Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya
Mwenyeji

Makufuli ya chumba cha kulala na bafu kwa ajili ya tangazo lako la Chumba

Wageni wanatarajia kwamba watakuwa na chaguo la kufunga chumba chao cha kulala au bafu lolote wanaloweza kufikia. Tunapendekeza sana uweke kufuli kwenye vyumba vyovyote vya kulala na mabafu ambayo wageni wanaweza kutumia.

Kusasisha taarifa za kufuli kwa ajili ya tangazo lako la Chumba

Ikiwa sehemu yako tayari ina makufuli kwenye vyumba vya kulala na bafuni, hakikisha unabadilisha maelezo ya tangazo lako. Unaweza kusasisha taarifa za kufuli za chumba cha kulala kwa tangazo la Chumba kwa kufungua mipangilio ya tangazo lako, kisha uende kwenye Maelezo ya tangazo, ukabofya sehemu ya Vyumba na Sehemu, kisha uchague chumba cha kulala ambapo ungependa kuweka taarifa za kufuli.

Aina za kufuli zilizopendekezwa

Makufuli ya chumbani

Wageni wanapaswa kuwa na uwezo wa kufunga mlango wa chumba cha kulala kwa ndani (kwa sababu ya faragha yao) na kwa nje (kwa sababu ya usalama wa mali zao). Inapendekezwa kufuli yenye ufunguo, iliyounganishwa na komeo la ndani.

Makufuli ya bafuni

Kwa mabafu ambayo wageni wanaweza kufikia, wageni wanapaswa kuweza kufunga au kubana mlango wa bafuni kwa faragha.

Mambo ya kuzingatia kuhusu funguo na vicharazio

Aina yoyote ya kufuli au komeo utakayochagua, zingatia kufuata mazoea haya bora:

  • Ikiwa kuna Vyumba vingi katika tangazo moja vinavyotumia vicharazio, kila msimbo unapaswa kuwa wa kipekee. Vivyo hivyo, ikiwa kuna Vyumba vingi vyenye kufuli za nje ambazo zinazofunguliwa kwa ufunguo, kufuli na funguo zinapaswa kuwa za kipekee.
  • Ikiwa unatumia kicharazio cha kidijitali, msimbo haupaswi kuwekwa ndani ya tangazo ambapo wengine wanaweza kuupata. Vivyo hivyo, ikiwa kuna funguo mbili za Chumba, zinapaswa kuhifadhiwa mahali salama na funguo hazipaswi kuachwa katika sehemu ya pamoja au ambapo watu wasioidhinishwa wanaweza kuzipata.

Kabla ya kuweka kufuli, hakikisha unaangalia sheria za eneo husika na vizuizi vingine ambavyo vinaweza kutumika kuweka kufuli kwenye sehemu yako, kama vile mahitaji kuhusu aina za kufuli ambazo unaweza kuweka au vibali unavyohitaji.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili