Wageni wanatoka kila pembe ya kila bara, wakitumia Airbnb katika lugha zaidi ya 60. Kuweka maelezo ya tangazo lako katika lugha moja au zaidi hufanya iwe rahisi kwa watu kutoka nchi tofauti au wanaozungumza lugha tofauti kupata na kuweka nafasi kwenye sehemu yako.
Mara baada ya kuweka lugha, unaweza kuandika maelezo katika lugha hiyo kwa ajili ya tangazo lako. Kwa jambo jingine lolote, wageni wataonyeshwa tafsiri za kiotomatiki.
Unaweza pia kubadilisha lugha ya akaunti yako ya Airbnb ikiwa unataka.