TAKRIMA

Mwenyeji anashiriki sanaa na utamaduni wa Mexico kupitia Airbnb iliyojengwa ndani ya mungu nyoka wa Azteki

Kwa mwenyeji Patricia, Kiota cha Quetzalcoatl sio tu ni mahali pazuri pa kukaa; lakini pia ni daraja kati ya watu na tamaduni

Uso wa Patricia unajaa changamko anapokumbuka utoto wake, akicheza na watoto wengine kwenye vilima karibu na Naucalpan de Juarez, eneo lenye misitu lililo magharibi mwa Mexico City ambalo limejaa mapango, lililopambwa na mito iliyochimbwa na mifereji, lililojaa wanyama pori. Sasa, kwa fahari hutumika kama mwongoza watalii na mwenyeji wa kipande cha Naucalpan ambacho kimehifadhiwa na kubadilishwa sana kuwa jamii ya kipekee kama kumbukumbu ya sanaa na utamaduni wa Mexico. "Ninapenda kushiriki mahali hapa kwa sababu ninajivunia," Patricia anasema. "Sitaki kuwa nayo mwenyewe, au kwa ajili ya majirani zangu tu. Nadhani ni jambo linalostahili kuonwa na kulihisi na kuliishi. " Kushiriki kona inayopendwa ya ulimwengu na wengine ni motisha ambayo inaunganisha wenyeji mbalimbali wa Airbnb. Ni wachache wanaoshiriki mahali penye uzuri kama huo wa Kiota cha Patricia Quetzalcoatl. Ikipewa jina la mungu ambaye ni -nusu-ndege-nusu-nyoka anayeheshimiwa na Waazteki, ni mchanganyiko wa bustani nzuri na eneo la makazi lililojengwa ndani ya sanamu kubwa, iliyopambwa vizuri, yenye rangi kali ambayo hutoka nje na kuingia ndani ya uwanja. Ni kitu cha thamani kilichosanifiwa na Javier Senosiain, mbunifu wa Mexico ambaye alianzisha mtindo huu mzuri wa "usanifu wa majengo hai". Nyumba ya Patricia ni moja kati ya 10 kwenye eneo hili la makazi na ndio pekee inayopatikana kwenye Airbnb. Ni fleti yenye nafasi ya vyumba vya kulala 5 na madirisha mviringo, dari zilizochongwa, na vifaa vingine vya usanifu vilivyojengwa ndani ya tumbo la nyoka. Mapambo ya kisasa inafanya mahali hapa pawe na mzunguko mzuri wa hewa ambako kunaendana na mazingira yake mazuri.

"Sitaki kuwa nayo mwenyewe, au kwa ajili ya majirani zangu tu. Nadhani ni jambo linalostahili kuonwa na kulihisi na kuliishi. "

Patricia, Kiota cha Quetzalcoatl

"Sitaki kuwa nayo mwenyewe, au kwa ajili ya majirani zangu tu. Nadhani ni jambo linalostahili kuonwa na kulihisi na kuliishi. "

Patricia, Kiota cha Quetzalcoatl

Wazo la kuwa mwenyeji wa muda mrefu lilikuja kwa Patricia kutoka kwa mmoja wa dada zake, ambaye hapo awali alikuwa ameorodhesha nyumba kwenye Airbnb. Na iliambatana na hamu ya Patricia ya kuondoka katika pilika pilika za Jiji la Mexico kwenda mahali ambayo ni kijani na tulivu. Tangu 2015, amekubaliana na jukumu lake kwa bidii moja. Patricia kawaida hupokea wageni mwenyewe na kuwaongoza kuelekea kwenye nyumba yake kupitia uwazi pembezoni mwa nyoka. Yeye hufurahia maneno ya mshangao kutoka kwa wageni katika lugha mbalimbali kadiri wanavyoyazoea mazingira yao- "wows" na "oohs" na "ooh la las." "Ingawa wameona picha, hawatarajii ukubwa wa jumba na mazingira yanayoizunguka, ukimya, na amani watakayohisi," anasema. Patricia anapenda kuwatembeza wageni wake katika ziara ya nyumba hiyo. Na kwa wengi, inakuwa moja ya mambo muhimu ya kukaa kwao kwenye Kiota cha Quetzalcoatl. Ziara hiyo inaweza kugeuka kuwa tukio la hadi saa 3 hadi 4 ikiwa wageni watataka. Kuna mengi ya kuona katika shamba la karibu ekari 40 ambalo limepambwa kwa sehemu na sehemu nyingine iko katika hali ya asili. Na kasi ya Patricia ni kidogo kidogo. Ataonyesha kinywa cha nyoka kilichojengwa karibu na pango la asili, akihimiza wageni wachunguze maua na miti tofauti, angalia rangi safi ya majani, sauti za msitu, na mitindo yote tofauti, ya asili na ya kutengenezwa. "Wakati mwingine huwaalika watembee bila viatu kwenye nyasi na kuihisi sehemu hii," anasema.

Katika kila ziara, atazungumzia kuhusu Huichol, watu asilia kutoka milima ya kati ya Mexico, ambao hujulikana kwa vito vyao vya kupendeza na sanaa ya shanga. "Kichwa cha nyoka kinatengenezwa na ushawishi mwingi wa Huichol," Patricia anasema. Maduara ya kauri yenye kuzungushwa katika kichwa, macho, meno ya nyoka, pamoja na maelezo mengine mengi ya jengo zuri la Senosiain, hutiwa msukumo na sanaa ya Huichol. "Mojawapo ya vitu ambavyo tulitaka kuweka alama mahali hapa ni rangi ya Mexico," anaongeza Patricia. Patricia pia hufundisha wageni kuhusu mimea ya dawa kwenye nyumba hii na matumizi yake na watu wa Huichol na wengineo. Ikiwa anahisi wageni wanapendelea, anaweza kuwaalika wajiunge naye katika kutafakari mwishoni mwa safari. Mwishowe, kinachomsukuma ni hamu ya kushiriki sanaa, utamaduni, na uzuri wa asili wa Mexico, pamoja na uzoefu na unganisho la kibinadamu. "Nimegundua kuwa ingawa wageni wangu wanaweza kuwa Wachina, Wamexico, Wahispania, Waaustralia au kitu kingine chochote, sote tuna hisia, sote tunapenda, sote ni wanadamu," anasema. Watu wanaweza kuonekana tofauti, anaongeza, "lakini kwa ndani, tunafanana sana." Ana matumaini kupitia kujikita kwao katika asili, tamaduni ya Mexico, na kukaa kwao ndani ya Kiota cha Quetzalcoatl, wageni wake wataondoka wakiwa na badiliko. "Ninachopenda juu ya kukaribisha wageni na kuwasiliana na wageni wangu ni kwamba wasiwe na safari tu, lakini wawe na uzoefu, na uzoefu huo ni muhimu sana kwao," anasema. "Wakati wa likizo ni kama kila kitu kinasimama, na ningependa kushiriki kusimama huko nao kwa kuingia ndani yao na kugundua wanachotaka, na wao ni kina nani."

Kuwa mwenyeji leo