Ofa ya Airbnb ya Kuweka Tangazo Tena

Sheria na Masharti ya Promosheni ya Mwenyeji ya Kuweka Tangazo Tena

Wenyeji wanaostahiki Promosheni ya Mwenyeji ya Kuweka Tangazo Tena ("Promosheni") wanastahiki kupokea malipo kutoka Airbnb.Ili kustahiki, Mwenyeji lazima: (1) abofye kiungo kilicho kwenye barua pepe yake ya mwaliko, arifa kwa simu au arifa kwenye bidhaa; (2) aamilishe tena tangazo lililopo ambalo halitumiki au aunde tangazo jipya ifikapo tarehe 31 Machi, 2023 saa 5:59 usiku majira ya PST; na (3) akaribishe wageni kwenye Ukaaji Unaostahiki kwenye tangazo lake ambapo tarehe ya kutoka ni mnamo au kabla ya tarehe 31 Mei, 2023 saa 5:59 usiku majira ya PST."Ukaaji Unaostahiki" (i) ni ukaaji unaohudumiwa na Mwenyeji aliyepo kwenye Airbnb, (ii) katika mojawapo ya (a) tangazo (matangazo) lake ambalo hapo awali halikuwa likitumika au (b) tangazo (matangazo) jipya baada ya tarehe 16 Februari, 2023, (iii) lenye tarehe ya kutoka ifikapo tarehe 31 Mei, 2023 na (iv) ambalo halijaghairiwa kabla au wakati wa ukaaji. Wenyeji wanapaswa kuhakikisha kwamba tangazo hilo linatii matakwa yote na sheria za eneo husika.Baada ya Ukaaji Unaostahiki kukamilika, Wenyeji watapokea malipo kutoka Airbnb kupitia njia yao ya kawaida ya kupokea malipo. Malipo yatatolewa kwa ajili ya ukaaji wa kwanza unaostahiki unaokamilika ifikapo tarehe 31 Mei, 2023 kwenye hadi matangazo mawili (2) ya Mwenyeji, ikiwa Mwenyeji ana tangazo zaidi ya moja. Malipo yatafanywa ndani ya siku 90 baada ya ukaaji unaostahiki kukamilika. Kiasi cha malipo ambacho kila Mwenyeji anastahiki kinajumuishwa kwenye ofa kupitia barua pepe kutoka Airbnb. Wenyeji ambao hawatapokea ofa kupitia barua pepe kutoka Airbnb hawastahiki Promosheni hii.
Weka sehemu yako kwenye Airbnb