Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sera ya jumuiya

Sera ya Maudhui ya Airbnb

Kwa kuchapisha maudhui kwenye Airbnb, unakubali kufuata sera hii. Tuna haki ya kuondoa maudhui yoyote, yote au kwa sehemu, ambayo yanakiuka sera hii, Masharti yetu ya Huduma, Miongozo yetu ya Jumuiya, Sera yetu ya Tathmini, au kwa sababu nyingine yoyote kwa busara yetu wenyewe.

Katika hali ambapo kuna ukiukaji wa tena na tena au mbaya sana, tunaweza kusimamisha au kulemaza kabisa akaunti inayohusika (zinazohusika).

Unaweza kuripoti maudhui hayo moja kwa moja au uwasiliane nasi ili kuripoti maudhui ambayo yanaonekana kukiuka sera hii.

Maudhui yafuatayo hayaruhusiwi kwenye Airbnb:

 • Maudhui yaliyoundwa kwa lengo tu la kutangaza au kufanya maudhui mengine ya biashara, pamoja na nembo za kampuni, viunganishi au majina ya kampuni
 • Baruataka, mawasiliano yasiyotakiwa, au maudhui ambayo yanashirikiwa tena na tena kwa njia yenye kuvuruga
 • Maudhui yanayoidhinisha au kutangaza shughuli haramu au zenye madhara, au ambayo yanaonyesha mambo ya ngono waziwazi, yenye ukatili, dhahiri, kutishia, au kusumbua
 • Maudhui ya ubaguzi (tathmini Sera yetu ya Kutobagua kwa taarifa zaidi)
 • Majaribio ya kujifanya mtu mwingine, kuiga akaunti, au taasisi, ikiwemo mwakilishi wa Airbnb
 • Maudhui haramu au yanayokiuka haki za mtu mwingine au taasisi, ikiwemo haki miliki na haki za faragha
 • Maudhui yanayojumuisha taarifa binafsi au ya faragha ya mtu mwingine, ikiwemo maudhui yanayotosha kutambulisha eneo la tangazo

Pata maelezo zaidi kuhusu Sera ya Airbnb ya Maudhui na Virusi vya Korona.

Ukiukaji wa sera

Ufuatao ni ukiukaji wa sera mahususi kwa aina ya maudhui:

Vichwa vya tangazo

 • Vichwa vya tangazo ambavyo vinajumuisha taarifa isiyohusiana na aina ya tangazo, mtindo, au tukio
 • Vichwa vya tangazo ambavyo vinajumuisha alama au emoji

Kurasa za tangazo au wasifu

 • Matangazo na wasifu ambazo hutoa taarifa za ulaghai, za uwongo, au za kupotosha

Kituo cha Jumuiya

 • Maudhui yaliyo nje ya mada, yasiyouliza swali, au yasiyotoa maarifa kwa kujibu swali kama sehemu ya mazungumzo mapana
 • Kuchokoza au kulenga wanajumuiya kwa kurudiarudia

Tathmini

 • Tathmini za kibaguzi au zinazoonyesha dalili za vitisho/kuhimiza, migongano ya masilahi, au mashindano ya moja kwa moja
 • Tathmini ambazo hazina taarifa inayomhusu mwenyeji au mgeni, tangazo, au tukio zinaweza kuondolewa. Tathmini ambazo zina taarifa nyingi zisizo na uhusiano pia zinaweza kuondolewa, lakini katika hali tu ambapo taarifa ambayo inahusika haitarajiwi kutoa taarifa ya maana kuhusu uamuzi wa kuweka nafasi wa wanajumuiya wengine.

Pata maelezo zaidi kuhusu Sera ya Tathmini ya Airbnb na jinsi ambavyo Airbnb inapatanisha mabishano ya tathmini.

URL Mahususi

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili