SIMULIZI ZA WENYEJI

Jinsi Lym anavyokaribisha wageni

Lym hukaribisha wageni huko Puerto Rico, ili ajiongezee mapato.

Ni nini kilichokupa motisha yako ya kuanza kukaribisha wageni?

Mimi ni mama ambaye hajaolewa. Nilikuwa nafanya kazi ya serikali kama wakili na sikuwa na mapato mengi kama nilivyotaka. Nilikuwa na jirani ambaye alikuwa akifanya Airbnb akikodi chumba cha kibinafsi ndani ya nyumba yake. Aliniambia jinsi hali ilivyokuwa na nikawaza, "Nadhani naweza kufanya hivyo na fleti yangu."

Je, unajiandaa vipi kuhakikisha kuwa wageni wanafurahia wanapowasili?

Kwa kweli, huwa nafanya usafi sana. Huwa ninaisafisha fleti mimi mwenyewe kwa sababu wakati mwingine huwa nawalipa watu wanisafishie lakini hawawezi kusafisha nifanyavyo mimi. Huwa natayarisha friji endapo watataka kuhifadhi chakula chao. Ninaweza kuweka bia za huku kwenye friji ili wazijaribu na huwa naweka dokezo juu yake ili niwajulishe ni zao.

Ni kwa nini unaendelea kuwa mwenyeji?

Sisi hujenga urafiki. Vilevile, hii ni njia ya kuwa na mapato ya ziada kutokana na kufanya mambo ninayoyafurahia.

Je, una vidokezi au ushauri wowote kwa mtu anayefikiria kuwa mwenyeji?

Nadhani wanapaswa kuangalia tovuti ya Airbnb na wafahamu jinsi inavyofanya kazi. Angalia kinga na aina za usalama unazoweza kuweka kwa ajili ya nyumba unayoitangaza, kama vile aina za ukaguzi ambazo unaweza kufanya ili kutayarisha tangazo lako. Tovuti ya Airbnb ina chaguo nyingi kwa wenyeji wa aina tofauti.

Je, kuna matukio mnayoyathamini sana katika muda wenu wa kuwakaribisha wageni?

Kitu ninachokipenda zaidi ni kukutana na watu wapya. Huwa nina mazungumzo mazuri na wageni wangu. Wakati mwingine huwa wananialika tunywe mvinyo pamoja na tunakuwa na mazungumzo marefu nyumbani tu. Ninawachukulia wageni kama marafiki. Na wananiachia tathmini ambazo... Huwa nataka kulia kila ninapozisoma. Huwa wanasema mambo mazuri juu yangu na nyumba yangu, hilo hunipa hisia nzuri kweli.

Umeshawahi kuwa na wageni waliozidi matarajio yako?

Wengi wao, kwa sababu wanaiacha nyumba ikiwa nadhifu, kwa mfano wakati mwingine wao hutengeneza kitanda. Ni kama wao ni wanafamilia au marafiki. Ikiwa wamevunja kitu, wataniambia, "Samahani nimevunja glasi" ama kitu kama hicho. Sijawahi kukosa kitu nyumbani kwangu. Vifaa vyangu. Vitabu vyangu. Huwa ninaacha kila kitu hapa.

Simulizi zingine za wenyeji

Anza kutayarisha tangazo lako