Kukaribisha wageni kwenye Airbnb
  Unda ukaaji wa kuridhisha na upate tathmini bora

Ni nini kinachotarajiwa kutoka kwa wenyeji?

Tungependa kukupa mwongozo wazi ili ujue kinachotarajiwa na kinaweza kukupa nyota 5 kila unaposhiriki nyumba yako.
Sisi huwaomba wenyeji wetu wote kutimiza mahitaji manne ya msingi: kiwango cha jumla, kiwango cha kutoa majibu, ughairishaji na kukubalika kwa uwekaji nafasi. Zaidi ya misingi, pia utatathminiwa na wageni wanaokaa na wewe.
Wewe tayari ni mwenyeji? Tazama kuendelea kwako ili ufahamu unavyoendelea.

Mahitaji ya msingi

Ili kusaidia kuunda ukaaji wa kuridhisha, wa kutegemewa wa wageni wote, ni lazima nyumba na wenyeji wote watimize mahitaji manne ya msingi.
Toa majibu
Kujibu haraka wageni wanapowasiliana nawe huonyesha kuwa wewe ni mwenyeji aliye mwangalifu na mwenye busara. Jinsi unavyojibu maombi ya kuweka nafasi na maulizo ya kuweka nafasi mara kwa mara na kwa haraka hupimwa kwa kiwango chako cha kutoa majibu. Sisi huwaomba wenyeji kujibu maswali ya aina hizi ndani ya saa 24.
Kubali maombi ya kuweka nafasi
Hakuna mgeni anayependa kutuma maombi 4 au 5 ili kupata nafasi hivyo tunatarajia kuwa iwapo kalenda yako inaonyesha kuwa uko huru, ukubali maombi mengi. Hakikisha kuwa kalenda ya tangazo lako inaonyesha siku ambazo unaweza kukaribisha wageni. Kwa njia hii una uwezekano mkubwa wa kupata maombi ya kuweka nafasi ambayo kwa kweli unaweza kuyashughulikia. Unaweza kutumia mipangilio yako ya upatikanaji ili kuficha muda usiofanya kazi kati ya uwekaji nafasi, au kuzuia maombi ya uwekaji nafasi wa siku hiyo hiyo au uwekaji nafasi wa siku za usoni zilizo mbali sana.
Epuka kughairishia wageni
Tunachukulia ughairishaji kwa uzito na kuwaomba wenyeji wote kujiepusha na ughairishaji kwa wageni –mipango yao ya usafiri huitegemea! Utakuwa chini ya adhabu, ikiwa ni pamoja na adhabu za kifedha, ikiwa utaghairi uwekaji nafasi uliothibitishwa. Tunaomba kuwa ujiepushe na kughairi uwekaji nafasi uliothibitishwa isipokuwa iwapo kuna sababu zisizozuilika.
Pata tathmini chanya
Wageni hupenda kujua kuwa wanaweza kutarajia kiwango thabiti cha ubora, bila kujali wanakoweka nafasi. Mwishoni mwa kila ukaaji, wageni watatathmini tukio lao na wewe, ambayo ni mojawapo ya njia za kukutathmini kama mwenyeji. Kiwango chako cha jumla ni alama ya tathmini yako ya wastani kutoka kwa wageni wote uliokaribisha.
Kama mwenyeji, utakuwa na fursa ya kuwapa kiwango wageni –kuhusu usafi wao, heshima na mawasiliano. Maoni yako hutusaidia kuhakikisha kuwa wageni wanashughulikia nyumba wanazokaa kama ambazo ni zao. Wageni ambao hushtakiwa mara kwa mara na wenyeji huenda wakawa chini ya adhabu.

Kupata tathmini nzuri kutoka kwa wageni

Tumegundua kwamba wenyeji ambao hupata tathmini bora hulenga mambo matano: usafi, vistawishi muhimu, maelezo sahihi ya tangazo, uingiaji usio na tatizo, na mawasiliano ya usuluhishaji wa mapema.

Usafi

Wageni watatarajia sehemu safi na nadhifu ambayo huwa wanaona katika picha zako za tangazo. Hakikisha kuwa unajipa muda wa kutosha wa kusafisha kati ya mgeni mmoja hadi mwingine, hasa unapokuwa na uwekaji nafasi unaofuatana.
Wageni watakuwa na nafasi ya kuupa kiwango usafi wa sehemu yako, na kiwango cha wastani cha viwango vyako kitaonekana kwenye ukurasa wako wa tangazo. Ikiwa unapokea mara kwa mara viwango vya chini vya usafi, huenda ukawa chini ya adhabu.
KINACHOTARAJIWA
 • Osha kila chumba ambacho wageni wanaweza kufikia, hasa vyumba vya kulala, mabafu na jikoni
 • Hakikisha kwamba hakuna nywele, vumbi, au ukungu kwenye sehemu tofauti na sakafu
 • Hesabu mapato kati ya kila ukaaji:
 • Toa vitani safi /shuka na taulo za wageni
 • Ondoa takataka, chakula, na vifaa vilivyobaki kutoka kwa wageni wa hapo awali
VIDOKEZI
 • Hakikisha kuna nafasi kati ya uwekaji nafasi wako ili kukupa muda zaidi wa kujitayarisha kati ya mgeni mmoja hadi mwingine. Unaweza kusasisha mapendekezo yako ya uwekaji nafasi ili kuziba usiku mmoja au mbili kabla ya uwekaji nafasi
 • Toza ada ya usafi na utumie pesa za ziada kulipia bidhaa za usafi au uajiri huduma ya kitaaluma ya usafi
 • Acha bidhaa za kusafisha katika sehemu yako ili wageni wako waweze kushughulikia uchafu unaomwagika na usiokusudiwa

