Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sheria
Mwenyeji

Sheria na kodi za eneo lako

Kuwa tayari ni muhimu. Tunataka kuhakikisha kwamba una kila kitu unachohitaji ili safari yako ya kukaribisha wageni ianze vizuri na hiyo inajumuisha kutathmini sheria na kanuni za eneo husika unapotangaza eneo lako.

Mambo ambayo majiji mengine yanaweza kuyahitaji

Majiji mengi yana sheria zinazoshughulikia upangishaji wa nyumba na kanuni na maagizo mahususi yanaweza kupatikana katika maeneo mengi (kama vile sheria za ugawanyaji wa maeneo, ujenzi, utoaji leseni au kanuni za kodi).

Katika baadhi ya maeneo, unaweza kuhitajiwa ujisajili, upate kibali ama upate leseni kabla ya kutangaza eneo lako au kukubali wageni. Pia unaweza kuwajibika kukusanya na kutoa kodi fulani.

Wajibu wako kama Mwenyeji

Unawajibika kujua ni wapi, wakati gani na jinsi gani unakaribisha wageni, kwa hivyo tunataka usiwe na wasiwasi kuhusu sheria na kodi za eneo husika. Unaweza kuwasiliana na serikali ya eneo lako ukiwa na maswali yoyote.

Ili uanze, tunatoa nyenzo muhimu kuhusu kukaribisha wageni kwa kuwajibika.

Tunakuomba ujielimishe kuhusu sheria na taratibu katika eneo lako kisha utathmini Sera yetu ya Kutobagua kabla ya kutangaza eneo lako. Unapokubali Masharti yetu ya Huduma na kutangaza eneo lako, unathibitisha kwamba utafuata sheria na taratibu zinazotumika.

Ikiwa wewe ni Mwenyeji nchini Ufaransa, unathibitisha kuwa utafuata sheria zinazotumika na makubaliano yoyote yaliyofanywa na wahusika wengine (mfano: mkataba wa kupangisha).

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili