Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sera ya jumuiya

Matumizi na ufichuzi wa kamera za usalama, vifaa vya kurekodi, vifuatiliaji vya kiwango cha sauti na vifaa janja vya nyumbani

Haturuhusu Wenyeji wawe na kamera za usalama au vifaa vya kurekodi vinavyofuatilia sehemu za ndani, hata ikiwa vifaa hivi vimezimwa. Kamera zilizofichwa zimepigwa marufuku kila wakati na zitaendelea kupigwa marufuku. Wenyeji wanaruhusiwa kuwa na kamera za usalama za nje, vifuatiliaji vya kiwango cha sauti na vifaa mahiri ili mradi wazingatie miongozo ifuatayo na sheria zinazotumika.

Sheria hizi zinaanza kutumika tarehe 30 Aprili, 2024.

Kamera za usalama na vifaa vya kurekodi

  • Kamera za usalama na vifaa vya kurekodia ni kifaa chochote ambacho kinarekodi au kusambaza video, picha au sauti kama vile kifuatiliaji cha mtoto au kamera ya kengele ya mlangoni.
  • Kamera za usalama zilizofichwa zimepigwa marufuku kabisa.
  • Wenyeji hawaruhusiwi kuwa na kamera za usalama na vifaa vya kurekodia ambavyo vinafuatilia sehemu yoyote ya ndani ya nyumba, kama vile korido, bafu, sebule au nyumba ya mgeni, hata kama vimeziwa au havijaunganishwa. Makatazo hayo pia yanatumika kwenye maeneo ya pamoja na sehemu za pamoja kwenye nyumba zenye vyumba vya kujitegemea (mf. sebule)
    • Kwa baadhi ya matangazo nchini Japani yenye Leseni ya Biashara ya Hoteli, Wenyeji wanaweza kutakiwa na sheria inayotumika kuwa na kamera ambayo inafuatilia njia ya kuingia ndani kwenye nyumba hiyo pekee. Kamera hizo lazima zionyeshwe kwa wageni, haziruhusiwi kufuatilia sehemu yoyote ya tangazo nje ya njia ya kuingia na haziruhusiwi kurekodi sauti.
  • Wenyeji hawaruhusiwi kuweka kamera za usalama na vifaa vya kurekodia kwenye maeneo ya nje kwenye nyumba ambapo watumiaji wana matarajio makubwa ya faragha, kama vile ndani ya bafu la nje lililofungwa au kwenye sauna.
  • Wenyeji wanaruhusiwa kuwa na kamera za usalama za nje na vifaa vya kurekodia na wanatakiwa kuhakikisha kuwa mahali vilipo pamewekwa wazi kwenye maelezo ya tangazo (mf: “Nina kamera kwenye ua wangu wa mbele,” “Nina kamera kwenye baraza langu,” “Nina kamera kwenye bwawa langu” au “Nina kamera ya kengele ya mlangoni inayofuatilia mlango wangu wa mbele na korido ya jengo langu la fleti.”)
  • Wenyeji wanatakiwa kuweka wazi kuhusu kamera za usalama za nje na vifaa vya kurekodia wanavyosimamia, kama vile korido ya jengo lao la fleti au kwenye ua wao.

Vifuatiliaji vya kiwango cha sauti

  • Vifuatiliaji vya kiwango cha sauti ni vifaa vinavyotathmini viwango vya sauti na muda wake lakini havirekodi sauti.
  • Wenyeji wanaruhusiwa kuwa na vifuatiliaji vya kiwango cha sauti ndani ya nyumba yao ili mradi Mwenyeji ataweka wazi kwamba vifaa hivyo vipo na havipo kwenye vyumba vya kulala, mabafu au sehemu za kulala. Wenyeji hawahitajiki kuweka wazi kuhusu mahali vilipo vifuatiliaji vyao vya kiwango cha sauti.

Vifaa vya nyumba mahiri

  • Vifaa vya nyumba mahiri vinavyounganisha na kuingiliana na vifaa au mitandao mingine, kama vile Alexa ya Amazon na Nest ya Google.
  • Wenyeji wanaruhusiwa kuwa na vifaa janja vya nyumbani.
  • Wenyeji wanahimizwa, lakini si lazima, waweke wazi kuhusu uwepo wa vifaa hivyo nyumbani kwao. Pia tunawahimiza Wenyeji wawape wageni chaguo la kuondoa au kulemaza vifaa janja.

Weka wazi kamera yako ya usalama au kifaa cha kurekodi

  1. Bofya Matangazo kisha uchague tangazo unalotaka kuhariri
  2. Chini ya Kihariri tangazo, bofya Sehemu yako
  3. Bofya Usalama wa mgeni
  4. Bofya Vifaa vya usalama, kisha ubofye Kamera za usalama au vifaa vya kurekodi sauti vilivyopo
  5. Bofya Weka maelezo na uelezee kila kifaa cha nje, mahali kilipo (k.m: “Nina kamera ya kengele ya mlangoni inayofuatilia mlango wangu wa mbele na korido ya jengo la fleti yangu”), na endapo kitazimwa au kuwashwa
  6. Bofya Endelea kisha Hifadhi

Onyesha vifuatiliaji vyako vya kiwango cha sauti

  1. Bofya Matangazo kisha uchague matangazo unayotaka kuhariri
  2. Chini ya Kihariri tangazo, bofya Sehemu yako
  3. Bofya Usalama wa mgeni
  4. Bofya Vifaa vya usalama, kisha ubofye Kamera za usalama au vifaa vya kurekodi sauti vilivyopo
  5. Bofya Vifuatiliaji vya kiwango cha sauti kisha ubofye Hifadhi
Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili