Pata pesa kwenye eneo lako la kipekee

Tupatie maelezo mafupi kuhusu eneo lako

Pata pesa kwenye eneo lako la kipekee

Tupatie maelezo mafupi kuhusu eneo lako

Andaa sehemu ya kipekee ya kukaa kwenye Airbnb

Zaidi na zaidi, wageni wanakuja kwenye Airbnb wakitafuta matukio ya kipekee ya kusafiri. Kuna nyumba zaidi ya 150,000 za kukumbukwa kama vile boti, nyumba za kwenye mti, hema, vijumba na nyumba za mashambani kwenye tovuti yetu leo. Aina hizi za sehemu za kukaa za kipekee na wenyeji wanaoziandaa, ni sehemu ya kile kinachoifanya jumuiya yetu kuwa ya kipekee. Karibisha wageni katika nyumba yako kwenye Airbnb na upate pesa unaposhiriki sehemu yako ya kipekee na jumuiya yetu ya wageni wa kimataifa.

Zaidi na zaidi, wageni wanakuja kwenye Airbnb wakitafuta matukio ya kipekee ya kusafiri. Kuna nyumba zaidi ya 150,000 za kukumbukwa kama vile boti, nyumba za kwenye mti, hema, vijumba na nyumba za mashambani kwenye tovuti yetu leo. Aina hizi za sehemu za kukaa za kipekee na wenyeji wanaoziandaa, ni sehemu ya kile kinachoifanya jumuiya yetu kuwa ya kipekee. Karibisha wageni katika nyumba yako kwenye Airbnb na upate pesa unaposhiriki sehemu yako ya kipekee na jumuiya yetu ya wageni wa kimataifa.

Airbnb ni nini?

Airbnb huwaunganisha watu na maeneo ya kukaa na mambo ya kufanya duniani kote. Jumuiya hii huendeshwa na wenyeji, ambao huwapa wageni wao fursa ya kipekee ya kusafiri kama wakazi.

Kwa nini ukaribishe wageni kwenye Airbnb?

Airbnb inafanya iwe rahisi na salama kuwakaribisha wasafiri. Una udhibiti kamili juu ya upatikanaji, bei, sheria za nyumba na jinsi unavyoingiliana na wageni.

Tunakuunga mkono

Ili kulinda usalama wako, wa nyumba na mali zako, tuna bima ya USD Milioni 1 ya kulinda kila nafasi iliyowekwa dhidi ya uharibifu wa mali na bima nyingine ya USD Milioni 1 dhidi ya ajali.

Kukaribisha wageni katika hatua 3

Tangaza sehemu yako bila malipo

Shiriki sehemu yoyote bila malipo ya kujisajili, kuanzia nyumba ya kulala wageni hadi banda na sehemu nyingine mbalimbali.

Chagua jinsi unavyotaka kukaribisha wageni

Chagua ratiba yako mwenyewe, bei na mahitaji kwa wageni. Tuko tayari kukusaidia mpaka mwisho.

Mkaribishe mgeni wako wa kwanza

Mara tangazo lako litakapoanza kupeperushwa, wageni wanaostahiki wanaweza kuwasiliana nawe. Unaweza kuwatumia ujumbe wa maswali yoyote kabla ya wao kufika kwenye sehemu ya kukaa.

Guarantii ya Mwenyeji ilinisaidia kuamua nijiunge na Airbnb kwa sababu ikiwa kutatokea uharibifu au matatizo, watanisaidia.
Guarantii ya Mwenyeji ilinisaidia kuamua nijiunge na Airbnb kwa sababu ikiwa kutatokea uharibifu au matatizo, watanisaidia.

Dennis hukaribisha wageni jijini London kwa sababu ya urahisi wa kufanya mambo jijini humo

Dennis hukaribisha wageni jijini London kwa sababu ya urahisi wa kufanya mambo jijini humo

Pata maelezo kuhusu wanavyokaribisha wageni
Guarantii ya Mwenyeji ilinisaidia kuamua nijiunge na Airbnb kwa sababu ikiwa kutatokea uharibifu au matatizo, watanisaidia.
Guarantii ya Mwenyeji ilinisaidia kuamua nijiunge na Airbnb kwa sababu ikiwa kutatokea uharibifu au matatizo, watanisaidia.

Dennis hukaribisha wageni jijini London kwa sababu ya urahisi wa kufanya mambo jijini humo

Dennis hukaribisha wageni jijini London kwa sababu ya urahisi wa kufanya mambo jijini humo

Pata maelezo kuhusu wanavyokaribisha wageni

Tunakushughulikia

Tunafahamu kwamba ni kipaumbele kuwaamini watu wanaoishi nyumbani kwako. Airbnb inakuruhusu uweke mahitaji madhubuti kwa watu wanaoweza kuweka nafasi na uwajue wageni kabla hawajaja kukaa.

Hata hivyo, jambo fulani likitokea, tuko tayari kukusaidia. Kuanzia bima yetu ya USD milioni 1 dhidi ya uharibifu wa nyumba hadi huduma ya kimataifa ya saa 24 kwa siku, unasaidiwa kama mwenyeji wakati wote.

Uwezo wa kuhitaji kitambulisho cha serikali kabla ya kuweka nafasi
Sheria za Nyumba ambazo ni lazima wageni wazikubali
Fursa ya kusoma tathmini za safari zilizopita
Bima isiyolipishwa ya USD Milioni 1 dhidi ya uharibifu wa nyumba
Usaidizi kwa wateja ulimwenguni kote wa saa 24 kwa siku

Malipo yamerahisishwa

Toza unachotaka

Daima unachagua bei yako. Unahitaji msaada? Tuna nyenzo za kukusaidia ukidhi mahitaji katika eneo lako.

Lipa ada ya kiwango cha chini

Hakuna gharama ya kujisajili. Kwa kawaida Airbnb hutoza wenyeji kiwango sawa cha asilimia 3 kwa kila nafasi inayowekwa, hizi ni kati ya ada za chini zaidi katika tasnia hii.

Pokea malipo haraka

Mara mgeni anapoingia, tunaweza kutuma pesa zako kupitia Paypal, kuweka kwenye akaunti yako moja kwa moja, au kupitia njia nyingine zilizopo.

Majibu kwa maswali yako

Nani anaweza kuwa mwenyeji wa Airbnb?

Ni rahisi kuwa mwenyeji wa Airbnb katika maeneo mengi na kutengeneza tangazo ni bila malipo wakati wote. Fleti nzima na nyumba, vyumba vya kujitegemea, nyumba za kwenye mti na makasri ni baadhi tu ya majengo ambayo wenyeji wameshiriki kwenye Airbnb.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kile kinachotarajiwa kwa wenyeji, angalia miongozo ya jumuiya ya Airbnb, ambayo inazingatia usalama, ulinzi na kutegemeka na viwango vya ukarimu, ambavyo husaidia wenyeji kupata tathmini nzuri kutoka kwa wageni.

Ni nini kinachohitajika kwa wageni kabla ya kuweka nafasi?

Tunaomba kila mtu anayetumia Airbnb atupatie taarifa fulani kabla ya kusafiri pamoja nasi. Wageni wanahitaji kujaza taarifa hii kikamilifu kabla ya kutuma ombi la kuweka nafasi. Taarifa hizi husaidia kuhakikisha kuwa unamjua mtu anayekuja na jinsi ya kuwasiliana na mgeni.

Mahitaji ya Airbnb kwa wageni ni pamoja na: • Jina kamili • Anwani ya barua pepe • Nambari ya simu iliyothibitishwa • Ujumbe wa utambulisho • Kukubaliana na Sheria za Nyumba yako • Taarifa za malipo

Wageni wanatarajiwa kuwa na picha ya wasifu, ingawa hilo si takwa. Unaweza pia kuwahitaji wageni kutoa kitambulisho kabla ya kuweka nafasi kwenye sehemu yako.

Je, inagharimu kiasi gani kutangaza sehemu yangu?

Kujisajili kwenye Airbnb na kutangaza nyumba yako ni bila malipo kabisa.

Mara tu mtu anapoweka nafasi kwako, tunatoza ada ya huduma ya Airbnb kwa wenyeji, kwa jumla ni asilimia 3, ili kusaidia kugharamia uendeshaji wa biashara.

Je, nina kinga gani dhidi ya uharibifu wa nyumba?

Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb hutoa bima ya hadi dola 1,000,000 kwa mwenyeji kwa uharibifu wa mali iliyowekewa bima katika hali ambayo ni ya nadra ambapo uharibifu wa mgeni uko juu ya amana ya ulinzi au ikiwa amana ya ulinzi haijawekwa.

Mpango wa Garantii ya Mwenyeji haushughulikii pesa taslimu na hisa, vitu vya thamani vinavyokusanywa, sanaa adimu, vito, wanyama vipenzi au dhima ya mtu binafsi. Tunapendekeza wenyeji waweke vitu vyao vya thamani mahali salama au waviondoe wanapopangisha nyumba yao. Mpango huu pia haushughulikii upoteaji au uharibifu wa mali kwa sababu ya uchakavu unaotokana na matumizi.

Pata maelezo zaidi kuhusu Garantii ya Mwenyeji kwenye http://airbnb.com/guarantee

Ni jinsi gani ninaweza kuchagua bei ya tangazo langu?

Bei unayotoza kwa ajili ya tangazo lako ni uamuzi wako mwenyewe kabisa. Ili kukusaidia kuamua, unaweza kutafuta matangazo yanayofanana na lako katika jiji lako au kitongoji ili upate kujua bei za soko.

Ada za Ziada • Ada ya usafi: Unaweza kujumuisha ada ya usafi katika bei yako ya kila usiku au unaweza kuongeza ada ya usafi katika mipangilio yako ya bei. Ada nyinginezo: Ili kutoza ada za ziada nje ya bei zako (kama ada ya kuchelewa kuingia au ada ya mnyama kipenzi), lazima kwanza uwafichulie wageni tozo kama hizo kabla hawajaweka nafasi kisha utumie Kituo chetu cha Usuluhishi ili kuomba kwa usalama malipo ya ada za ziada.

Airbnb inawezaje kunisaidia katika kupanga bei?

Nyenzo ya Upangaji Bei Kiotomatiki hukuruhusu kuweka bei zako kwenda juu au chini kiotomatiki kulingana na mabadiliko katika mahitaji ya matangazo kama yako.

Nyakati zote wewe huwajibika kwa bei yako, kwa hivyo Upangaji Bei Kiotomatiki unadhibitiwa na mipangilio mingine ya bei unayochagua, nawe unaweza kurekebisha bei za usiku wakati wowote.

Upangaji Bei Kiotomatiki unategemea aina na eneo la tangazo lako, msimu, mahitaji na mambo mengine (kama vile mambo yanayotukia katika eneo lako).

Uko tayari kupata mapato?

Uko tayari kupata mapato?