Mwenyeji Bingwa:Kuwatambua wenyeji bora

Mpango wa Mwenyeji Bingwa unawaenzi na kuwatuza wenyeji wa Airbnb wenye ukadiriaji wa juu na wenye uzoefu mkubwa.
Angalia maendeleo yako

Faida za Mwenyeji Bingwa

Kama Mwenyeji Bingwa, utaonekana zaidi, utapata usaidizi mahususi na zawadi za kipekee. Ni njia yetu ya kusema asante kwa ukarimu wako wa kipekee.

Utambuzi maalumu

Beji ya Mwenyeji Bingwa hukusaidia kuonekana zaidi na inaweza kusababisha kuwekewa nafasi zaidi.

Usaidizi wa kipaumbele

Kama Mwenyeji Bingwa, utapokea usaidizi wa kipaumbele unapowasiliana na Airbnb Usaidizi.

Zawadi za kipekee

Kila unapofikia robo nne mfululizo kama Mwenyeji Bingwa, unapata kuponi ya USD 100 ya kutumia kwenye Airbnb. Pia unapata 20% ya ziada pamoja na bonasi ya mwalikwa.

Kinachomfanya mtu awe Mwenyeji Bingwa

Kila baada ya miezi mitatu, tunaangalia iwapo umetimiza vigezo hivi kwa mwaka uliopita. Ikiwa umefanya hivyo utapata au kudumisha hadhi yako ya Mwenyeji Bingwa.

Ukaaji mara 10 na zaidi

Kamilisha angalau ukaaji mara 10 ndani ya mwaka au usiku 100 kwa ukaaji mara tatu au zaidi uliokamilika. Wageni wako wanaweza kuhisi kuwa wanakaa kwa mwenyeji mzoefu.

Kiwango cha kughairi kilicho chini ya asilimia 1

Ghairi chini ya asilimia 1 ya wakati, bila kujumuisha matukio makubwa yenye kuvuruga. Hii inamaanisha ughairi 0 kwa wenyeji waliowekewa nafasi zilizo chini ya 100 kwa mwaka. Ughairi nadra unamaanisha utulivu wa akili kwa wageni wako.

Ukadiriaji wa jumla wa 4.8

Dumisha ukadiriaji wa 4.8 au zaidi kulingana na tathmini kutoka kwa wageni wako mwaka uliopita. Wageni wanatarajia ukarimu wa hali ya juu kutoka kwa wenyeji kama wewe.

Kiwango cha kutoa majibu cha asilimia 90

Jibu asilimia 90 ya ujumbe mpya na ukubali au ukatae maombi ya kuweka nafasi, ndani ya saa 24. Kwa njia hiyo, wageni wanajua utajibu kwa wakati maulizo mapya.

Majibu kwa maswali yako

Pata ushauri kutoka kwa Wenyeji Bingwa

Wanawake wawili wameegemea nje ya dirisha lililo wazi la nyumba ya Airbnb huku wakishikana mikono na kutabasamu