Jiunge na Mtandao wa Wenyeji Wenza
Wenyeji wengi wanataka mshirika mkazi mwenye ubora wa juu* ili awasaidie kukaribisha wageni. Kuanzia kuweka tangazo hadi usaidizi kwa wageni, unaweza kuchagua huduma unazotoa na ujipatie pesa kwa kuwasaidia wengine kukaribisha wageni.
Jiunge sasa

Tunakuletea Mtandao wa Wenyeji Wenza
Sasa unaweza kutoa usaidizi mahususi kwa wenyeji walio na matangazo katika eneo lako kupitia Mtandao wa Wenyeji Wenza.
Kujiunga na mtandao ni njia bora ya:- Kukuza huduma zako na bei
- Kuungana na washirika watarajiwa.
- Kufanya kazi kwa kujitegemea kwa kasi yako mwenyewe.
Jinsi Mtandao wa Wenyeji Wenza unavyofanya kazi


Huduma unazoweza kutoa
Wasifu wako wa mwenyeji mwenza ni mahali ambapo unatangaza ujuzi wako na kuweka maelezo kuhusu huduma unazotoa. Chagua kutoka kwenye orodha ya huduma za kushirikiana kukaribisha wageni
- Kuandaa tangazo
- Kuweka bei na upatikanaji
- Usimamizi wa maombi ya kuweka nafasi
- Ujumbe wa mgeni
- Usaidizi wa mgeni kwenye eneo
- Kufanya usafi na matengenezo
- Upigaji picha wa nyumba
- Usanifu wa ndani na mitindo
- Vibali vya leseni za huduma ya kukaribisha wageni
Ili ustahiki kujiunga na Mtandao wa Wenyeji Wenza lazima utimize matakwa mahususi.
Pata maelezo zaidiMichael, mwenyeji mwenza jijini Paris
"Tangu niwe mwenyeji mwenza, sijihisi tena kuwa peke yangu katika kazi yangu. Ninahisi kama nina usaidizi na hamasa ninayohitaji ili kukuza biashara yangu na kutoka katika maisha niliyozoea."
Usaidizi wa kukusaidia kufanikiwa
Nyenzo maalumu
Simamia biashara yako jinsi unavyopenda. Mtandao hutoa nyenzo za kukusaidia kuanzisha mahusiano yenye mafanikio na wenyeji na kukusaidia unapokuza biashara yako ya kushirikiana kukaribisha wageni.
Nyenzo na jumuiya
Angalia mfululizo wa nyenzo za elimu kuhusu zana unazoweza kutumia na uungane na jumuiya amilifu ya wenyeji wenza ambao wanaweza kukusaidia kuanza.

Michael
Ufaransa (Paris)

Guillermo
Uhispania (Granada)

Julie
Ufaransa (Le Touquet)

Anne-Lie
Uhispania (Tenerife)

Clarysse & Arthur
Ufaransa (Paris)

Ousmane
Ufaransa (Nanterre)

Gabriel
Uhispania (Marbella)

Je, unatafuta mwenyeji mwenza?
Pata mwenyeji mkazi mwenye ubora wa juu, ambaye anaweza kutunza nyumba yako na wageni kwenye Mtandao wa Wenyeji Wenza. Wenyeji kwenye Mtandao wa Wenyeji Wenza kwa kawaida wana ukadiriaji wa juu, viwango vya chini vya kughairi na uzoefu thabiti wa kukaribisha wageni kwenye Airbnb. Ukadiriaji unategemea tathmini za wageni kwa matangazo wanayokaribisha wageni au kushirikiana kukaribisha wageni na huenda usiwakilishe huduma za kipekee za mwenyeji mwenza.
Maswali yaulizwayo mara kwa mara
Je, matakwa ya kuwa mwenyeji mwenza ni gani?
Matakwa ya kujiunga na Mtandao wa Wenyeji Wenza ni:
- Una tangazo amilifu kama mwenyeji au kama mwenyeji mwenza mwenye ufikiaji kamili au ufikiaji wa kalenda na ujumbe.
- Umekaribisha wageni au umeshirikiana kukaribisha wageni kwenye sehemu 10 au zaidi za kukaa au sehemu tatu au zaidi za kukaa kwa jumla ya angalau usiku 100 kwenye Airbnb katika miezi 12 iliyopita.
- Umedumisha ukadiriaji wa wastani wa nyota 4.8 au zaidi kutoka kwa wageni katika miezi 12 iliyopita kwa matangazo yote unayokaribisha wageni au unayoshirikiana kukaribisha wageni ukiwa na ufikiaji kamili au ufikiaji wa kalenda na ujumbe.
- Una kiwango cha kughairi cha chini ya asilimia 3, isipokuwa kwa sababu fulani halali usizoweza kudhibiti.
- Akaunti yako ya Airbnb iko katika hali nzuri. Utambulisho wako lazima uthibitishwe na picha yako ya wasifu lazima ikidhi matakwa yetu ya picha ili kuonyeshwa kwenye mtandao.
Mtandao wa Wenyeji Wenza utapatikana wapi?
Mtandao wa Wenyeji Wenza unapatikana katika nchi 12 ikiwemo Australia, Brazili, Kanada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Meksiko, Korea Kusini, Uhispania, Uingereza na Marekani. Endelea kufuatilia kwa ajili ya nchi za ziada kadiri mtandao unavyopanuka.
Je, kuna matakwa yoyote ya kisheria?
Kama mwenyeji mwenza, unawakilisha na unathibitisha kwamba wewe na wafanyakazi au mawakala wowote wanaofanya kazi na wewe au kwa niaba yako, mna vibali vyote, leseni, bima na/au sifa zinazohitajika kwa ajili ya huduma zenu. Kwa mfano, kutoa huduma za usimamizi wa nyumba kunaweza kuhitaji kwamba uwe dalali wa mali isiyohamishika aliye na leseni na kufanya kazi bila leseni kunaweza kuwa na adhabu kubwa kwako na/au kwa wenyeji unaofanya nao kazi. Iwapo una maswali kuhusu jinsi sheria za eneo husika zinavyotumika, unapaswa kutafuta ushauri wa kisheria kila wakati kabla ya kujaza fomu.
Ninaweza kutarajia kujipatia kiasi gani cha fedha?
Kabla ya kuanza, wewe na mwenyeji wako mnapaswa kukubaliana kuhusu bei ya huduma zenu. Wenyeji wenza wengi huchagua kulipwa asilimia au kiasi mahususi kwa kila nafasi iliyowekwa.**
Nitaunganishwa vipi na wenyeji wapya?
Utapokea ujumbe kutoka kwa wenyeji katika kikasha chako cha Airbnb. Utaweza kujadili masharti ya ushirikiano wako, kukubaliana kuhusu bei kwa kila nafasi iliyowekwa na kukamilisha makubaliano yenu pamoja. Uko huru kuchagua matangazo unayotaka kusimamia na wenyeji ambao ungependa kushirikiana nao.
Ungependa kuanza vipi?
Kwanza utajaza fomu. Ikiwa unastahiki, utapokea mwaliko wa kukamilisha usajili wako, kujaza wasifu wako na kuweka bei yako iliyopendekezwa. Baada ya hapo, wenyeji wanaotafuta usaidizi katika eneo lako wataweza kukupata.
Mtandao wa Wenyeji Wenza sasa unapatikana nchini Australia, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japani, Meksiko, Korea Kusini, Uhispania na Uingereza (unaendeshwa na Airbnb Global Services); Kanada, Marekani (unaendeshwa na Airbnb Living LLC) na Brazili (unaendeshwa na Airbnb Plataforma Digital Ltda).Pata maelezo zaidi.
*Wenyeji kwenye Mtandao wa Wenyeji Wenza kwa kawaida wana ukadiriaji wa juu, viwango vya chini vya kughairi na uzoefu wa kukaribisha wageni kwenye Airbnb. Ukadiriaji unategemea tathmini za wageni kwa matangazo wanayokaribisha wageni au kushirikiana kukaribisha wageni na huenda usiwakilishe huduma za kipekee za mwenyeji mwenza. ** Katika nchi nyingi, unaweza kugawana na mwenyeji mwenza wako sehemu ya malipo ya kila nafasi iliyowekwa kupitia Airbnb. Kuna vizuizi fulani kulingana na mahali ulipo au mahali alipo mwenyeji mwenza wako au mahali nyumba yako ilipo.