Kuelewa kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo

Huduma ya Kuweka Nafasi Papo Hapo inaweza kurahisisha mchakato wa kuweka nafasi na kusaidia tangazo lako lionekane.
Na Airbnb tarehe 14 Des 2020
Inachukua dakika 3 kusoma
Imesasishwa tarehe 17 Nov 2022

Vidokezi

  • Sasisha kalenda yako unapotumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo

  • Chagua vigezo vyako mwenyewe vya Kuweka Nafasi Papo Hapo

  • Washa kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kutengeneza tangazo lenye mafanikio

Kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo huwaruhusu wageni kuweka nafasi kwenye nyumba yako papo hapo kwa tarehe zinazopatikana, kwa hivyo hulazimiki kutathmini na kukubali kila ombi la kuweka nafasi kivyake. Wageni wanapenda chaguo la kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo na Wenyeji wengi huripoti kwamba wanapata pesa zaidi kwa kutumia nyenzo hii, pia wanathamini urahisi wake.

Kuhakikisha kwamba kalenda yako imesasishwa ni muhimu katika kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo kwa ufanisi. Ikiwa kalenda yako imepitwa na wakati, unaweza kushangazwa na nafasi zilizowekwa usizotarajia au ulazimike kughairi nafasi iliyowekwa kwa sababu ya hitilafu ya uratibu, hali ambayo inaweza kusababisha kutozwa ada ya kughairi. Ili uhakikishe kwamba kalenda yako ya Airbnb imesasishwa kila wakati, ni wazo zuri kuioanisha na kalenda yako ya msingi (iCal, Google, n.k.).

Nyenzo za kusaidia kuwa na utulivu zaidi wa akili

Mwanzoni baadhi ya Wenyeji wanaweza kusita kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo kwa sababu wana wasiwasi kwamba hawatakuwa na taarifa za kutosha kuhusu wageni watarajiwa kabla ya kuweka nafasi. Kabla wageni hawajatumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, wanapaswa kukidhi masharti yako yote ya wageni na wakubali Sheria za Nyumba yako.

Unaweza kuweka masharti yako ya kutoa huduma ya Kuweka Nafasi Papo Hapo kwa wageni wale tu walio na rekodi nzuri, ikiwa na maana kwamba waliwahi kukaa angalau mara moja na hawajapokea tathmini zozote mbaya, vilevile wageni ambao wamepitia mchakato wa Airbnb wenye hatua nyingi wa kuthibitisha utambulisho.

Tumepanua mchakato wa kuthibitisha utambulisho kwa wageni wote wanaoweka nafasi wanaosafiri kwenda katika nchi na maeneo 35 maarufu kwenye Airbnb, yakiwakilisha asilimia 90 ya nafasi zote zilizowekwa. Tutafanya mchakato huu upatikane duniani kote kufikia mapema mwaka 2023. Ikiwa unahitaji kitambulisho cha serikali kutoka kwa wageni wako kwa sababu binafsi au ikiwa ni masharti ya eneo ambapo nyumba yako ipo, unaweza kuwaomba wageni kwa kuwatumia ujumbe kupitia kikasha chako cha kukaribisha wageni.

Kwa nini bado unaweza kupata maombi ya kuweka nafasi

Hata ikiwa umewasha kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, kuna matukio ambapo unaweza kupokea maombi ya kuweka nafasi kutoka kwa wageni. Hili linaweza kutokea ikiwa hujasasisha kalenda yako kwa muda au ikiwa hivi karibuni ulighairi nafasi iliyowekwa. Wageni ambao hawakidhi vigezo vyako vya kuweka nafasi papo hapo wanaweza pia kutuma maombi ya kuweka nafasi. Kwa kila ombi ambalo utalipokea, utahitaji kujibu kwa kukubali au kukataa nafasi iliyowekwa au kutuma ujumbe kwa wageni wako watarajiwa ndani ya saa 24.

Kwa nini baadhi ya Wenyeji hawatumii kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo

Licha ya faida za Kuweka Nafasi Papo Hapo, baadhi ya Wenyeji wanaona kuwa kuhitaji maombi ya kuweka nafasi kunawafaa zaidi:

  • Wanatoa ukaaji wa muda mrefu pekee. Annie, Mwenyeji huko Sonoma, California, hutumia maombi ya kuweka nafasi kwa sababu yeye hutoa tu ukaaji wa siku 30 au zaidi ili kuzingatia kanuni za kukaribisha wageni katika eneo lake. “Ningependa kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, lakini kuna masuala zaidi ya kuzingatia wakati unamkaribisha mtu kwa muda mrefu kiasi hicho,” anasema.
  • Wana mahitaji ya kipekee ya binafsi. Nichola, ambaye ni Mwenyeji huko Guelph, Kanada, ana mizio ya kimazingira ambayo inamhitaji kuhakikisha kwamba sehemu yake haina harufu, kwa hivyo anatumia maombi ya kuweka nafasi ili kuhakikisha kuwa wageni wapo tayari kukubali sheria mahususi za nyumba yake. “Huwa ninaumwa kichwa kutokana na bidhaa zenye harufu kwa hiyo ninahitaji kuhakikisha kwamba wageni wangu ni watu ambao wanaelewa mizio ya harufu,” anasema.
  • Sehemu yao ina vipengele au changamoto maalumu. Mifano inaweza kujumuisha chumba cha kujitegemea ndani ya makazi ambayo yana wanyama vipenzi au watoto au sehemu isiyo na mapambo ambayo inaweza kuwa changamoto kwa baadhi ya wageni. Maombi ya kuweka nafasi yanaweza kuwa chaguo zuri la kuhakikisha kwamba wageni wanafahamu mambo yote ya kipekee ya nyumba yako kabla ya kuitembelea.

Kuaminika ni muhimu katika kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo

Ni uamuzi wako kuchagua kutumia au kutotumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, lakini kumbuka kwamba kuaminika ni sehemu muhimu ya kuwa Mwenyeji bora. Zingatia sera za kughairi za Mwenyeji za Airbnb na ujaribu kuepuka kughairi inapowezekana.

Kwa kuongezea hayo, ikiwa unatumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo na una mashaka na nafasi fulani baada ya hiyo kuwekwa (kwa mfano, kwa sababu wageni wako watarajiwa wanauliza ikiwa wanaweza kuvunja sheria za nyumba yako), unaweza kughairi nafasi iliyowekwa bila adhabu kwa kutumia nyenzo ya kughairi mtandaoni hadi mara tatu kwa mwaka wa kalenda.

Kumbuka kwamba huwezi kamwe kughairi kwa sababu yoyote inayokiuka sera ya kutobagua ya Airbnb. Na ikiwa utaghairi nafasi iliyowekwa, hiyo inaashiria kwamba kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo huenda kisikufae kwa sasa, kwa hiyo Airbnb inaweza kukutumia maombi ya kuweka nafasi badala yake kwa ajili ya nafasi kadhaa zijazo utakazowekewa.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Sasisha kalenda yako unapotumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo

  • Chagua vigezo vyako mwenyewe vya Kuweka Nafasi Papo Hapo

  • Washa kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo

  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kutengeneza tangazo lenye mafanikio
Airbnb
14 Des 2020
Ilikuwa na manufaa?