Maboresho kwa ajili ya Wenyeji weledi

Dhibiti kazi za kila siku na ufuatilie ubora wa tangazo kutoka kwenye programu yako iliyounganishwa.
Na Airbnb tarehe 26 Mac 2024
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 26 Mac 2024

Maelezo ya mhariri: Makala haya yalichapishwa kama sehemu ya Airbnb 2023 Toleo la Kiangazi. Taarifa zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa. Pata maelezo zaidi kuhusu toleo letu la hivi karibuni.

Airbnb 2023 Toleo la Kiangazi inakuletea maboresho 25 kwa ajili ya Wenyeji pamoja na maboresho nane ya ziada kwa ajili ya Wenyeji wanaotumia programu iliyounganishwa na API. Haya yameundwa ili kukusaidia kufuatilia ubora wa matangazo yako kwa urahisi zaidi na kusaidia shughuli zako za kila siku za kukaribisha wageni.

Utaweza kufikia matoleo yote mapya nane moja kwa moja kutoka kwenye programu yako  ikiwa mtoa huduma wako wa programu ameyaunganisha. Ikiwa sivyo, wasiliana na mtoa huduma wako wa programu ili kujua ni lini yatapatikana.

Maelekezo ya kutoka

Weka maelekezo ya kina ya kutoka moja kwa moja kutoka kwenye programu yako, sawa na jinsi unavyoweka sheria za kawaida za nyumba. Andaa kwa haraka orodha ya kutoka kwa kuchagua kutoka kwenye kazi hizi za kawaida: 

  • Kusanya taulo zilizotumika
  • Tupa taka
  • Zima vifaa vya umeme
  • Funga mlango
  • Rejesha funguo

Unaweza kuweka maelezo kwa kila kazi. Kwa mfano, unaweza kubainisha kwamba wageni huweka takataka kwenye pipa moja na vitu vinavyoweza kutumika tena kwenye pipa jingine. Unaweza pia kuandika maombi ya ziada, kama vile kufunika jiko la kuchoma nyama baada ya matumizi. 

Tutawatumia wageni kikumbusho cha kiotomatiki kikiwa na wakati wako wa kutoka na maelekezo siku moja kabla ya kutoka. Kama ilivyo kwa sheria zako za nyumba, wageni wanaweza kusoma maelekezo yako ya kutoka kabla hawajaweka nafasi kwako. Mara baada ya kutoka, wageni wanaweza kukujulisha kuwa wameondoka kwa mbofyo au mguso mmoja tu.

Lebo za tathmini

Katika Airbnb 2022 Toleo la Novemba, tuliongeza uwezo kwa wageni na Wenyeji kutoleana maoni ya kina zaidi. Nyote mnaweza kuweka ukadiriaji wa nyota na kubainisha kilichokwenda vizuri au kinachoweza kuboreshwa, katika aina kadhaa. Kwa mfano, wageni wanaweza kuchagua lebo za tathmini "anajibu kila wakati" au "maelekezo yanasaidia" ikiwa watakadiria mawasiliano yako kwa nyota tano. 

Sasa unaweza kufikia vipengele hivi kutoka kwenye programu yako iliyounganishwa. Utaweza kuandika tathmini za kina zaidi za wageni na kupata maoni kuhusu kile ambacho wageni walipenda na kile kinachoweza kuboreshwa.

Matatizo ya tangazo

Ikiwa mojawapo ya matangazo yako hayafuati sheria za msingi kwa ajili ya Wenyeji, utapata rekodi ya safari za hivi karibuni ambazo zilikuwa na matatizo katika programu yako. Kwa mfano, ikiwa mgeni atakadiria mchakato wake wa kuingia kwa nyota mbili kwa sababu hakuweza kuingia ndani, hiyo itaingizwa hapa na mabadiliko yanayopendekezwa ili kuboresha utaratibu wako wa kukaribisha wageni.

Matatizo ya tangazo yanayoonekana hapa ni matokeo ya ukadiriaji wa chini, maoni ya wageni kuhusu huduma kwa wateja au Mwenyeji kughairi. Rejesta hiyo pia inakujulisha ikiwa tangazo lako liko hatarini kuzuiwa au kuondolewa.

Arifa za sheria za msingi

Tutakutumia barua pepe na arifa kwa simu kupitia mtoa huduma wako wa programu ikiwa mojawapo ya matangazo yako hayafuati sheria za msingi kwa ajili ya Wenyeji na limepokea onyo au liko katika hatari ya kusimamishwa au kuondolewa. Arifa itakupeleke kwenye rejesta ya matatizo ya tangazo, ambayo inaonyesha ni matatizo gani yaliyoripotiwa, na mapendekezo kuhusu jinsi ya kuyatatua. 

Pia utapata taarifa kuhusu wakati ambapo tangazo linaweza kuamilishwa tena baada ya kusimamishwa na pia jinsi kuondolewa kwa tangazo kunavyoweza kukatiwa rufaa. Unaweza tu kukata rufaa moja kwa moja kwenye Airbnb.

Taarifa za aina

Airbnb za Airbnb huwasaidia wageni kugundua mamilioni ya maeneo ya kipekee ya kukaa duniani kote. Zaidi ya aina 60 tofauti huainisha maeneo kulingana na mtindo, eneo au ukaribu wake na shughuli fulani.

Sasa unaweza kujua ni aina gani ya Airbnb ambayo kila tangazo lako lipo kwenye programu yako. Hili lilikuwa ombi lililoombwa na wengi kutoka kwa Wenyeji na litakuwezesha kuelewa jinsi matangazo yako yanavyoonyeshwa kwenye Airbnb.

Arifa za uzingatiaji

Utapata arifa katika programu yako iliyounganishwa utakapohitaji kujaza fomu ya uzingatiaji inayohitajika au kutoa taarifa nyingine ya biashara. Utaweza pia kupokea ujumbe kwenye programu yako ikiwa taarifa za ziada zinahitajika.  

Tunahitaji kukusanya na kuthibitisha taarifa za biashara za Wenyeji kwenye Airbnb ili kuzingatia sheria za eneo husika. Sasisho hili hukuruhusu kujua na kukamilisha mahitaji ya uzingatiaji kutoka kwenye programu yako.

Idadi ya wanyama vipenzi wanaoruhusiwa

Ulituambia kwamba ulitaka kuweza kubainisha hasa idadi ya wanyama vipenzi unaweza kuwakaribisha. Sasa unaweza kuweka kwa urahisi idadi ya juu ya wanyama vipenzi unaotaka kuwakaribisha, hadi watano.

Promosheni ya tangazo jipya

Tulisikia pia kwamba ulitaka uwe na uwezo wa kutoa promosheni ya tangazo jipya kwa wageni kutoka kwenye programu yako. Tumia kiotomatiki promosheni ya punguzo la asilimia 20 kwenye nafasi zako tatu za kwanza zinazowekwa unapounda tangazo jipya.

Airbnb
26 Mac 2024
Ilikuwa na manufaa?