusafirisha binadamu kwenye nyumba yako. Kwa kuzingatia jambo hili, tunakuhimiza sana uripoti visa vinavyotuhumiwa vya biashara haramu ya kusafirisha binadamu kwenye shirika la National Human Trafficking Hotline la Marekani. Ikiwa uko nje ya Marekani, unaweza kupata mashirika kote ulimwenguni ambayo hushughulikia tatizo la biashara haramu ya kusafirisha binadamu katika Global Modern Slavery Directory (GMSD).

Kufafanua biashara haramu ya kusafirisha binadamu

Fasili ya biashara haramu ya kusafirisha binadamu inaweza kutofautiana kulingana na nchi uliyopo, lakini fasili za nchi nyingi zinatumia mambo matatu ya msingi  yaliyotolewa na Umoja wa Mataifa. Hali za usafirishaji haramu wa binadamu lazima zijumuishe: 

  1. Kitendo: kuajiri, kusafirisha, kuhamisha, kuhifadhi au kupokea watu. 
  2. Njia: tishio au matumizi ya shuruti, utekaji, ulaghai, kulazimishwa au matumizi mabaya ya madaraka. 
  3. Kusudi: unyanyasaji ikiwemo unyanyasaji wa kazi ya ngono kwa wengine au aina nyingine za unyanyasaji wa kingono, kazi au huduma za kulazimishwa, utumwa au vitendo sawa na utumwa au kuondolewa kwa viungo.

Ni nani aliye hatarini

Ingawa mtu yeyote anaweza kusafirishwa kiharamu, watu wengine wako hatarini zaidi kuliko wengine kwa sababu ya mahitaji ya msingi ambayo hayajatimizwa. Hawa ni pamoja na watu wanaoishi katika umaskini au katika makazi duni, na watu wenye historia ya kiwewe au uraibu. Kwa sababu ya ubaguzi wa sasa na wa kihistoria na ukosefu wa usawa, watu wasio wazungu, wahamiaji na watu wanaotambulika kama LGBTQ+ wana uwezekano mkubwa wa kutumiwa kwa sababu ya udhaifu huu na kukabiliwa na biashara haramu ya kusafirisha watu kiharamu. 

Ili hali iwe biashara haramu ya kusafirisha binadamu, ishara za ulaghai wa nguvu, au kulazimishwa zinahitaji kuwepo. Hizi zinaweza kuonekana kama:

  • Mtu hawezi kuondoka kwenye hali fulani kwa uhuru au kwa usalama na hana udhibiti wa pesa zake na  mali zake binafsi.
  • Mtu analazimika kufanya kazi katika hali tofauti na zile ambazo zilikubaliwa hapo awali wakati wa kumwajiri
  • Mtu analazimishwa kutumia dawa za kulevya au pombe na mtu mwingine
  • Vitisho vya kutumia nguvu au matumizi ya nguvu za kimwili au vurugu 
  • Kumzuia mtu kihalisi
  • Majeraha ya kimwili

Sifa unazoweza kukutana nazo ikiwa unyonyaji unatokea kwenye nyumba:

  • Kazi ya kulazimishwa:
    • Mfanyakazi ni mtoto
    • Dalili za usafi duni, utapiamlo au uchovu
    • Mfanyakazi anapewa malazi na mwajiri katika sehemu isiyofaa (hakuna faragha/mpangilio wa kulala wa muda)
    • Kudai pesa kwa mwajiri na/au kutolipwa kile walichoahidiwa au wanachodai
    • Mfanyakazi haruhusiwi kupumzika kwa wakati unaofaa
    • Mfanyakazi anafanya kazi katika mazingira hatarishi au yasiyofaa na hajapewa vifaa au mafunzo sahihi ya usalama
    • Anaonekana kufuatiliwa na mtu mwingine wakati wa kuzungumza au kuingiliana na wengine
  • Biashara haramu ya kusafirisha watu kwa ajili ya ngono:
    • Anwani ya tangazo inarejelewa katika matangazo ya mtandaoni ya biashara ya ngono
    • Ripoti za wageni wa mara kwa mara wasioidhinishwa kwa saa tofauti.
    • Idadi kubwa ya vifaa vya ngono katika nyumba hiyo
    • Uwepo wa vifaa vya kibiashara vilivyowekwa kwa ajili ya kurekodi video/kupiga picha

Nini cha kufanya ukikumbana na hali inayoweza kutokea ya biashara haramu ya kusafirisha binadamu

Kama Mwenyeji au mgeni, unaweza kusaidia kukomesha biashara haramu ya kusafirisha binadamu. Ukikumbana na hali inayoweza kuwa biashara haramu ya kusafirisha binadamu kwenye nyumba yako, unaweza kupata msaada kwa kuwasiliana na National Human Trafficking Hotline kwa simu 1-888-373-7888, kwa kutuma ujumbe "BeFree" kwenda 233733 au kwa mawasiliano ya moja kwa moja kwenye humantraffickinghotline.org/chat. Nambari hii ya simu ya dharura inapatikana saa 24, bila malipo, ni ya siri na iko katika lugha 200 na zaidi. 

Unapaswa pia kuripoti tukio linaloweza kutokea la biashara haramu ya kusafirisha binadamu kwa Airbnb. Kituo cha Usalama cha Airbnb ni kitovu cha usalama cha ndani ya programu kilicho na nyenzo muhimu. Unaweza kufikia Simu ya Usaidizi wa Dharura ya Airbnb kupitia Kituo cha Usalama na pia huduma za dharura za eneo husika popote ulipo ulimwenguni.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili