Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Jinsi unavyolipwa kwa kukaribisha wageni

  Pata maelezo ya misingi kuhusu lini na jinsi utakavyopokea malipo.
  Na Airbnb tarehe 12 Feb 2020
  Inachukua dakika 2 kusoma
  Imesasishwa tarehe 13 Ago 2021

  Vidokezi

  Wenyeji wapya mara nyingi huuliza, "Nitalipwa vipi?" Airbnb hufanya iwe rahisi kupokea malipo—au kile tunachokiita kutuma malipo—kwa hatua chache rahisi. Hivi ndivyo inavyofanya kazi:

  Jinsi utakavyolipwa

  Ili kupokea malipo kwenye Airbnb, ni lazima uchague njia yako ya kupokea malipo katika sehemu ya Malipo na Kupokea Malipo ya akaunti yako. Njia za kupokea malipo zinajumuisha malipo kwa njia benki au ACH, PayPal, Kadi za Malipo ya Awali za Payonner na Western Union, miongoni mwa nyinginezo, kulingana na mahali ulipo.

  Hapa kuna muhtasari mfupi wa jinsi ya kuweka njia ya kupokea malipo kutoka kwenye akaunti yako:

  Njia yako ya kupokea malipo itathibitishwa ili kusaidia kuhakikisha pesa zako zote ulizopata kwa jasho zinatumwa kwa mafanikio. Mchakato wa kuthibitisha unaweza kuchukua takribani siku 2 hadi 10, kulingana na njia ya kupokea malipo ambayo umechagua.

  Kiasi utakacholipwa

  Ili kupiga hesabu ya malipo yako, weka malipo yoyote ya ziada ya hiari (kama vile ada yako ya usafi au ada ya mgeni wa ziada) kwenye bei yako ya kila usiku. Hii ndiyo jumla yako ndogo.

  Ukiisha kupata jumla yako ndogo, toa ada na kodi zinazotumika. Ingawa kodi zinaweza kutofautiana kulingana na mahali unapoishi, Wenyeji wengi hulipa ada ya huduma ya asilimia 3. Ada hii huisaidia Airbnb kulipia gharama za bidhaa na huduma tunazotoa (kama vile usaidizi kwa wateja wa saa 24!) na hesabu yake hufanywa kutokana na jumla ndogo ya nafasi iliyowekwa.

  Kumbuka kuwa mapato yako yatatofautiana kulingana na urefu wa ukaaji wa mgeni, mapunguzo yoyote uliyoweka, n.k. Ikiwa malipo yako yamechelewa au yanaonekana kuwa chini kuliko ulivyotarajia, pengine ni kwa sababu ya nafasi iliyowekwa ambayo ilighairiwa au kubadilishwa na ambayo ilisababisha mgeni wako kurejeshewa fedha zote au sehemu ya fedha.

  Wakati ambapo utalipwa

  Pesa unayopata kutoka kwenye huduma ya kukaribisha wageni kwa kawaida itatumwa kwako saa 24 baada ya muda ulioratibiwa wa kuingia kwa mgeni wako. Muda halisi ambao fedha zitafika kwenye akaunti yako utategemea njia ya kupokea malipo ambayo umechagua.

  Kwa mfano, pesa kwa kawaida hufika kwenye akaunti yako ndani ya siku 7 za kazi kwa malipo kwa njia ya benki na ndani ya siku 1 ya kazi kwa kadi za PayPal na Payoneer—ingawa wakati halisi unategemea akaunti yako iko wapi. Unapokaribisha wageni kwenye sehemu ya kukaa ya muda mrefu (usiku 28 au zaidi), kwa ujumla Airbnb itatuma mapato kwa awamu za kila mwezi, kuanzia saa 24 baada ya mgeni wako kuwasili.

  Unaweza kuangalia hali ya malipo yako katika Historia yako ya Muamala wakati wowote.

  Taarifa zilizo ndani ya makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Vidokezi

  Airbnb
  12 Feb 2020
  Ilikuwa na manufaa?