Masharti ya kisheria
Matumizi ya kamera na vifaa vya kurekodi
Matumizi ya kamera na vifaa vya kurekodi
Kusaidia kuwapatia Wenyeji na wageni utulivu wa akili, hatua za usalama kama kamera za usalama na vifaa vya ufuatiliaji kelele vinaruhusiwa, maadamu vinafichuliwa wazi katika maelezo ya tangazo na havikiuki faragha ya mtu mwingine. Sheria kuhusu vifaa zinahusu kamera zote, vifaa vya kurekodia, vifaa janja na vifaa vya kufuatilia.
Kile tunachoruhusu
- Vifaa vilivyofichuliwa vinavyofuatilia sehemu za umma na sehemu za pamoja: Vifaa vinavyoruhusu kutazama au kufuatilia sehemu ya umma pekee (mfano: mlango wa mbele, au njia ya kuendesha gari) au sehemu ya pamoja ambavyo vimetambuliwa wazi na kufichuliwa kabla ya kuweka nafasi vinaruhusiwa. Sehemu za pamoja hazijumuishi maeneo ya kulala au bafu.
Kile ambacho haturuhusu
- Vifaa vilivyofichwa na visivyojulikana vinavyofuatilia sehemu ya pamoja: Kifaa chochote kinachofuatilia sehemu ya pamoja kinapaswa kuwekwa katika eneo linaloonekana na kuelezwa katika maelezo ya tangazo.
- Vifaa vilivyo ndani au vinavyofuatilia sehemu za kujitegemea: Vifaa havipaswi kufuatilia sehemu za kujitegemea (kwa mfano: vyumba vya kulala, mabafu, au sehemu za pamoja ambazo zinatumika kama maeneo ya kulala, kama vile sebule yenye kitanda cha sofa). Vifaa ambavyo havijaunganishwa vinaruhusiwa maadamu vimezimwa na kufichuliwa kwa wageni.
- Vifaa vya kurekodia katika nyumba nzima au fleti (China Bara pekee): Kamera na vifaa vya kurekodia haviruhusiwi kwenye nyumba nzima au fleti isipokuwa kama vimebainishwa waziwazi na kufichuliwa katika sehemu za pamoja za sehemu ya kukaa iliyobainishwa kama "risoti," "kasri," au "villa." Pata maelezo zaidi kuhusu sheria hizi katika China Bara.
Tuko hapa kukusaidia
Ikiwa wewe au mtu mwingine anahisi kutishiwa au hayuko salama, tafadhali kwanza wasiliana na mamlaka za utekelezaji wa sheria za eneo husika ili kupata usaidizi. Aidha, ikiwa unashuhudia au unapitia uzoefu wa tabia ambayo inakwenda kinyume cha sera zetu, tafadhali tujulishe.
Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa ili kutoa mwongozo wa jumla kwa sera za jumuiya za Airbnb.
Makala yanayohusiana
- Sera ya jumuiya•MgeniKulinda faragha yakoIli kuunda mazingira ambayo yanakuza si tu usalama wa kimwili pekee, bali pia usalama na ulinzi wa taarifa binafsi, tabia na shughuli fulani…
- ImestaafishwaRetired article 887: What are Airbnb’s rules about security cameras and other recording devices in listings?All members of the Airbnb community are required to respect each other’s privacy. Hosts should disclose all recording devices in their listi…
- Masharti ya kisheriaKamera na vifaa vya kurekodi huko China BaraPata sheria zinazotumika mahususi kwa China Bara kuhusu kamera za usalama na vifaa vingine vya kurekodi.