Vistawishi muhimu

Tunapendekeza kuwa wenyeji wote watoe vistawishi muhimu ili wageni wapate wanachohitaji ili kuridhika na kuwa na mapumziko mazuri ya usiku.
 • Karatasi ya chooni
 • Sabuni
 • Vitani / shuka
 • Angalau taulo moja kwa kila mgeni aliyewekewa nafasi
 • Angalau mto mmoja kwa kila mgeni aliyewekewa nafasi

Maelezo ya tangazo yaliyo sahihi

Kuweka matarajio sahihi kabla ya safari kunaweza kuchangia tukio bora zaidi kwako na pia kwa wageni wako. Unaweza kuwasaidia wasafiri kuamua sehemu yako inatimiza mahitaji yao kwa kutoa taarifa ya uwazi na ni lazima wajue iwapo wewe hukubali wanyama vipenzi. Tangazo la kina na wasifu husaidia kuwavutia wageni wanaotafuta eneo linalofanana tu na lako.
Wageni watakuwa na fursa ya kupima usahihi wa taarifa unayotoa.
TAARIFA YA TANGAZO
KINACHOTARAJIWA
 • Anwani sahihi na inayosasishwa mara kwa mara (Tutaishiriki tu baada ya mgeni kuweka nafasi)
 • Maelezo ya faragha ya chumba cha kulala na bafu ni sahihi
 • Kutangaza picha vizuri huonyesha hali na mpangilio wa sehemu yako
 • Vistawishi viko vile vimetangazwa, vilivyopo na vinavyofanya kazi
VIDOKEZI
 • Tumia pichambalimbali za ubora wa hali ya juu zilizo na maelezo mafupi na uandike maelezo ya kina ya sehemu
 • Toa Sheria za Nyumba ambazo hushughulikia hali ambazo zitakuwa za maana kwa wageni wako. Sheria zako zinaweza kutoa maelezo ya uwazi kuhusu kile ufanyacho na usichoruhusu, kama vile uvutaji sigara, wanyama vipenzi, au wageni wa ziada.
 • Wajulishe wageni ikiwa kuna sehemu za tangazo zilizopigwa marufuku, kama vile gereji au darini
 • Kuwa mwaminifu kuhusu vipengele ambavyo vitaathiri ukaaji wa mgeni wako. Wageni wako wanastahili kujua iwapo majirani wako walianza tu mradi wa ujenzi wenye kelele au ikiwa watahitaji kupanda ngazi 8 ili kufika kwenye eneo lako.
VISTAWISHI
Tangaza vistawishi vyote unavyotoa na uhakikishe kuwa kila kimoja kinapatikana na kiko katika hali nzuri
BEI YA KILA USIKU
Hakikisha kuwa sehemu yako inafanana na bei uliyoweka. Bei ya juu sana inaweza kuwafanya wasafiri kuchukulia kuwa tangazo lako ni la starehe zaidi. Unahitaji msaada? Jaribu kutazama matangazo mengine katika eneo lako au uwashe Upangaji bei Kiotomatiki.

Kuingia kulio rahisi

Mfumo wa uwazi na rahisi wa kuingia utawasaidia wageni wako kuwa na utulivu baada ya siku ya kusafiri. Wageni wataombwa kulipa kiwango tukio lao la kuingia mwishoni mwa ukaaji wao.
VIDOKEZI
 • Tengeneza mwongozo wa kuingia wa tangazo lako–tutaushiriki na wageni wako saa 24 kabla ya kuingia ili wawe na kila wanachohitaji ili kuwasili bila tatizo
 • Ikiwa unapanga kukutana na wageni wewe binafsi, hakikisha kuwa umeratibu muda wa kuingia mapema
 • Iwapo unatoa huduma ya uingiaji mwenyewe, weka maelezo hayo katika kitengo cha Rasilimali ya wageni kwenye tangazo lako
 • Hakikisha kuwa wageni wako wanajua jinsi ya kuwasiliana nawe iwapo wana kuchelewa kwa usafiri au swali la dakika za mwisho
 • Wape wageni wako maelekezo ya kina ya kufika kwenye eneo —unaweza kuokoa muda kwa kuweka yote katika mwongozo wa nyumba yako

Kuwasaidia wageni wakati wa ukaaji wao

Uwe unaishi katika sehemu sawa na wageni wako au la, ni muhimu kupatikana katika ukaaji wao wote. Wageni wako watakuwa na fursa ya kuupa kiwango uwazi na uthabiti wa mawasiliano yako mwishoni mwa ukaaji —na kiwango cha wastani cha viwango hivi kitaonekana kwenye ukurasa wa tangazo lako.
VIDOKEZI
 • Shughulika mapema katika mawasiliano yako ili wageni wajue kuwa unapatikana. Wasiliana mapema ili kuratibu mipango ya kuwasili. Ikiwa hutakuwa ukiwasalimu wageni wako watakapokuwa wakiwasili, unaweza kuwatumia ujumbe wakati wao wa kuingia ili kuhakikisha kila kitu kiliendelea vyema.
 • Ikiwa utathibitisha uwekaji nafasi na jambo fulani kuhusu tangazo lako libadilike, mjulishe mgeni wako mapema.
 • Pakua programu ya Airbnb ili uweze kujibu ujumbe popote.
 • Ikiwa hutakuwa katika eneo hilo wakati wa ukaaji wao, unaweza kuwapa wageni mkazi wa kuwasiliana nao.