ULINZI WA MWENYEJI

Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb

Ikiwa mgeni anaharibu eneo lako au mali zako wakati wa kukaa na hakulipi gharama, unaweza kupata ulinzi wa uharibifu wa mali wa hadi Dola za Marekani 1,000,000.

Ikiwa mgeni anaharibu eneo lako au mali zako wakati wa kukaa na hakulipi gharama, unaweza kupata ulinzi wa uharibifu wa mali wa hadi Dola za Marekani 1,000,000.

Inatumika kiotomatiki kwa wenyeji kote ulimwenguni*
Huwalinda wenyeji tangu kuingia hadi kuondoka
Hailinganishwi katika tasnia ya safari

*Doesn’t apply to hosts who offer accommodations through Airbnb Travel, LLC, hosts in mainland China, hosts in Japan, hosts of experiences, or hosts of adventures.

Nini kimelindwa?

Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb inaweza kulinda:

  • Uharibifu katika eneo lako unaosababishwa na wageni
  • Uharibifu wa mali yako unaosababishwa na wageni
  • Uharibifu unaosababishwa na mnyama wa kumsaidia mgeni

Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb hailindi:

  • Wizi wa pesa na amana (Mfano: amana za akiba, vyeti vya hisa)
  • Uharibifu kutokana na uchakavu wa kawaida
  • Kujeruhiwa mwili au uharibifu wa mali kwa wageni au wengineo (hizo zinaweza kushughulikiwa na Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji)

Karibisha wageni kwa ujasiri

Uthibitisho wa utambulisho

Unaweza kuhitaji kwamba wageni wako wapitie mchakato wa kuthibitisha utambulisho wao kabla hatujathibitisha nafasi waliyoweka. Wageni huenda wakahitajika kutoa taarifa binafsi ili Airbnb iithibitishe, kama vile kitambulisho rasmi cha serikali.

Mawasiliano salama

Kisa fulani kikitokea, tovuti yetu salama ya kutuma ujumbe inakuruhusu uwasiliane na wageni na kusuluhisha matatizo. Ikiwa suluhisho haliwezi kupatikana, Garantii ya Mwenyeji imekusudiwa kusaidia.

Usaidizi wa saa 24

Ikiwa wewe, mali zako au wageni wako mtakumbwa na jambo fulani, timu yetu ya kimataifa ya Usaidizi wa Jumuiya iko tayari kutoa msaada.

Garantii ya Mwenyeji ni mojawapo ya mambo yaliyonisaidia kufanya uamuzi wa kujiunga na Airbnb, kwa sababu ikiwa kutatokea uharibifu au matatzio, hiyo itanisaidia."
Garantii ya Mwenyeji ni mojawapo ya mambo yaliyonisaidia kufanya uamuzi wa kujiunga na Airbnb, kwa sababu ikiwa kutatokea uharibifu au matatzio, hiyo itanisaidia."

Dennis, mwenyeji jijini London

Dennis, mwenyeji jijini London

Garantii ya Mwenyeji ni mojawapo ya mambo yaliyonisaidia kufanya uamuzi wa kujiunga na Airbnb, kwa sababu ikiwa kutatokea uharibifu au matatzio, hiyo itanisaidia."
Garantii ya Mwenyeji ni mojawapo ya mambo yaliyonisaidia kufanya uamuzi wa kujiunga na Airbnb, kwa sababu ikiwa kutatokea uharibifu au matatzio, hiyo itanisaidia."

Dennis, mwenyeji jijini London

Dennis, mwenyeji jijini London

Tumejitolea kuendeleza jumuiya salama na inayoaminika duniani kote.

Tumejitolea kuendeleza jumuiya salama na inayoaminika duniani kote.

Kidokezi cha usalama: Tathmini wasifu wa wageni

Ikiwa unataka kujua zaidi kumhusu mgeni kabla ya kukubali ombi lake la kuweka nafasi, angalia wasifu wake au usome tathmini kutoka kwa wenyeji wa zamani. Wenyeji na wageni wanaweza tu kutathminiana baada ya mgeni kuondoka, kwa hivyo unajua maoni hayo yanategemea ukaaji halisi.

Kidokezi cha usalama: Tathmini wasifu wa wageni

Ikiwa unataka kujua zaidi kumhusu mgeni kabla ya kukubali ombi lake la kuweka nafasi, angalia wasifu wake au usome tathmini kutoka kwa wenyeji wa zamani. Wenyeji na wageni wanaweza tu kutathminiana baada ya mgeni kuondoka, kwa hivyo unajua maoni hayo yanategemea ukaaji halisi.

Jinsi ya kuandikisha ombi la kurudishiwa gharama

1. Kusanya ushahidi wa uharibifu

Hii inaweza kujumuisha picha, video, makadirio, na/au risiti.

2. Wasiliana na mgeni wako kupitia Kituo cha Usuluhishi

Omba kurudishiwa pesa ndani ya siku 14 baada ya kuondoka au kabla ya mgeni wako ajaye kuingia, lolote linalotangulia. Atakuwa na saa 72 kujibu ombi lako.

3. Rudishiwa gharama au husisha Airbnb

Ikiwa mgeni hataki kulipa kiasi kamili, unaweza kustahiki kurudishiwa gharama chini ya Garantii ya Mwenyeji ya Airbnb. Mtaalamu wa usaidizi atakusaidia kwenye mchakato huu.

Airbnb's Host Guarantee is subject to certain terms, conditions, and exclusions. Visit our Host Guarantee Terms and Conditions to learn more.

Airbnb’s Host Guarantee is not an insurance policy, and not all property damage caused by guests is within its terms. If you want more protection, you’re encouraged to purchase personal insurance that will cover property damage not protected by the Host Guarantee.

Majibu kwa maswali yako

Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb ni nini?

Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb hutoa ulinzi wa hadi Dola za Marekani 1,000,000 kwa mwenyeji kwa uharibifu wa mali iliyowekewa bima katika hali ambayo ni ya nadra mgeni amefanya uharibifu unaozidi amana ya ulinzi au ikiwa amana ya ulinzi haijawekwa.

Mpango wa Garantii ya Mwenyeji haushughulikii pesa taslimu au hisa, vitu vya kukusanywa, sanaa adimu, vito, wanyama vipenzi au dhima ya mtu binafsi. Tunapendekeza wenyeji waweke vitu vyao vya thamani mahali salama au waviondoe wanapopangisha nyumba yao. Mpango huu pia haushughulikii kupotea au uharibifu wa mali kwa sababu ya uchakavu. Pata maelezo zaidi

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji ni nini?

Mpango wa Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji hutoa kinga ya dhima ya msingi ya hadi dola 1,000,000 kwa kila kisa iwapo kutakuwepo na mtu mwingine atakayedai kujeruhiwa mwili au kuharibiwa mali kunakohusiana na ukaaji wa Airbnb.

Kinga hii inadhibitiwa na kikomo cha dola 1,000,000 kwa kila eneo la tangazo na hali fulani, vikomo na vighairi vinavyoweza kutumika. Pata maelezo zaidi

Kuna tofauti gani kati ya Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb na Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji?

Mpango wa Garantii ya Mwenyeji na Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji ni mipango miwili tofauti ambayo Airbnb inatoa ili kuwalinda wenyeji iwapo uharibifu au majeraha yatatokea.

Garantii ya Mwenyeji: Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb imebuniwa ili kulinda wenyeji katika kisa nadra cha uharibifu wa mali zao, chumba au nyumba unaosababishwa na mgeni anayekaa kwenye sehemu hiyo. Garantii ya Mwenyeji si bima na si mbadala wa bima yako ya mmiliki wa nyumba au mpangaji wa nyumba.

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji: Mpango wa Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji ni bima na umebuniwa ili kuwalinda wenyeji katika hali ambapo mtu mwingine anatoa madai ya kujeruhiwa mwili au uharibifu wa mali. Mpango wa Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji unapatikana kwa wenyeji bila kujali mipango mingine ya bima, lakini itafanya kazi tu kama kinga ya bima ya msingi kwa visa vinavyohusiana na ukaaji wa Airbnb. Pata maelezo zaidi

Ninaombaje kurudishiwa gharama chini ya Garantii ya Mwenyeji?

Wenyeji na wageni mara nyingi hutatua matatizo wenyewe kupitia Kituo chetu cha Usuluhishi. Ikiwa hujafanya hivyo bado, wasiliana na mgeni wako kwanza ili kumwarifu kuhusu malalamiko yako na uwasilishe ombi la malipo katika Kituo chetu cha Usuluhishi.

Ikiwa huwezi kutatua tatizo na mgeni: Kwanza, tafadhali jifahamishe sheria na masharti ya Garantii ya Mwenyeji. Kumbuka kwamba maombi lazima yawasilishwe ama siku 14 tangu kuondoka kwa mgeni, au kabla ya mgeni mwingine kuingia, lolote litakalotokea kwanza. Pata maelezo zaidi

Bima ya mmiliki wa nyumba hufanyaje kazi kwenye Airbnb?

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji ya Airbnb itafanya kazi kama bima ya msingi na hutoa kinga ya dhima kwa wenyeji na pale inapofaa, wamiliki wao wa nyumba, chini ya masharti fulani, vikomo na vighairi.

Ikiwa una maswali kuhusu jinsi sera hii inavyoingiliana na bima yoyote ya mmiliki wa nyumba au ya mpangaji, unapaswa kujadili kinga yako ya bima na mtoa huduma wako wa bima. Baadhi ya sera zinawalinda wamiliki wa nyumba na wapangaji kutokana na mashtaka fulani yanayotokana na kujeruhiwa kwa mgeni, lakini nyingine hazifanyi hivyo. Daima ni wazo zuri kuijulisha kampuni yako ya bima kuhusu shughuli ya upangaji kwenye sehemu yako hata ingawa dhima inayotokea wakati wa ukaaji wa Airbnb inapaswa kushughulikiwa na sera ya Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji. Pata maelezo zaidi

Je, Garantii ya Mwenyeji inatumika kwenye Open Homes?

Ndiyo. Garantii ya Mwenyeji ya Airbnb hutoa ulinzi wa hadi Dola za Marekani 1,000,000 kwa mwenyeji kwa ajili ya uharibifu wa mali iliyokingwa katika tukio la nadra la mgeni kufanya uharibifu unaozidi amana ya ulinzi au ikiwa hakuna amana ya ulinzi iliyowekwa. Garantii ya Mwenyeji inatumika katika sehemu zote za kukaa zilizowekewa nafasi kwenye Airbnb, ikijumuisha Open Homes. Pata maelezo zaidi

Uko tayari kuanza kukaribisha wageni?

Uko tayari kuanza kukaribisha wageni?