Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kubadilisha sehemu yako iwe bingwa wa mitandao ya kijamii

  Pata maelezo kuhusu kuwepo katika mitandao ya kijamii kunavyoweza kukusaidia ili sehemu yako iwekewe nafasi zaidi.
  Na Airbnb tarehe 22 Mei 2019
  Inachukua dakika 8 kusoma
  Imesasishwa tarehe 14 Mei 2021

  Vidokezi

  • Chagua jina la kukumbukwa na lenye kuvutia kwa ajili ya kutangaza sehemu yako

  • Chapisha picha nzuri zenye ubora wa hali ya juu ili kuhamasisha watu na kupigia debe tangazo yako

  • Unda ushirikiano na waraghibishaji wa eneo husika ili kutoa sehemu za kukaa zenye mapunguzo huku wao wakikupa maudhui

  • Ongeza wafuasi kwa kuwa balozi mtandaoni katika eneo lako

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni

  Kupenya katika mazingira ya mitandao ya kijamii kunaweza kuhisi kana kwamba umepotea msituni. Unaanzia wapi? Je, maudhui mazuri yanaundwa vipi? Na yanawezaje kuwa nafasi zaidi zinazowekwa? Tom Feldman wa Tye Haus huko Skykomish, Washington, anashiriki mtazamo wake wenye mafanikio (na ambao kwa kweli una ubinadamu) wa kuongeza wafuatiliaji mtandaoni na kuifanya nyumba yako iwape wageni hamu ya kuizuru.

  “Simulizi letu la kuwa kukaribisha wageni lilianza mnamo 2012 wakati tulinunua nyumba yetu ya kwanza yenye umbo la A, inaitwa Tye Haus. Tuliiboresha, tukaitangaza kwenye Airbnb na tukaanzishaakaunti ya Instagram ikiwa na picha za nyumba yetu pamoja na maonyesho ya kisinema kutoka eneo letu—yakiangazia ziara zetu, vivutio vya karibu na tulichopenda kwenye bustani. Mara tu baada ya hapo, mpigapicha maarufu Alex Strohl aliwasiliana nasi na kuuliza kama tunaweza kushirikiana. Tulimkaribisha kwa miezi miwili katika hali ya likizo ya ubunifu na kwa upande wetu tukapata picha za kushiriki kwenye mipasho yetu mtandaoni. Tulipoanza kuchapisha picha za Alex, hapo ndipo umaarufu wetu ulipoanza. Huo ulikuwa mwazo wa ushirikiano na mashindano mengi yaliyofuata.

  “Mimi na familia yangu sasa tunasimamia nyumba tatu za mbao zenye mwonekano wa A na tunaendelea kuwakaribisha waraghibishaji kutoka kote ulimwenguni. Baada ya kushiriki maudhui yao yaliyotambulika kwenye mpasho wetu, sisi tunawapa sehemu ya kuvinjari, kusisimka na kupumzika. Hii imekuwa moja ya mbinu zetu kuu za uuzaji. Tumepanda kutoka asilimia 30 hadi takribani asilimia 100 ya kiwango cha ukaaji, hivyo kujaza siku za wiki na vilevile miezi yenye wageni wachache. Pia tuna takribani wafuatiliaji elfu 115 mtandaoni. Haya ni baadhi ya vidokezi vyetu vya jinsi ya kuweka nyumba yako katika ramani ya mitandao ya kijamii.”

  1. Ipe sehemu yako jina

  “Hatua ya kwanza ya kutangaza nyumba yako inaweza kuonekana kuwa ndogo, lakini ni muhimu—nayo ni kuipa sehemu yako jina. Unashauriwa kutafuta jina ambalo ni tofauti, linaweza kukumbukwa, na lenye mtindo. Kisha, unaweza kuitangaza nyumba yako na kusajili jina lako la mtumiaji kwenye Instagram.

  “Haya hapa ni baadhi ya maswali ya kukusaidia kutafuta jina:

  • Una nyumba ya aina gani? Je, ni chalet, au nyumba iliyo ufukweni? Je, ni nyumba yenye muundo wa Tudor au roshani?
  • Una mada mahususi? Je, mwonekano wa ndani wa nyumba yako hufuata mtindo fulani? Je, ina mada ya maharamia (naam zipo!)?
  • Je, ina uhusiano na eneo, jiji au mji wako? Je, inaweza kushirikishwa na jina lako?
  • Je, kuna umuhimu wa kihistoria? Jina zuri linaweza kutokana na matukio ya zamani.

  “Fanya utafiti mtandaoni ujue ni nini matangazo mengine yanafanya na pia ni majina gani yanayopatikana kwenye mitandao ya kijamii. Kwa upande wetu, tuliipa nyumba yetu ya mbao ya kwanza jina la mto jirani, Mto Tye. Tahajia ya nusu ya pili, Haus, ilitokana na mji wa karibu wa muundo wa Bavaria wenye jina Leavenworth. Kwa pamoja, ikawa Tye Haus”.

  2. Anza kwa picha nzuri

  “Ukishapata jina lako na akaunti za mitandao ya kijamii, unafaa kuanza kwa picha nzuri. Usijaribu, ninarudia, usijaribu, kuanza na rundo la picha zenye ubora duni. Picha zilizo kwenye mpasho wako ndicho kitu cha kwanza ambacho watu wataona—bila shaka unataka wahisi mshawasha! Ndizo zitakazouza tangazo lako. Picha zako zinapaswa:

  • Kutobadilika: Dumisha mwonekano sawa na ustadi wa kutamanika.
  • Ubora wa juu: Chapisha picha na video zenye mwonekano bayana, wazi na zenye ubora wa juu—epuka picha zenye ukungu au michelemichele.
  • Sahihi: Maudhui yanafaa kuakisi nyumba yako vizuri.

  “Jaribu kuangazia kinachotofautisha nyumba yako na nyinginezo. Je, ni mambo ya ndani, sifa au eneo? Pata kinachofanya nyumba yako ipendeze. Kumbuka kuwa hutangazi tu sehemu yako, bali pia unashiriki uzoefu ambao watu wanaweza kupata ikiwa watatembelea: eneo lako, mandhari na shughuli katika eneo husika. Ikiwa huwezi kupiga picha nzuri, zingatia kupata huduma za mtaalamu wa kupiga picha unapoanza.”

  3. Unda ushirikiano wa ubunifu

  “Njia nyingine ya kuzalisha maudhui mazuri kwa ajili ya mpasho wako ni kushirikiana na waraghibishaji (kwa mfano, wapigapicha, wanablogu na wapigavideo) na uwape sehemu za kukaa zenye mapunguzo ili na wao wakupe maudhui. Tunapendekeza utafiti na uwasiliane na wapigapicha wa karibu, wanablogu na wapiga video pamoja na waunda maudhui walio katika eneo lako.

  “Mkakati huu ni mojawapo ya vichangiaji vikuu vya idadi kubwa ya wanaotembelea ukurasa wetu. Huku waraghibishaji wakishiriki machapisho yao kuhusu sehemu yako, watumiaji wapya watayaona na kugundua nyumba yako.

  “Unapowasiliana na mraghibishaji ili kuomba ushirikiano, ni muhimu:

  • Kuwa mtaalamu. Anza ukiwa tayari na mwenye ujuzi. Uliza maswali sahihi ambayo yatasaidia kusogeza ushirikiano mbele.
  • Kuwa wazi. Inaweza kuwa rahisi tu kama kusema: ‘Jamani, naipenda kazi yako. Ninaanzisha biashara yangu ya Airbnb. Je, ungependa tushirikiane katika ubadilishanaji wa ubunifu: ukae kwangu huku ukinipa picha au kuniandikia kisha nisema maudhui hayo ni kwa hisani yako?’
  • Bainisha matarajio yako. Andaa makubaliano kwa ajili ya pande zote mbili ili iwe wazi ni nini kila mmoja wenu anatarajia na nini atapokea. Makubaliano yanapaswa kujumuisha maelezo kama vile tarehe za utekelezaji, haki za picha, kutambulisha, idadi ya picha/video na aina za faili, nk.
  • Fanikisha ushindi kwa wote. Ichukulie kuwa ushirikiano na ujitahidi kuhakikisha kuwa ushirikiano huo ni wa faida kwa pande zote mbili.

  Kidokezi kingine kinachohusiana ni kutokuwa kamwe na ratiba isiyo na chochote. Ikiwa una tarehe zozote zisizo na watu dakika za mwisho, nufaika na wakati wa kutokuwa na shughuli nyingi na uitumie katika juhudi zako za uuzaji. Alika mraghibishi wa eneo husika akae kwako ili uweze kutumia wakati huo kutengeneza maudhui ya ziada kwa ajili ya mpasho wako.

  4. Ongeza wafuasi

  Ukishaanzisha uwepo mtandaoni na kuwa na mpasho uliojaa picha nzuri, basi ni wakati wa kujitambulisha. Unaweza kufanywa hivi kwa njia tofautitofauti:

  • Kuwa balozi wa mtandaoni wa eneo lako. Tafuta sehemu zinazokufaa mtandaoni na uzifuatilie. Kwa hivyo kwa Tye Haus, tunapenda kufuatilia yanayoendelea katika mitandao ya kijamii ya biashara za karibu na vitambulishi vya maeneo jirani. Tunafuata kituo cha mchezo wa kuteleza kwenya theluji kilicho karibu, kwa mfano, tunaweza kujibu maswali yanayoachwa na watu wengine au kutoa maoni na kusema “Habari, wakati mwingine ukiwa mjini, njoo ukae kwetu.”
  • Shirikiana na wadau kuandaa mashindano na zawadi. Pia huwa tunaendesha mashindano na matangazo ili kuongeza idadi ya wanaotufuatilia. Kuwa na uthubutu ili upate ushirikiano unaoingiana vyema na “chapa” yako. Tumeshirikiana na kampuni ya blanketi, matandiko na ya vyombo vya kulia ili kupigiana debe kwa hadhira zetu. Tumewasiliana nao kuwaambia, “Aisee, tunaenda kutafuta waraghibishaji ili wahamasishe kuhusu bidhaa yako, ungependa kushirikiana nasi? Ninaweza kutoa ofa ya sehemu ya kukaa bila malipo.” Hizi pia ni fursa nzuri za kuanza kanzidata ya barua pepe.

  5. Kuwa mkweli

  Kwa kawaida, watu huwavutiwi sana na kujitangaza, iwe ni mtandaoni au ana kwa ana—kwa hivyo ni muhimu kuwa mkweli katika utangamano wako wote. Usitoe tu maoni kwenye chapisho la kila mraghibishi ukitumia ujumbe huo huo ili tu uonekane—au uanze kutuma taka kwa kila akaunti unayoona. Kuna tofauti isiyo bayana, na watu wanaweza kuhisi unapolazimishia kitu kugumu kukubalika. Kuwa mkweli katika kile unachosema na utavutia watu sahihi.

  Nina kanuni moja inayoniongoza binafsi, huwa ninajaribu nisitumie maneno mengi yenye alama ya reli. Huwa tunaweka manukuu kadhaa yanayohusiana kwenye picha na kujumuisha alama reli 5-10 pekee kwa kila chapisho. Watu wengine hutumia manukuu mengi ya kutambulisha picha na alama reli ili kugundulika, lakini napendelea mtindo wa kutojishaua.

  Kumbuka kuwa kuongeza wafuatiliaji kunachukua muda na kwa hakika hakufanyiki ghafla bin vuu. Ninakuhimiza utumie vidokezi hivi, uwe mbunifu na kwa hakika utajipatia ufuasi katika jumuiya inayokua ya wanamitandao ya kijamii—utaona matokeo katika viwango vya ukaaji.

  Kila la heri katika kukaribisha wageni!
  Tom

  Vidokezi

  • Chagua jina la kukumbukwa na lenye kuvutia kwa ajili ya kutangaza sehemu yako

  • Chapisha picha nzuri zenye ubora wa hali ya juu ili kuhamasisha watu na kupigia debe tangazo yako

  • Unda ushirikiano na waraghibishaji wa eneo husika ili kutoa sehemu za kukaa zenye mapunguzo huku wao wakikupa maudhui

  • Ongeza wafuasi kwa kuwa balozi mtandaoni katika eneo lako

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni
  Airbnb
  22 Mei 2019
  Ilikuwa na manufaa?