Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sera ya jumuiya

Usalama wa Wenyeji na wageni

Ili kusaidia kuhakikisha ukaaji salama, matukio na maingiliano, shughuli na tabia fulani haziruhusiwi katika jumuiya yetu.

Kile tunachoruhusu

  • Kujilinda: Ikiwa umeshambuliwa kimwili katika sehemu ya kukaa au Tukio, unaruhusiwa kujilinda kwa nguvu stahili hadi hatari itakapokoma.
  • Silaha zinazoruhusiwa: Isipokuwa vifaa vya kulipuka au vya kusababisha moto na silaha za kushambulia, kama mgeni, unaweza tu kuwenda na silaha zinazomilikiwa kisheria au silaha zisizo za kufisha ikiwa zimelindwa kwa usalama na kufichuliwa kwa Mwenyeji wako kabla ya kuwasili. Kama Mwenyeji, unaweza kuweka silaha zinazomilikiwa kisheria katika nyumba yako maadamu zimehifadhiwa salama; lazima silaha zifichuliwe ikiwa zimewekwa katika eneo la wazi au kwa njia ambayo zinaweza kugunduliwa na wageni. Pata maelezo zaidi kuhusu sheria zetu zinazohusu silaha kwenye nyumba.

Kile ambacho haturuhusu

  • Vitisho au unyanyasaji: Vitisho, ukatili, au unyanyasaji dhidi ya wengine, ikiwemo wenzi wa ndoa, watoto, wanyama, na watu wagonjwa au walemavu, havina nafasi katika jumuiya yetu.
  • Ukatili wa kingono na mwenendo mbaya: Ukatili wa kingono na mwenendo mbaya wa aina yoyote umepigwa marufuku. Tabia zozote za kugusa bila ridhaa au bila kuombwa, tabia za kimapenzi au ngono, au mazungumzo ya uhusiano binafsi au mapendeleo ya kingono hazikubaliki.
  • Wanyama hatari au haramu: Mnyama yeyote ambaye uzao wake au spishi yake ni haramu kumiliki katika eneo la tangazo au Tukio umepigwa marufuku. Wanyama wa nyumbani, shambani, na porini ambao wanaweza kuleta hatari ya usalama katika nafasi iliyowekwa lazima walindwe vizuri na kufichuliwa wazi. Wanyama ambao hawajaonyesha dalili za kuleta hatari hawahitaji kufichuliwa kwani nyenzo ya ufichuzi ni kwa ajili ya "wanyama hatari." Pata maelezo zaidi kuhusu sheria zetu zinazowahusu wanyama hatari.
  • Vifaa vya kulipuka, vifaa vya kusababisha moto, au silaha za kushambulia: Vitu hivi haviruhusiwi katika sehemu ya kukaa au Tukio, hata ikiwa ni halali kuwa navyo katika eneo lako.
  • Silaha zisizo salama/zisizojulikana. lazima silaha zozote zinazomilikiwa kisheria zifichuliwe vizuri na kulindwa salama.

Tuko hapa kukusaidia

Ikiwa kuna jambo la dharura linaloendelea, tafadhali wasiliana na huduma za dharura za eneo lako au mamlaka za utekelezaji wa sheria ili upate usaidizi.

Kwa matatizo mengine ya usalama, tunapatikana saa 24 kwa siku. Soma zaidi kuhusu jinsi ya kuwasiliana nasi katika Kituo chetu cha Msaada.

Tunachukulia vitisho vya kujiua na kujidhuru kwa uzito sana na tunaweza kuwasiliana na mamlaka ili kuomba ukaguzi wa afya ikiwa tumejulishwa kwamba kuna hatari ya usalama inayokaribia. Ikiwa wewe au mtu mwingine anahisi kutishiwa au hayuko salama, tafadhali wasiliana kwanza na mamlaka za utekelezaji wa sheria za eneo lako ili upate usaidizi.

Kama kawaida, ikiwa unashuhudia au unatendewa kwa namna ambayo inakwenda kinyume cha masharti au sera zetu, tafadhali tujulishe.

Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa ili kutoa mwongozo wa jumla kwa sera za jumuiya za Airbnb.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili