
Nyumba yako kwa ajili ya Kombe la Dunia la FIFA
Popote mchezo unapokupeleka, pata sehemu za kukaa na mambo ya kufanya ya kipekee.


Pata sehemu nzuri ya kukaa
Kanada
Meksiko
Marekani
Nenda zaidi ya uwanja wa michezo
Nufaika zaidi na safari yako kupitia matukio halisi na shughuli za eneo husika.
Maswali yako yamejibiwa
Nitapataje sehemu ya kukaa karibu na uwanja wa michezo wa Kombe la Dunia?
Anza kwa kuchagua jiji la mwenyeji kutoka kwenye ukurasa huu. Utapelekwa kwenye ramani iliyo na maeneo ya uwanja wa michezo na matangazo yaliyo karibu. Wenyeji wengi hutaja umbali wa kutembea au ukaribu na viwanja vya michezo katika maelezo ya tangazo lao, kwa hivyo hakikisha unaangalia hilo kabla ya kuweka nafasi.
Je, Airbnb inafaa kwa safari ya kikundi na marafiki au familia?
Ndiyo! Kuweka nafasi ya nyumba nzima hulipa kundi lako nafasi ya kutosha ya kupumzika, kupika chakula na kutumia muda pamoja. Unaweza kutumia vichujio ili kupata matangazo yaliyo na idadi sahihi ya vyumba vya kulala na mabafu na uangalie idadi ya juu ya wageni ili kuhakikisha kila mtu ana mahali pazuri pa kulala.
Ninawezaje kuchagua Airbnb bora?
Tafuta matangazo yaliyo na alama ya Vipendwa vya Wageni. Hizi ni nyumba zinazopendwa zaidi kwenye Airbnb, zilizochaguliwa kwa ajili ya ukadiriaji, tathmini na kutegemeka. Hakikisha unaangalia tathmini za wageni, picha za tangazo na vistawishi ili upate nyumba inayofaa zaidi mahitaji yako.
Itakuwaje ikiwa ninahitaji kubadilisha au kughairi nafasi niliyoweka?
Matangazo mengi hutoa ughairi unaoweza kubadilika, hivyo kufanya iwe rahisi kuweka nafasi tena ikiwa ratiba yako itabadilika. Unaweza kuchuja utafutaji wako ili uone matangazo yenye machaguo yanayoweza kubadilika pekee.
Ninawezaje kupata usaidizi ikiwa ninahitaji msaada wakati wa ukaaji wangu?
Timu ya usaidizi ya Airbnb inapatikana saa 24, popote ulipo ulimwenguni. Unaweza kuwasiliana nao kupitia programu, tovuti au kwa simu.





















