Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Matakwa ya afya na usalama kwa ajili ya sehemu za kukaa za Airbnb

  Wakati wa janga la COVID-19, ni muhimu kuzingatia afya na usalama. Tumetengeneza mkusanyo wa mazoea ya usalama ya lazima ya COVID-19 kwa ajili ya Wenyeji na wageni wa matangazo ya Airbnb, kulingana na mwongozo kutoka kwenye Shirika la Afya Duniani na Vituo vya Marekani vya Kudhibiti Magonjwa. Aidha, unapaswa kufahamu mazoea ya jumla ya afya na usalama kwa ajili ya usalama wa COVID-19, uendelee kufuatilia vizuizi husika vya kusafiri na ushauri wa serikali na ufuate sheria zote za kitaifa na za eneo husika na miongozo.

  Airbnb imeanzisha miongozo na mipango ya kusaidia kushughulikia wasiwasi wa kiafya na usalama, lakini hatua hizi haziwezi kuondoa hatari zote. Hasa ikiwa uko katika kundi linalokabili hatari kubwa (mfano: watu wenye umri wa zaidi ya miaka 65 au watu walio na matatizo ya afya kama vile kisukari au ugonjwa wa moyo), tunapendekeza upate mwongozo wa kitaalamu na uchukue tahadhari za ziada unapofanya uamuzi wa kuweka nafasi ya sehemu ya kukaa au ya tukio kwenye Airbnb. Pata maelezo zaidi kuhusu miongozo ya afya na usalama kwa ajili ya Wenyeji wa Matukio ya Airbnb na wageni.

  Mazoea ya usalama ya COVID-19 (inahitajika)

  Vaa barakoa na uepuke mikusanyiko unapohitajiwa kufanya hivyo na sheria na miongozo ya eneo husika

  Wanapohitajiwa na sheria na miongozo ya eneo husika, Wenyeji wote na wageni lazima wakubali:

  • Vaa barakoa au kifuniko cha uso unaposhirikiana na watu ana kwa ana
  • Dumisha umbali wa futi 6/mita 2 kutoka kwa watu wengine nyakati zote

  Fuata mchakato wa hatua 5 wa Airbnb wa kufanya usafi wa kina baada ya mgeni kutoka na kabla ya mwingine kuingia

  Wenyeji wote na wageni wanahitajika kufuata mazoea ya usalama ya COVID-19 yaliyoainishwa hapo juu, kama inavyohusika, ikiwemo mchakato wa hatua 5 wa Airbnb wa kufanya usafi wa kina baada ya mgeni kutoka na kabla ya mwingine kuingia. Wenyeji ambao hawakubaliani na mazoea haya, kalenda zao zinaweza kuzuiwa. Mwenyeji au mgeni yeyote ambaye anakiuka mara kwa mara miongozo hii anaweza kukabiliwa na athari nyingine, ikiwemo kusimamishwa kwa akaunti au kuondolewa kwenye jumuiya.

  Mwongozo wa ziada wa kusafiri na kukaribisha wageni wakati wa COVID-19

  Usisafiri au kukaribisha wageni ikiwa hivi karibuni umekuwa katika hali ya kuweza kuambukizwa au ikiwa una dalili za COVID-19

  Ili kulinda afya na usalama wa jumuiya yetu, ni sera ya Airbnb kwamba Wenyeji (na watu wote ambao wanaweza kuwapo kwenye nyumba kabla au wakati wa ukaaji) hawapaswi kuingia kwenye nyumba yao (zao) au kushirikiana na wageni wao na wageni hawapaswi kuingia kwenye nyumba iwapo lolote kati ya mambo yafuatayo ni kweli:

  • Umeambukizwa au umepimwa na kupatikana kuwa na COVID-19 katika siku 14 zilizopita
  • Unashuku kuwa wewe ni mgonjwa au umekuwa katika hali ya kuweza kuambukizwa na unasubiri matokeo ya kipimo ili kuthibitisha au kukataa utambuzi wa COVID-19
  • Unaonyesha dalili au una wasiwasi kuhusu uwezekano wa kuambukizwa COVID-19
  • Umekuwa na mtagusano wa karibu, ulio endelevu na mtu aliyethibitishwa au kushukiwa kuambukizwa COVID-19, ndani ya siku 14 zilizopita*

  Kwa maelezo zaidi kuhusu nini cha kufanya endapo una ugonjwa au umekuwa katika hali ya kuweza kuambukizwa COVID-19, tathmini hati zifuatazo:

  *Tafadhali kumbuka kuwa Sehemu za Kukaa za Mstari wa Mbele zinadhibitiwa na viwango tofauti.

  Nawa mikono mara kwa mara

  Hakikisha unanawa mikono mara nyingi, hasa ikiwa unaingiliana na watu ambao hamkai nao kwenye nafasi iliyowekwa na unagusa sehemu mbalimbali na vyombo vilivyo katika sehemu ya pamoja au eneo la pamoja.

  • Nawa mikono vizuri kwa sabuni na maji kwa angalau sekunde 20
  • Ikiwa sabuni na maji hazipatikani kwa urahisi, tumia kitakasa mikono kilicho na alkoholi ya angalau asilimia 60; pakaza mikono yako na uisugue pamoja hadi ikauke

  Fuata sheria au miongozo ya eneo lako kuhusu barakoa na kuepuka mikusanyiko katika maeneo ya pamoja na sehemu za pamoja

  Unapokuwa katika eneo au sehemu ya pamoja (kama Mwenyeji au mgeni), fuata sheria na miongozo ya eneo lako kuhusu kuvaa barakoa na kuepuka mikusanyiko kutoka kwa mtu yeyote ambaye hakai kwenye nafasi uliyoweka. Wenyeji wanapaswa kuzingatia kutoa huduma ya kuingia bila kukutana ana kwa ana pale inapowezekana.

  Kumbuka, ikiwa una wasiwasi kuhusu kukaa kwenye chumba cha kujitegemea au sehemu ya pamoja, zingatia kuweka nafasi ya nyumba nzima badala yake. Ikiwa una wasiwasi kuhusu kukaribisha wageni kwenye chumba cha kujitegemea au sehemu ya pamoja, unaweza kutangaza nyumba nzima, au usitishe shughuli ya kukaribisha wageni ikiwa hiyo haiwezekani.

  Wenyeji wanapaswa pia kufuata miongozo ya eneo husika kuhusu kukaribisha wageni kwenye vyumba vya kujitegemea, sehemu za pamoja na jumla ya idadi ya watu wanaoruhusiwa kukusanyika kwenye nyumba hiyo.

  Arifa: Kufikia tarehe 20 Agosti, 2020, Airbnb imetangaza marufuku ya kimataifa kwa sherehe na hafla zote kwenye matangazo ya Airbnb, pamoja na kikomo cha idadi ya wakaaji 16. Marufuku haya ya sherehe yanatumika kwa nafasi zote zitakazowekwa katika siku zijazo kwenye Airbnb na yataendelea kuwepo kwa muda usiojulikana, mpaka itakapotangazwa vinginevyo. Soma Sera yetu ya Karamu na Hafla kwa taarifa zaidi.

  Miongozo ya ziada kwa ajili ya Wenyeji wa vyumba vya kujitegemea na sehemu za pamoja

  Wenyeji wa matangazo ya chumba cha kujitegemea au sehemu ya pamoja wanapaswa pia:

  • Kuweka kikomo cha idadi ya wageni kama inavyohitajiwa ili kuruhusu uepukaji wa mikusanyiko katika maeneo yote ya pamoja pale ambapo sheria au miongozo ya eneo husika inahitaji kufanya hivyo
  • Kufanya hewa izunguke kwenye maeneo ya pamoja wakati wa ukaaji, pale ambapo ni salama kufanya hivyo, kama ilivyoainishwa katika itifaki ya kufanya usafi
  • Kusafisha na kutakasa maeneo ya pamoja (kama vile mabafu na majiko) mara nyingi kadiri iwezekanavyo

  Baadhi ya serikali zinaweza kuweka vizuizi katika kukaribisha wageni kwenye vyumba vya kujitegemea au vya pamoja au zinaweza kuweka majukumu au matakwa ya ziada kwenye sehemu hizo. Tafadhali hakikisha unatathmini na kufuata mwongozo wowote wa ziada wa usalama na usafishaji kutoka serikalini na/au mamlaka za afya katika eneo lako.

  Nini cha kufanya ikiwa utapimwa na kukutwa na COVID-19 wakati wa ukaaji wako au baada ya hapo

  Ikiwa hivi karibuni ulipimwa na kugunduliwa kuwa na ugonjwa wa COVID-19 au umeanza kuhisi dalili zozote za COVID-19, fikiria kumjulisha mtu yeyote ambaye huenda ameathiriwa au kuwa na uwezekano wa mtagusano, pamoja na mamlaka za eneo husika.

  Ulipata msaada uliohitaji?