Faragha

Katika Airbnb, tunataka kujenga ulimwengu ambapo mtu yeyote anaweza kujisikia nyumbani mahali popote – na hatua ya kwanza katika mwelekeo huo ni kutengeneza jumuiya yenye uwazi, jumuishi na ambayo msingi wake ni uaminifu. Sehemu ya msingi ya kupata uaminifu huo inamaanisha kuwa wazi kuhusu jinsi tunavyotumia taarifa yako na kulinda haki yako ya binadamu ya faragha. Tunajua inaweza kutisha wakati kampuni zinatumia taarifa yako, kwa hivyo tumeweka sera na mazoea madhubuti ambayo yanaheshimu faragha yako katika sehemu halisi na za kidijitali za maisha yako.

Kanuni zetu za faragha

Kujizatiti kwetu kwa faragha kunaonyeshwa katika kanuni ambazo zinatuongoza katika kufanya maamuzi tunapojitahidi kila mara kupata uaminifu wako.

Kwa faida yako

Tunatumia data kuwezesha uzoefu wako na kukuweka salama. Hatumuuzii mtu yeyote data yako binafsi.

Uwazi

Tuna uwazi kuhusu jinsi tunavyokusanya na kutumia data yako binafsi.

Udhibiti

Tunakuweka udhibiti data yako binafsi.

Usalama

Tunalinda data binafsi unayotukabidhi kupitia hatua madhubuti za usalama.
Kwa taarifa za kina kuhusu data tunayokusanya, jinsi tunavyoitumia na jinsi ya kutumia haki zako kuhusu data yako, tafadhali tathmini sera yetu ya faragha.