Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Sera ya Sababu Zisizozuilika na virusi vya korona (COVID-19)

  ImesasishwaTarehe 1 Oktoba, 2020

  Mnamo Machi 11, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilitangaza kuzuka kwa ugonjwa wa virusi vya korona, unaojulikana kama COVID-19, kuwa janga la ulimwengu. Tangu wakati huo, mlipuko huo umeenea haraka huku serikali ulimwenguni kote zikichukua hatua za haraka ili kupunguza kuenea kwa COVID-19.

  Kwa sababu hiyo, tunachukua hatua hizi ili kujumuisha ugonjwa wa COVID-19 chini ya sera yetu ya sababu zisizozuilika ili kusaidia kuilinda jumuiya yetu na kuleta utulivu wa akili. Tafadhali angalia ukurasa huu mara kwa mara kwa mabadiliko kuhusu ujumuishaji.

  Kidokezi: Ikiwa wewe ni mgeni, unaweza kupata machaguo ya kughairi na kurejesha fedha kwa kwenda kwenyeUkurasa wa Safari na kuchagua safari yako-jua jinsi ya kufanya. Ikiwa wewe ni mwenyeji, utapata taarifa katika dashibodi yako ya kukaribisha wageni.

  Muhtasari

  Nafasi kwa ajili ya sehemu za kukaa na Matukio ya Airbnb zilizowekwa mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi, 2020, zenye tarehe ya kuingia iliyo ndani ya siku 45 zijazo kuanzia leo, zinashughulikiwa na sera hiyo na zinaweza kughairiwa kabla ya kuingia. Wageni ambao wanaghairi watakuwa na machaguo ya kughairi na kurejeshewa fedha na wenyeji wanaweza kughairi bila malipo au athari kwa hadhi yao ya Mwenyeji Bingwa. Airbnb itarejesha fedha, au itatoa salio la safari ambalo linajumuisha ada zote za huduma kwa ughairi unaoshughulikiwa. Ili ughairi chini ya sera hiyo, utatakiwa kuthibitisha ukweli wa na/au kutoa hati za ushahidi wa sababu zako zisizozuilika.

  Sera ya kughairi ya mwenyeji itatumika kama kawaida kwa nafasi zilizowekwa baada ya tarehe 14 Machi, 2020.

  Kughairi kutashughulikiwa kulingana na bima ya sababu zisizozuilika inayotumika wakati wa kuwasilisha, nafasi zilizowekwa ambazo zilikuwa zimeghairiwa tayari hazitazingatiwa tena.

  Ikiwa nafasi iliyowekwa tayari imekwishaanza (muda wa kuingia umepita) sababu hii isiyozuilika haitumiki

  Sera tofauti zinatumika kwa nafasi zilizowekwa nchini China bara na kwa nafasi zilizowekwa za Luxe au Luxury Retreats.

  Nafasi zilizowekwa ambazo zimejumuishwa

  Nafasi zilizowekwa mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi, 2020

  Nafasi za sehemu za kukaa na Matukio ya Airbnb zilizowekwa mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi, 2020, zenye tarehe ya kuingia kati ya tarehe 14 Machi, 2020 na tarehe ya kuingia iliyo ndani ya siku 45 kuanzia leo, zinaweza kughairiwa kabla ya kuingia. Hii inamaanisha kuwa wageni ambao wanaghairi chini ya sera hiyo watarejeshewa fedha zote taslimu au salio la safari kwa kiasi walicholipa (ambapo salio la safari linapatikana), wenyeji wanaweza kughairi chini ya sera hiyo bila malipo au athari kwa hadhi yao ya Mwenyeji Bingwa na Airbnb itarejesha fedha au kutoa salio la safari kwa kiasi ambacho kinajumuisha ada zote za huduma.

  Nafasi za sehemu za kukaa na Matukio ya Airbnb zilizowekwa mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi, 2020, zenye tarehe ya kuingia ya zaidi ya siku 45 kuanzia leo, kwa sasa hazishughulikiwi na sababu zisizozuilika zinazohusiana na COVID-19. Sera ya kughairi ya mwenyeji itatumika kama kawaida.

  Ikiwa nafasi iliyowekwa tayari imeanza (tarehe ya kuingia imepita) sababu hii isiyozuilika haitatumika.

  Nafasi zilizowekwa baada ya tarehe 14 Machi, 2020

  Nafasi za sehemu za kukaa na Matukio ya Airbnb zilizowekwa baada ya tarehe 14 Machi, 2020 hazitashughulikiwa chini ya sera yetu ya sababu zisizozuilika, isipokuwa ambapo mgeni au mwenyeji anaugua COVID-19. Hali zinazohusiana na COVID-19 ambazo hazishughulikiwi ni pamoja na: kuvurugwa kwa safari na kughairi; ushauri na vizuizi vya safari; ushauri wa kiafya na karantini; mabadiliko katika sheria inayotumika; pamoja na maagizo mengine ya serikali—kama vile amri za kuhamisha watu, kufungwa kwa mipaka, marufuku ya kukodisha nyumba kwa muda mfupi na matakwa ya kuwataka watu wasitoke maeneo walipo. Sera ya mwenyeji ya kughairi itatumika kama kawaida.

  Sera yetu ya sababu zisizozuilika imekusudiwa kuwalinda wageni na wenyeji dhidi ya hali ambazo hazikutarajiwa ambazo hutokea baada ya kuweka nafasi. Baada ya tamko la Shirika la Afya Duniani kwamba ugonjwa wa COVID-19 ni janga la kimataifa, sera ya sababu zisizozuilika haitatumika tena kwa sababu COVID-19 na athari zake hazipo tena miongoni mwa mambo yasiyotabirika au yasiyotarajiwa. Tafadhali kumbuka kutathmini kwa uangalifu sera ya mwenyeji ya kughairi wakati wa kuweka nafasi na uzingatie chaguo ambalo linakubali mabadiliko.

  Jinsi inavyofanya kazi

  Ikiwa wewe ni mgeni, unaweza kupata machaguo ya kughairi na kurejesha fedha kwa kwenda kwenyeUkurasa wa safari kisha kuchagua safari yako-jua jinsi ya kufanya. Ikiwa wewe ni mwenyeji, utapata taarifa katika dashibodi yako ya kukaribisha wageni.

  Habari za hivi punde na nyenzo za virusi vya korona

  Tumekusanya na kuhariri makala ya kusaidia jumuiya yetu katika wakati huu kwenye Kituo cha Nyenzo. Unaweza kupata taarifa za hivi karibuni kuhusu juhudi zetu za kupambana na COVID-19, kuanzia mabadiliko kwenye sera hadi nyenzo kwa ajili ya wenyeji na wageni.

  Unaweza pia kusoma sera ya sababu zisizozuilika ili kupata maelezo zaidi kuhusu ujumuishaji wa hali zisizohusiana na COVID-19.

  Tunawaomba wanajumuiya wote wakumbuke heshima, ujumuishaji na sera yetu ya kutobagua wanapoingiliana na wanajumuiya wetu wengine.

  Tutaendelea kutathmini matumizi ya sera hii. Tafadhali angalia ukurasa huu mara kwa mara kwa habari za hivi punde na taarifa mpya.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana