Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kuelewa kalenda yako na mipangilio ya kuweka nafasi

  Weka upatikanaji wako ili uwekewe nafasi unazotaka.
  Na Airbnb tarehe 1 Des 2020
  Inachukua dakika 4 kusoma
  Imesasishwa tarehe 20 Okt 2022

  Vidokezi

  • Sasisha mipangilio yako ya bei na upatikanaji

  • Oanisha kalenda zako ili usaidie kuepuka ughairi na adhabu

  • Chagua jinsi ambavyo wageni wanaweza kuweka nafasi kwenye eneo lako

  Mipangilio ya kalenda yako na ya kuweka nafasi inakupa udhibiti kamili kuhusu wakati unapopangisha sehemu yako, kuanzia wikendi chache hadi siku 365 kwa mwaka. Kufahamu mipangilio hii kunaweza kukusaidia uendeshe biashara yako ya kukaribisha wageni kwa utaratibu zaidi na kukidhi mahitaji ya wageni wako pia.

  Kusasisha upatikanaji wa kalenda yako pia kunaweza kukusaidia uepuke kughairi nafasi iliyowekwa, hatua ambayo inaweza kusababisha ada na adhabu nyingine kwako na kuwapa wageni huduma mbaya. Hivi ndivyo unavyoweza kuweka mipangilio ya kalenda na ya kuweka nafasi inayokufaa.
  Ninatumia kalenda yangu na mipangilio ya kuweka nafasi ili kutengeneza aina ya tangazo ninalotafuta kama msafiri—lile ambalo ninaweza kuliwekea nafasi haraka na kuingia mapema.
  Superhost Kevino,
  Mexico City

  Kuweka upatikanaji wa kalenda yako

  Kusasisha kalenda yako ni muhimu: Kadiri tarehe zako zinavyopatikana, hadi miaka miwili mapema, ndivyo machaguo ya wageni yanavyokuwa mengi.

  Unaweza kutumia mipangilio ya kalenda yako na ya kuweka nafasi ili kuweka usawa kati ya kutoa upatikanaji mwingi kwa wageni na kuweka ratiba inayokufaa. Mwenyeji Bingwa Kevino hutumia mipangilio hii ili:
  • Sasisha bei kulingana na uhitaji katika eneo hilo. “Huwa ninatoza bei ya juu mwezi Oktoba na Novemba, ambao unazingatiwa kuwa msimu wa shughuli nyingi huko Mexico City kwa sababu ya sherehe nyingi zinazofanyika. Kila mtu anataka kuwa hapa kwa ajili ya Siku ya Wafu!”
  • Weka nyakati maalumu za kuingia na kutoka. “Wageni wanaweza kuingia kuanzia saa 8:00 alasiri na kutoka wakati wowote kabla ya saa 6:00 mchana, ninataka wageni wangu wahisi kwamba wana muda wa kupumzika na kupata kifungua kinywa kabla ya kuondoka. Mimi pia hutoa sehemu iliyofungwa ambapo wageni ambao wanataka kukaa jijini baada ya kutoka wanaweza kuhifadhi mizigo yao kwa usalama.”
  • Zuia tarehe ambazo ametenga kwa ajili ya familia, marafiki au wageni wa mara kwa mara. "Pia nina baadhi ya wageni ambao wanapenda kurudi kila mwaka kwa wakati ule ule, kwa hivyo mara nyingi mimi huzuia tarehe hizo."

  Unaweza pia kutumia mapendeleo yako ya kuweka nafasi ili:

  • Kuchagua muda unaohitaji ili kujiandaa kwa ajili ya wageni. Baadhi ya Wenyeji hawaruhusu kuwekewa nafasi siku hiyo hiyo au siku inayofuata kwa sababu wanataka muda zaidi wa kufuata mchakato wa kufanya usafi wa hatua tano.
  • Weka muda wa chini na wa juu wa kukaa. Baadhi ya Wenyeji huhitaji ukaaji wa angalau usiku mbili, ilhali wengine huhitaji ukaaji wa wiki moja au zaidi wakati wa msimu wa wageni wengi katika eneo lao.
  • Oanisha kalenda yako ya Airbnb na kalenda zako nyingine za mtandaoni ili uhakikishe kwamba kila wakati unafahamu nafasi zilizowekwa zinazokaribia.

  Ni muhimu kukumbuka kwamba kalenda yako inafuatilia nafasi zinazowekwa na wageni wako pia. Unaweza kuchagua kuonyesha au kuficha maelezo ili kuangalia upatikanaji wa muda mrefu, kutathmini bei za kila usiku za zamani, kurekebisha bei na promosheni za siku zijazo na kupanga mapema ukiwa na uhakika.

  Kuchagua jinsi wageni wanavyoweza kuweka nafasi ya sehemu yako

  Wageni wanaweza kuweka nafasi kwenye sehemu yako kwa njia moja kati ya mbili: kupitia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo au ombi la kuweka nafasi.

  Kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo huwaruhusu wageni ambao wanakidhi matakwa yako yote na kukubali sheria za nyumba yako kuweka nafasi papo hapo kwa tarehe zozote zinazopatikana. Nyenzo hii huharakisha mchakato wa kuweka nafasi kwa ajili ya wageni, huku ukiondoa uhitaji wako wa kutathmini na kukubali kila ombi la kuweka nafasi.

  Nilifanya jaribio ambapo nilichapisha tangazo langu kwanza likiwa na maombi ya kuweka nafasi mwenyewe kisha likiwa na kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo. Kupitia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, nilipata nafasi nyingi zaidi zilizowekwa.
  Superhost Kevino,
  Mexico City

  Maombi ya kuweka nafasi huwaruhusu Wenyeji kukubali nafasi zilizowekwa kivyake, ndani ya saa 24 baada ya kuyapokea. Njia hii hupendelewa na Wenyeji ambao:

  • Wana upatikanaji usiotabirika kwa sababu ya mahitaji yao binafsi na ratiba
  • Wanatoa sehemu iliyo na vipengele vya kipekee, kama vile hali ngumu sana za mashambani, wanayotaka kuwasiliana na wageni kuhusu kuweka matarajio kabla ya kuweka nafasi
  • Wanatoa ukaaji wa muda mrefu wa usiku 28 au zaidi
  Kupitia mipangilio hii na mingine, una udhibiti kuhusu lini na jinsi gani sehemu yako itawekewa nafasi na kuunda kalenda ya kukaribisha wageni inayokufaa.

  Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu wa kuweka tangazo lenye mafanikio

  Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Vidokezi

  • Sasisha mipangilio yako ya bei na upatikanaji

  • Oanisha kalenda zako ili usaidie kuepuka ughairi na adhabu

  • Chagua jinsi ambavyo wageni wanaweza kuweka nafasi kwenye eneo lako

  Airbnb
  1 Des 2020
  Ilikuwa na manufaa?