Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Sera ya Karamu na Hafla

  Kumbuka: Kufikia tarehe 20 Agosti, 2020, Airbnb ilitangaza marufuku ya kimataifa kwa sherehe na hafla zote kwenye matangazo ya Airbnb, ikiwemo idadi ya watu kutozidi 16, ili kupatana na sera zetu za jumuiya. Marufuku hii ya karamu inatumika kwa nafasi zote zinazowekwa katika siku zijazo kwenye Airbnb na itaendelea kuwepo kwa muda usiojulikana, mpaka itakapotangazwa vinginevyo.

  Miongozo yetu ya Jumuiya inawapiga marufuku wanachama wa Jumuiya ya Airbnb wasisababishe adha inayoleta usumbufu kwa kitongoji jirani. Wenyeji na wageni wanaweza kukidhi kiwango hiki kwa kuhakikisha wanaenda sambamba kabisa na matarajio kwa ajili ya mikusanyiko kwenye matangazo. Ingawa tunaamini wageni wengi wana heshima, tumeunda sera yetu ya Sherehe na Hafla ili kutoa mwongozo ulio wazi kuhusu kinachotarajiwa kutoka kwa kila mtu. Hadi itakapotangazwa vinginevyo, sera hii inapiga marufuku:

  • Mikusanyiko ya watu zaidi ya 16
  • Sherehe na hafla zote zenye kuleta usumbufu

  Wageni ambao wameripotiwa kwa sababu ya kuandaa sherehe yenye kuleta usumbufu au kukiuka sheria zetu kuhusu mikusanyiko ya watu zaidi ya 16 wanaweza kusimamishwa au kuondolewa kwenye tovuti ya Airbnb. Katika baadhi ya visa, tathmini za wageni zilizoandikwa baada ya sherehe kama hizo zinaweza kuondolewa. Tunaweza pia kuondoa matangazo ikiwa tutatambua kwamba Mwenyeji ameidhinisha sherehe inayokiuka sera hii. Tukipokea ripoti kwamba tangazo linaleta usumbufu kwenye jumuiya jirani, tunaweza kumwomba Mwenyeji abadilishe sheria zake au azuie tangazo hilo kwa muda.

  Mbali na kuimarisha sheria zetu kuhusu sherehe, tunashughulikia pia teknolojia za kugundua hatari ambazo husaidia kukomesha sherehe zenye kuleta usumbufu hata kabla ya kuanza.

  Mikusanyiko mikubwa

  Hadi itakapotangazwa vinginevyo, mikusanyiko ya watu zaidi ya 16—ikiwemo wageni wanaolala usiku kucha na wanaozuru tu—hairuhusiwi, bila kujali idhini ya Mwenyeji.

  Sherehe na hafla

  Hadi itakapotangazwa vinginevyo, sherehe na hafla zote zenye kuleta usumbufu zimepigwa marufuku, bila kujali ukubwa. Kwa wageni wanaoandaa aina hizi za hafla, akaunti zao zinaweza kuondolewa na Wenyeji wanaokiuka sheria hii na kuwaruhusu wageni kuandaa sherehe, hatua zinaweza kuchukuliwa dhidi ya akaunti zao ikiwemo kuondolewa kwa tangazo lao.

  Kuripoti usumbufu

  Wakati nyumba iliyotangazwa kwenye Airbnb inasababisha usumbufu—iwe ni kelele nyingi mno, sherehe yenye vurugu, mkusanyiko wa watu zaidi ya 16, au mwenendo usio salama—wanachama wa jumuiya ya eneo husika wanaweza kuiripoti kupitia Usaidizi kwa Jumuiya, ambayo inatoa kiunganishi cha kwenda kwenye huduma za dharura za eneo husika. Pia wataweza kutumia nambari ya simu ya timu ya Usaidizi kwa Jumuiya, ambapo wanaweza kuripoti sherehe ambayo bado inaendelea. Mara tatizo likiisharipotiwa, Airbnb itatuma barua pepe ya kuthibitisha inayoelezea hatua itakayofuata.

  Uingiliaji wa sherehe bila idhini

  Kupunguza idadi ya sherehe za nyumba zisizoidhinishwa kwenye Airbnb kumekuwa kipaumbele kwa muda mrefu. Tunachukua hatua ili kusaidia usafiri salama na wa kuwajibika. Kama sehemu ya marufuku yetu ya kimataifa ya sherehe, tunaweza kuzuia baadhi ya nafasi zilizowekwa ambazo tunaona kwamba zina hatari kubwa ya kufanya sherehe zisizoidhinishwa.

  Miongozo ya maudhui ya tangazo

  Kwa mujibu wa sera hii, Wenyeji hawapaswi kuvutia sherehe na hafla zenye kuleta usumbufu katika nyumba yao kwa kutangaza kwamba sehemu yao inafaa kwa ajili ya sherehe au hafla. Vivyo hivyo, Wenyeji hawapaswi kutangaza sehemu yao kwa ajili ya mikusanyiko ya watu zaidi ya 16.

  Matangazo yanayokiuka sheria hizi kupitia kichwa cha tangazo, maelezo, sheria za nyumba, picha, nk, yanaweza kuzuiwa kwa muda hadi maudhui yanayokiuka yaondolewe. Pale ambapo tumepokea malalamiko kwamba nyumba inakiuka sheria hii, tunaweza pia kuzuia tangazo hilo kwa muda wa hadi siku 30 na kumwomba Mwenyeji abadilishe tangazo lake ili kujumuisha sheria iliyo wazi inayosema kuwa sherehe na hafla haziruhusiwi.

  Katika hali nadra ambapo inaonekana tangazo limekusudiwa tu kuandaa sherehe na hafla (kwa mfano, maeneo ya sherehe au hafla) au katika hali ambapo nyumba imesababisha kero mbaya sana kwenye kitongoji, tangazo hilo linaweza kuondolewa kabisa kwenye Airbnb.

  Sheria ambazo zinatumika kwa aina tofauti za nyumba

  Mipangilio ya ukarimu wa jadi

  Tunatumaini kwamba Wenyeji wa maeneo ya ukarimu wa jadi (kama vile hoteli mahususi) wataweza kuamua sheria zao wenyewe kwa ajili ya hafla. Wenyeji wa ukarimu wa jadi wanaweza kuruhusu hafla zinazofaa kwa busara yao wenyewe. Katika hali ambapo tunapokea malalamiko kuhusu matangazo na hafla hizi au ambapo aina za hafla hazifai, tutafuatilia maeneo haya kadiri inavyohitajika.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana