Pata pesa kwa kukaribisha wageni kwenye hema

Jua kiasi unachoweza kupata

Pata pesa kwa kukaribisha wageni kwenye hema

Jua kiasi unachoweza kupata

Karibisha wageni katika hema kwenye Airbnb

Mahema ni majengo yaliyotengenezwa kwa kitambaa na miti ambayo kwa kawaida hubebeka na kukunjika. Kukaribisha wageni katika hema kwenye Airbnb huwapatia wageni wako fursa ya kukaa kwa starehe na kupata uzoefu wa kijasura katika maeneo ya wazi.

Airbnb ni nini?

Airbnb huwaunganisha watu na sehemu za kukaa na mambo ya kufanya duniani kote. Jumuiya hii huendeshwa na wenyeji, ambao huwapa wageni wao fursa ya kipekee ya kusafiri kama mkazi.

Kwa nini ukaribishe wageni kwenye Airbnb?

Airbnb hufanya iwe rahisi na salama kuwakaribisha wasafiri. Una udhibiti kamili juu ya upatikanaji, bei, sheria za nyumba na jinsi unavyoingiliana na wageni.

Tupo nyuma yako

Ili kulinda usalama wako, wa nyumba na mali zako, tuna bima ya USD Milioni 1 ya kulinda kila nafasi iliyowekwa dhidi ya uharibifu wa mali na bima nyingine ya USD Milioni 1 dhidi ya ajali.

Kukaribisha wageni katika hatua 3

Tangaza sehemu yako bila malipo

Shiriki sehemu yoyote bila malipo ya kujisajili, kuanzia nyumba ya kulala wageni hadi banda na sehemu nyingine mbalimbali.

Chagua jinsi unavyotaka kukaribisha wageni

Chagua ratiba yako mwenyewe, bei na matakwa kwa ajili ya wageni. Tuko tayari kukusaidia mpaka mwisho.

Mkaribishe mgeni wako wa kwanza

Mara tangazo lako litakapoanza kuonekana mtandaoni, wageni wanaostahiki wanaweza kuwasiliana nawe. Unaweza kuwatumia ujumbe wa maswali yoyote kabla hawajafika kwenye sehemu ya kukaa.

Garantii ya Mwenyeji ilinisaidia kuamua nijiunge na Airbnb kwa sababu ikiwa kutatokea uharibifu au matatizo, watanisaidia.

Dennis hukaribisha wageni jijini London kwa sababu ya urahisi wa kufanya mambo jijini humo

Pata maelezo kuhusu wanavyokaribisha wageni
Garantii ya Mwenyeji ilinisaidia kuamua nijiunge na Airbnb kwa sababu ikiwa kutatokea uharibifu au matatizo, watanisaidia.

Dennis hukaribisha wageni jijini London kwa sababu ya urahisi wa kufanya mambo jijini humo

Pata maelezo kuhusu wanavyokaribisha wageni

Tunakushughulikia

Tunafahamu kwamba ni kipaumbele kuwaamini watu wanaoishi nyumbani kwako. Airbnb hukuruhusu kuweka mahitaji madhubuti kwa watu wanaoweza kuweka nafasi na kuwajua wageni kabla ya kuja kukaa.

Hata hivyo, jambo fulani likitokea, tuko tayari kukusaidia. Kuanzia kinga yetu ya USD milioni 1 dhidi ya uharibifu wa nyumba hadi huduma ya kimataifa ya saa 24, unasaidiwa kama mwenyeji wakati wote.

Uwezo wa kuhitaji kitambulisho cha serikali kabla ya kuweka nafasi
Sheria za Nyumba ambazo ni lazima wageni wazikubali
Fursa ya kusoma tathmini za safari zilizopita
Kinga isiyolipishwa ya USD Milioni 1 dhidi ya uharibifu wa nyumba
Usaidizi kwa wateja wa saa 24 ulimwenguni kote

Malipo yamerahisishwa

Toza unachotaka

Kila wakati unachagua bei yako. Unahitaji msaada? Tuna nyenzo za kukusaidia kuendana na mahitaji katika eneo lako.

Lipa ada ya kiwango cha chini

Hakuna gharama ya kujisajili. Kwa kawaida Airbnb hutoza wenyeji kiwango sawa cha asilimia 3 kwa kila nafasi inayowekwa, hizi ni kati ya ada za chini zaidi katika tasnia hii.

Pokea malipo haraka

Mara mgeni anapoingia, tunaweza kutuma pesa zako kupitia Paypal, kuweka kwenye akaunti yako moja kwa moja, au kupitia njia nyinginezo zilizopo.

Majibu kwa maswali yako

Nani anaweza kuwa mwenyeji wa Airbnb?

