Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Masharti ya kisheria
Mgeni

Mpango wa Usaidizi wa Wageni wa COVID

Mpango wa Usaidizi wa COVID wa Airbnb (“Mpango”), uliotangazwa mwezi Januari mwaka 2022, ulianzishwa ili kutoa msaada kwa wageni ambao nafasi walizoweka za sehemu za kukaa zimetatizwa na vizuizi vya hivi majuzi vya usafiri vya serikali vinavyohusiana na COVID ambavyo vimeelezwa hapa chini.

Airbnb inafurahi kufadhili Mpango huu kwa USD milioni 20, ambazo zitatolewa kwa uamuzi wetu pekee ili kuwasaidia wageni wanaokabiliwa na changamoto hizi zisizo za kawaida. Mpango huu utaisha wakati pesa zote za Mpango zitakuwa zimegawanywa au tarehe 30 Aprili, 2022, chochote kitakachotangulia.

Hali zinazolindwa na Sera ya Sababu Zisizozuilika ya Airbnb hazistahiki chini ya Mpango huu (ikiwemo pale ambapo mgeni anaugua COVID-19)

Nafasi zilizowekwa ambazo zimeghairiwa zinazostahiki

Nafasi zilizowekwa ambazo zimeghairiwa lazima zitimize vigezo vyote vifuatavyo:

 • Nafasi iliyowekwa ya sehemu ya kukaa iliyo na tarehe ya kuingia ambayo ni mnamo au baada ya tarehe 1 Desemba, 2021;
 • Ilighairiwa na mgeni (a) mnamo au baada ya tarehe 1 Desemba, 2021, (b) kabla ya kuingia na ndani ya siku 45 baada ya kuingia na (c) mnamo au kabla ya tarehe ya mwisho ya Mpango na
 • Ilighairiwa kwa sababu ya kizuizi cha usafiri kinachostahili ambacho kiliidhinishwa na serikali, kilichotokea baada ya muda wa kuweka nafasi.

Aina za vizuizi vya usafiri vilivyoidhinishwa na serikali ambavyo vimeshughulikiwa

Vizuizi vifuatavyo vya usafiri vinavyohusiana na COVID pekee ndivyo vinavyoshughulikiwa:

 • Agizo la kufungwa kwa mpaka, kutotoka mahali ulipo au amri ya kusitisha shughuli za kawaida ambalo linakataza:
  • Usafiri wote wa kuingia usio wa lazima unaoelekea mahali anakoenda mgeni au
  • Usafiri wote wa kuelekea kwingine usio wa lazima kutoka kwenye eneo anakotoka mgeni;
 • Takwa jipya au lililoongezwa muda kwamba wasafiri wote kutoka eneo lao la asili lazima wawekwe karantini au wajitenge watakapofika mahali wanakoenda.

Hii inajumuisha hali ambapo takwa la karantini katika mahali wanakoenda lilikuwepo wakati wa kuweka nafasi, lakini lilipanuliwa au kuongezwa muda baada ya kuweka nafasi na kabla ya tarehe ya kuingia. Kwa mfano, ikiwa takwa la karantini ya siku 7 katika mahali wanakoenda lilitumika wakati wa kuweka nafasi, lakini baadaye likaongezwa muda hadi siku 14, nafasi iliyowekwa inaweza kustahiki.

Hii haijumuishi hali ambapo takwa la karantini au la kujitenga linatumika tu kwa mgeni mahususi (au kundi la wageni) na si kwa wasafiri wote ambao safari zao si za lazima kutoka eneo la asili. Pia haijumuishi hali ambapo mgeni anahitajika kuwekwa karantini au kujitenga katika eneo la asili kabla ya kusafiri kwenda mahali anakoenda (kwa mfano, kwa sababu anachukuliwa kuwa aliyekaribiana na mtu aliyeambukizwa COVID-19).

Kumbuka kwamba Mpango huu unatumika tu kwa vizuizi vya usafiri ambavyo havikuwepo wakati wa kuweka nafasi. Kwa mfano, ikiwa mgeni anayesafiri kwenda Israeli aliweka nafasi mwezi Oktoba — kabla ya Israeli kuanza kuweka vizuizi vya usafiri wa kuingia kwa sababu ya Omicron — yenye tarehe ya kuingia iliyo mwezi Desemba, nafasi hiyo iliyowekwa itastahiki chini ya Mpango huu. Hata hivyo, ikiwa vizuizi hivyo vya usafiri vilikuwepo tayari wakati mgeni alipoweka nafasi ya sehemu hiyo ya kukaa, hangestahiki kupata msaada chini ya Mpango huu.

Aina za nafasi zilizowekwa ambazo hazistahiki

Nafasi zifuatazo zilizowekwa hazistahiki kupata msaada chini ya Mpango huu:

 • Nafasi zilizowekwa za Airbnb Luxe
 • Nafasi zilizowekwa za Airbnb Kikazi
 • Nafasi zilizowekwa za Matukio
 • Nafasi zilizowekwa na wageni wanaoishi China Bara

Kutuma ombi la msaada

Ikiwa nafasi iliyowekwa inakidhi vigezo vya ustahiki vilivyotajwa hapo juu, mgeni aliyeweka nafasi anaweza kuwasiliana na timu yetu ya Usaidizi wa Jumuiya inayopatikana saa 24 na atahitajika kutoa taarifa inayoonyesha kustahiki kwake. Ni lazima tupokee ombi lolote la usaidizi ndani ya siku 90 baada ya tarehe ya nafasi iliyowekwa kughairiwa.

