Ruka kwenda kwenye maudhui
  Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Habari za hivi punde kuhusu COVID-19
  Ili upate machaguo ya kughairi na kurejesha fedha, chagua nafasi iliyowekwa kwenye ukurasa wa Safari. Sera yetu ya sababu zisizozuilika inatumika tu kwenye nafasi fulani zilizowekwa. Ikiwa tarehe yako ya kuingia ni baada ya tarehe 15 Septemba, rudi hapa tena tarehe 15 Agosti, 2020 ili kupata habari za hivi punde.

  Je, ni mahitaji gani yanayohitajika ili kuweka nafasi kwenye Airbnb?

  Tunamwomba kila mtu anayetumia Airbnb kutupa taarifa chache kabla ya kuweka nafasi kwenye Airbnb. Wageni hutakiwa kujaza taarifa hizi kikamilifu kabla ya kutuma ombi la kuweka nafasi. Taarifa hizi husaidia wenyeji kuhakikisha kuwa wanajua ni nani wanatarajia, na jinsi ya kuwasiliana na mgeni.

  Mahitaji ya Airbnb kwa wageni ni pamoja na:

  • Jina kamili
  • Anwani ya barua pepe
  • Nambari ya simu iliyothibitishwa
  • Ujumbe wa utangulizi
  • Makubaliano ya sheria za nyumba
  • Taarifa ya malipo

  Wageni wanahimizwa, lakini sio lazima, kuwa na picha ya wasifu. Wenyeji hawataona anwani halisi za barua pepe za wageni, hata baada ya kuweka nafasi. Badala yake, wenyeji wataona anwani ya barua pepe ya Airbnb ya muda mfupi inayowasilisha ujumbe wao kwa mgeni.

  Baadhi ya wenyeji wanaweza pia kuwauliza wageni kutoa kitambulisho kabla ya kuwekea nafasi sehemu yao.

  Makala yanayohusiana
  Ulipata msaada uliohitaji?