Ni rahisi kuwa mwenyeji wa Airbnb katika maeneo mengi na tangazo linaundwa bila malipo daima. Fleti nzima na nyumba, vyumba vya kujitegemea, nyumba za kwenye mti na kasri ni baadhi tu ya majengo ambayo wenyeji wameshiriki kwenye Airbnb.

Kwa maelezo zaidi kuhusu kile kinachotarajiwa kwa wenyeji, angalia miongozo ya jumuiya ya Airbnb, inayozingatia usalama, ulinzi na kutegemeka na viwango vya ukarimu, ambavyo husaidia wenyeji kupata tathmini nzuri kutoka kwa wageni.

Ni nini kinachohitajika kwa wageni kabla ya kuweka nafasi?

Tunaomba kila mtu anayetumia Airbnb atupatie taarifa fulani kabla ya kusafiri pamoja nasi. Wageni wanahitaji kujaza taarifa hii kikamilifu kabla ya kutuma ombi la kuweka nafasi. Taarifa hizi husaidia kuhakikisha kuwa unamjua mtu anayekuja na jinsi ya kuwasiliana na mgeni.

Matakwa ya Airbnb kwa wageni ni pamoja na: • Jina kamili • Anwani ya barua pepe • Nambari ya simu iliyothibitishwa • Ujumbe wa utambulisho • Kukubaliana na Sheria za Nyumba yako • Taarifa za malipo

Wageni wanatarajiwa kuwa na picha ya wasifu, ingawa hilo si takwa. Unaweza pia kuwahitaji wageni kutoa kitambulisho kabla ya kuweka nafasi ya sehemu yako.

Je, inagharimu kiasi gani kutangaza sehemu yangu?

Kujisajili kwenye Airbnb na kutangaza nyumba yako ni bila malipo kabisa.

Mara tu mtu anapoweka nafasi kwako, tunatoza ada ya huduma ya Airbnb kwa wenyeji, kwa jumla ni asilimia 3, ili kusaidia kugharamia uendeshaji wa biashara.

Je, nina kinga gani dhidi ya uharibifu wa nyumba?

Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb hutoa ulinzi wa hadi dola 1,000,000 kwa mwenyeji kwa uharibifu wa mali iliyowekewa bima katika mazingira ya nadra ambapo uharibifu wa mgeni unapitiliza amana ya ulinzi au ikiwa amana ya ulinzi haijawekwa.

Mpango wa Garantii ya Mwenyeji haushughulikii pesa taslimu na hisa, vitu vya thamani vinavyokusanywa, sanaa adimu, vito, wanyama vipenzi au dhima ya mtu binafsi. Tunapendekeza wenyeji waweke vitu vyao vya thamani mahali salama au waviondoe wanapopangisha nyumba yao. Mpango huu pia haushughulikii upotevu au uharibifu wa mali kwa sababu ya uchakavu unaotokana na matumizi.

Pata maelezo zaidi kuhusu Garantii ya Mwenyeji kwenye http://airbnb.com/guarantee

Ninapaswa kuchaguaje bei ya tangazo langu?

Bei unayotoza kwa ajili ya tangazo lako ni uamuzi wako mwenyewe kabisa. Ili kukusaidia kuamua, unaweza kutafuta matangazo yanayofanana na lako katika jiji lako au kitongoji ili upate kujua bei za soko.

Ada za Ziada • Ada ya usafi: Unaweza kujumuisha ada ya usafi katika bei yako ya kila usiku au unaweza kuongeza ada ya usafi katika mipangilio yako ya bei. Ada nyinginezo: Ili kutoza ada za ziada nje ya bei zako (kama ada ya kuchelewa kuingia au ada ya mnyama kipenzi), lazima kwanza uwafichulie wageni tozo kama hizo kabla hawajaweka nafasi kisha utumie Kituo chetu cha Usuluhishi ili kuomba kwa usalama malipo ya ada za ziada.

Airbnb inawezaje kunisaidia katika kupanga bei?

Nyenzo ya Upangaji Bei Kiotomatiki hukuruhusu kuweka bei zako kwenda juu au chini kiotomatiki kulingana na mabadiliko katika mahitaji ya matangazo kama yako.

Nyakati zote wewe huwajibika kwa bei yako, kwa hivyo Upangaji Bei Kiotomatiki unadhibitiwa na mipangilio mingine ya bei unayochagua, nawe unaweza kurekebisha bei za usiku wakati wowote.

Upangaji Bei Kiotomatiki unategemea aina na eneo la tangazo lako, msimu, mahitaji na mambo mengine (kama matukio katika sehemu yako).

Uko tayari kupata mapato?