SIMULIZI ZA WENYEJI

Jinsi Silvia na Mateo wanavyokaribisha wageni

Silvia na Mateo hukaribisha wageni jijini London kwa sababu wana uhuru wa kubadilisha mambo

Ni nini kilichokupa motisha yako ya kuanza kukaribisha wageni?

Silvia: Nimekuwa mtumiaji wa Airbnb kwa miaka mingi kama mgeni na nimeipenda dhana hii wakati huo wote. Niliamua kuanza kuwa mwenyeji kwa sababu nina chumba cha ziada na Airbnb inanipa uhuru wa kubadilisha mambo.

Ulikuwa na wasiwasi upi kabla ya kuanza kukaribisha wageni?

Silvia: Kwas sababu mimi huwakaribisha wageni katika nyumba ninamoishi, nilikuwa na wasiwasi sana kuhusu usalama, kelele nyingi na uwezekano wa uharibifu kutokea ndani ya nyumba.

Je, Garantii ya Mwenyeji ni jambo muhimu kwako?

Mateo: Kuwa na Garantii ya Mwenyeji hutupa utulivu, kwa sababu ajali zinaweza kutokea. Kuwa na mpango wa ulinzi hukupa utulivu zaidi.

Je, una vidokezi au ushauri wowote kwa mtu anayefikiria kuwa mwenyeji?

Silvia: Ikiwa unafikiria kuifungua nyumba yako kwa wageni, usiogope kuweka sheria zako mwenyewe. Weka bayana mambo ambayo wageni wanaruhusiwa na hawarusiwi kuyafanya ili wasiwe na matarajio tofauti. Mawasiliano ni muhimu sana.

Je, kuwa mwenyeji kumebadilisha mtindo wako wa maisha?

Silvia: Nina mapato zaidi, ambayo yanawezesha kusafiri kwa njia ambayo haingewezekana bila Airbnb.

Ni nini unachopenda zaidi kuhusu kuwa mwenyeji?

Silvia: Kuwa mwenyeji kumeniwezesha kukutana na watu kutoka pande zote za ulimwengu. Wageni hawaachi kunishangaza. Kila wakati huwa tukio tofauti, na mara nyingi huwa wanaleta zawadi kutoka nchi zao. Mateo: Kwa kweli unapata kuwajua wageni wako nao wanapata kukujua. Na wakati mwingine huwa wanatualika nyumbani katika mji wao ili warudishe fadhila kwa njia fulani na kutufanya tuhisi kama tuko nyumbani.

Simulizi zingine za wenyeji

Anza kutayarisha tangazo lako