MAPATO YA KUKARIBISHA WAGENI

Kurahisisha umiliki wa nyumba

Kuna sababu nyingi kwa nini watu wanaanza kukaribisha wageni kwenye Airbnb-kuanzia kulipa bili hadi kukutana na watu wapya. Lakini kuna idadi inayokua ya wenyeji ambao wamegundua njia ya kumiliki nyumba kwa kushiriki mahali pao. Tim, mtengeneza filamu wa kujitegemea kutoka Seattle, alibadilisha sehemu ya chini kuwa tangazo maarufu la Airbnb Seattle. Kabla ya Tim kuorodhesha mahali pake Airbnb, alikuwa anajitahidi kukidhi mahitaji yake kwenye jiji lenye gharama kubwa ya maisha. Tim ansema, "Nikiwa mtu katika tasnia ya ubunifu, mapato yangu yanaweza kutofautiana sana mwaka hadi mwaka," anasema Tim, "kwa hivyo mimi na rafiki yangu wa kike tunajaribu kuishi maisha ya wastani." Tim aliona kuwekeza katika nyumba kungemsaidia kuwa na bajeti endelevu zaidi mbeleni. Lakini alipoanza utaftaji wa nyumba, mara moja alikabiliwa na ukweli wa kuvunja moyo: nyumba nyingi zilikuwa juu zaidi ya uwezo wake, au zilihitaji matengenezo ya maelfu ya dola. Hakuona njia ya kusonga mbele.

Hatungekuwa na nyumba kama si Airbnb. "

Tim, mwana Seattle wa muda mrefu

Hatungekuwa na nyumba kama si Airbnb. "

Tim, mwana Seattle wa muda mrefu

Baada ya utaftaji wa kina, mwishowe Tim alipata nyumba ya aina aliyokuwa akitafuta. Ni nini kilifanya nyumba ya Tim iwe nzuri? Sehemu ya chini ya ardhi ambayo haijakamilika aliiona ikigeuka kuwa tangazo la Airbnb. "Rafiki zetu wengine hutumia Airbnb, na tulitaka kuwa na uwezo wa kushiriki nafasi katika nyumba yetu mpya kusaidia kufidia gharama," Tim anasema. "Kwa hivyo nilipoona sehemu hii ya chini ya ardhi, nilijua ingefanya mradi mzuri kubadilisha kuwa tangazo la Airbnb." Kwa kufanya ujenzi mwenyewe, akabadilisha sehemu ya chini ya nyumba yake mpya kuwa moja ya matangazo maarufu zaidi ya Airbnb katika jamii yake. Kama mmiliki mpya wa nyumba, Tim anafafanua, "Tangazo langu la Airbnb linachangia theluthi moja ya mkopo wangu wa nyumba," akiendelea kusema, "Tungekuwa tumekosa kumiliki nyumba kama si kwa ajili ya Airbnb."

Gundua kiasi unachoweza kupata

Unataka kujua zaidi kuhusu kukaribisha wageni?