Iwapo tutagundua ulaghai wowote, udanganyifu au ukiukaji mwingine wa Masharti yetu ya Huduma au Masharti ya Huduma ya Malipo, Airbnb ina haki ya kukataa ombi, kuondoa msaada, kusimamisha au kusitisha akaunti ya mgeni au kuchukua hatua nyingine zinazofaa za kisheria.

Aina ya msaada unaopatikana

Iwapo fedha za Mpango bado zinapatikana na tukibainisha kwamba nafasi iliyowekwa inastahili kupata msaada, mgeni aliyeweka nafasi atastahiki kupokea kuponi ya usafiri itakayotumika mara moja ya asilimia 50 ya sehemu ya fedha ambazo hazikurejeshwa ya nafasi hiyo iliyowekwa. Kwa mfano, ikiwa mgeni alighairi nafasi iliyowekwa ya USD500 na kurejeshewa USD250 chini ya sera ya kughairi ya Mwenyeji, mgeni huyo atastahiki kupokea kuponi ya usafiri ya USD125 (asilimia 50 ya sehemu ya fedha ambazo hazikurejeshwa). Malipo ambayo Mwenyeji anapokea kwa nafasi hiyo iliyowekwa hayataathiriwa.

Airbnb inatarajia kutathmini maombi kwa utaratibu tunaoyapokea. Kuponi zote za usafiri zinazotolewa chini ya mpango huu zinategemea upatikanaji wa fedha ndani ya Mpango.

Wakati utapata kuponi yako ya usafiri

Tukibaini kwamba nafasi iliyowekwa inastahiki kupata msaada na kwamba fedha za Mpango bado zinapatikana, kuponi ya usafiri inapaswa kufika kwenye akaunti ya mgeni ndani ya siku 7-10 za kazi. Wageni wanaweza kutazama kuponi za usafiri chini ya Wasifu > Mipangilio ya Akaunti > Malipo na kupokea malipo > Masalio na kuponi.

Kuomba kuponi nyingi za usafiri

Ikiwa mgeni ana zaidi ya nafasi moja iliyowekwa inayostahiki, anaweza kuwasilisha ombi kwa kila nafasi iliyowekwa inayostahiki. Airbnb ina haki ya kuweka kikomo kwenye idadi ya kuponi za usafiri zinazotolewa kwa mgeni mmoja chini ya Mpango huu.

Masharti ya kuponi za usafiri

Kuponi ni ya matumizi ya mara moja na kuponi isiyorejeshewa fedha ambayo inaweza kutumika tu kwa nafasi iliyowekwa ya sehemu ya kukaa yenye tarehe ya kuingia ambayo ni mnamo au kabla ya tarehe 30 Desemba, 2023. Ni halali tu kwa nafasi iliyowekwa ya sehemu ya kukaa kwenye Airbnb. Ikiwa nafasi iliyowekwa kwa kutumia kuponi itaghairiwa na mgeni, kuponi hiyo haitakuwa halali tena. Kuponi hiyo haiwezi kukombolewa kwa pesa taslimu au kadi za zawadi au kutumiwa kwenye ununuzi wa awali na haiwezi kuhamishwa au kuunganishwa na ofa nyingine, kuponi au punguzo. Airbnb ina haki ya kutumia njia yoyote, ikiwemo kufutilia mbali kuponi hii, katika visa vya tuhuma za ulaghai, matumizi mabaya, ukiukaji wa Masharti yetu ya Huduma au Masharti ya Huduma ya Malipo au hitilafu za kiufundi.

Jinsi Mpango unavyofanya kazi

Airbnb ilianzisha Mpango wa Usaidizi wa Wageni wa COVID ili kusaidia jumuiya yetu ya wageni wakati wa ongezeko la hivi karibuni la visa vya COVID-19 kote ulimwenguni. Vipengele vyote vya Mpango huu viko kwa hiari yetu, ikiwemo kustahiki kwa wageni. Maamuzi ya Airbnb chini ya Mpango huu ni ya mwisho na ni shuruti kwa wageni lakini hayaathiri haki nyingine za kimkataba au za kisheria wanazoweza kuwa nazo, kama vile chini ya Sera yetu ya Kurejesha Fedha ya Mgeni, Sera ya Sababu Zisizozuilika au sera ya kughairi ya Mwenyeji kwa nafasi iliyowekwa. Haki yoyote ambayo mgeni anaweza kuwa nayo ya kuchukua hatua za kisheria haiathiriwi.

Tafadhali rejelea ukurasa huu kwa maelezo ya hivi punde kuhusu Mpango na tutachapisha habari za hivi karibuni Mpango utakapokamilika. Nafasi zilizowekwa ambazo zilighairiwa mnamo au kabla ya tarehe ya mwisho ya Mpango ndizo zitakazotastahiki msaada pekee. Kadiri janga la ugonjwa linavyoendelea kubadilika na hali kubadilika, tutafuatilia Mpango na tunaweza kuongeza muda, kuondoa kwa muda, kurekebisha au kusitisha Mpango kwa hiari yetu.

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili