Airbnb × PICC (Kampuni ya Bima ya Watu wa China)

Mpango wa Ulinzi wa Mwenyeji wa China

Huko China Bara, hatuwawezeshi tu wenyeji wa nyumba na matukio kufanya kazi kwa ufanisi, kama mtu binafsi na kwa mafanikio kupitia Airbnb. Pia tunashirikiana na Kampuni ya Bima ya Watu ya China (PICC) ili kuandaa Mpango wa Bima wa Mwenyeji wa China. Mpango huo unajumuisha programu tatu: [Bima ya Nyumba ya Mwenyeji wa China] (#host_property_insurance), [Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji wa China] (#host_protection_insurance) na [Bima ya Ulinzi ya Tukio ya China] (#experience_protection_insurance) ili kufanya mchakato wa kudai bima uwe rahisi, salama na thabiti zaidi. Tathmini mambo yafuatayo ili upate maelezo kuhusu ulinzi utakaopokea.

Je, faida ni nini?

Ulinzi kamili

Linda tangazo lako na mali zinazohusiana; na vilevile usalama wa wageni wako na wahusika wengine.

Kiasi cha juu

 • Bima ya Nyumba ya Mwenyeji wa China hadi CNY 1,000,000
 • Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji wa China hadi CNY 5,000,000
 • Bima ya Ulinzi ya Tukio ya China hadi CNY 5,000,000

Usaidizi wa kiweledi

 • Timu ya madai ya PICC inashirikiana na Sedgwick China Co., Ltd ili kutoa huduma zake za kipekee pamoja
 • Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Airbnb hutoa majibu bora kwa maswali yako na huduma muhimu binafsi

Bima ya Mali ya Mwenyeji wa China

Kiasi cha bima:

 • Uharibifu kwenye sehemu yako unaosababishwa na wageni
 • Uharibifu wa mali zako unaosababishwa na wageni
 • Uharibifu kwenye nyumba yako au mali unaosababishwa na mnyama au mnyama kipenzi wa mgeni (kwa mfano, mbwa wa kuongoza)
 • Upotevu wa mapato kutoka kwenye nafasi zote zilizowekwa unaotokana na ajali, hadi kiwango cha juu cha CNY 10,000

Vitu visivyoghulikiwa na bima

 • Wizi wa pesa na hisa (kwa mfano, amana za benki, hisa)
 • Uchakavu wa kawaida
 • Kujeruhiwa mwili au uharibifu wa mali ya wageni au wahusika wengine (hizo zinaweza kushughulikiwa na [Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji wa China] (#host_protection_insurance)
 • Madoa, kuvu, nk. kwenye nyumba
 • Majanga ya asili
 • Nyinginezo

Utaratibu wa madai

1. Ongea na mgeni wako

Katika kipindi cha majadiliano (siku 60), mwenyeji kwanza anaweza kuzungumza na mgeni kuhusu uharibifu wowote wa mali uliosababishwa na uzembe wa mgeni kupitia [Kituo cha Usuluhishi] (/masuluhisho); unaweza kuanzisha madai dhidi ya mgeni kulingana na kiasi cha upotevu.

Kwa madai zaidi ya kipindi cha majadiliano lakini bado yapo ndani ya kipindi cha bima ya kisheria (miaka 2), tafadhali [bonyeza hapa] (/bima/weka-madai?reservation_locale=cn&program_type=PICC_HOST_GUARANTEE) kuyawasilisha PICC moja kwa moja.

2. Wasilisha madai ya bima

Ikiwa mazungumzo hayakufanikiwa, mwenyeji anaweza kuwasilisha ombi la madai kwa PICC kupitia Historia ya Maombi katika [Kituo cha Usuluhishi] (/masuluhisho); Airbnb wakati huo huo itatuma ombi hilo la madai kwa PICC.

3. Fuatilia na PICC

Baada ya kutathmini na kuandikisha kesi hiyo, PICC watawasiliana na mwenyeji pamoja na kampuni huru ya nje ya kiweledi ya kufanya ukadiriaji (Sedgwick China Co.,Ltd) ili kukamilisha mchakato utakaofuata wa madai ya bima.

Kwa madai ya kabla ya tarehe 1 Agosti, 2020, ikiwa mazungumzo hayatafanikiwa, bado yatashughulikiwa na timu ya Airbnb na hayatawasilishwa kwa PICC.

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji wa China

Kiasi cha bima

 • Dhima yako ya kisheria ya kujeruhiwa mwili kwa wageni au watu wengine
 • Dhima yako ya kisheria ya uharibifu wa mali ya wageni au wahusika wengine

Vitu visivyoghulikiwa na bima

 • Uharibifu au jeraha la mwili linalosababishwa kwa kukusudia (si ajali)
 • Uharibifu kwenye nyumba yako au mali yako (inaweza kulindwa na [Bima ya Nyumba ya Mwenyeji wa China] (#host_property_insurance))
 • Nyingine (Magonjwa kama vile mizio, ukurutu, kifafa, nk.)

Utaratibu wa madai

1. Wasilisha madai ya bima

Jaza na uwasilishe [ombi la madai] (/bima/fungua madai?reservation_locale=cn) kulingana na uharibifu wako halisi (ajali lazima iwe ilitokea mnamo au baada ya tarehe 1 Agosti, 2020); Airbnb itarekodi ombi lako la madai wakati uleule na kulipeleka PICC.

2. Fuatilia kampuni ya nje ya ukadiriaji (Sedgwick China Co, Ltd)

Baada ya kutathmini na kuandikisha kesi hiyo, PICC itawasiliana nawe pamoja na kampuni huru ya nje ya kufanya ukadiriaji (Sedgwick China Co.,Ltd) ili kukamilisha mchakato utakaofuata wa madai ya bima.

Bima ya Ulinzi ya Tukio ya China

Kiasi cha bima

 • Wajibu wako wa kisheria kwa majeraha ya mwili ya washiriki au watu wengine
 • Wajibu wako wa kisheria kwa uharibifu wa mali ya washiriki au watu wengine

Vitu visivyoghulikiwa na bima

 • Majeraha au uharibifu wa mali uliofanywa kwa makusudi (si ajali)
 • Uharibifu kwa mali binafsi ya mwenyeji, vitu vilivyopotea au vilivyoibiwa wakati wa hafla ya tukio
 • Matukio yanayohusisha ndege na usafirishaji (sehemu hii imewekewa bima na usafirishaji, kama vile bima ya gari)
 • Michezo migumu au yenye mazoezi makali kama vile kukwea miamba na kuruka kutoka juu kwa kamba
 • Nyinginezo

Utaratibu wa madai

1. Wasilisha madai ya bima

Jaza na uwasilishe [ombi la madai] (/bima/andikisha-madai?reservation_locale=cn&program_type = PICC_EXPERIENCE_PROTECTION_INSURANCE) kulingana na uharibifu wako halisi (ajali lazima iwe ilitokea mnamo au baada ya tarehe 1 Agosti, 2020); Airbnb itarekodi ombi lako la madai na kulipeleka PICC wakati uleule.

2. Fuatilia kampuni ya nje ya ukadiriaji (Sedgwick China Co, Ltd)

Baada ya kutathmini na kuandikisha kesi hiyo, PICC itawasiliana nawe pamoja na kampuni huru ya nje ya kufanya ukadiriaji (Sedgwick China Co.,Ltd) ili kukamilisha mchakato utakaofuata wa madai ya bima.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Kwa nini Mpango wa Ulinzi wa Mwenyeji wa Airbnb China uliundwa?

Kama tovuti ya malazi inayoshirikiwa kimataifa, tunathamini uzoefu wa mtumiaji na sauti ya wenyeji katika kila nchi na eneo. Tukiwa na mamia ya maelfu ya nyumba amilifu na maelfu ya hafla za matukio nchini China Bara, ni jukumu letu kutoa bima bora, ya eneo husika kwa kundi kubwa la wenyeji wa nyumba na matukio wanaoshirikiana nasi.

Je, wigo wa Mpango huu ni nini?

Mpango wa Ulinzi wa Mwenyeji wa Airbnb China unatumika kwa nafasi zilizowekwa na matukio yaliyoko China Bara (bila kujumuisha Hong Kong (SAR), Macau (SAR) na Taiwan).Bima ya Nyumba ya Mwenyeji wa China inatumika kwa nafasi ambayo haijaghairiwa na kukaliwa kwa zaidi ya usiku 1 huko China Bara. Matatizo yote yanayohitaji bima ambayo yanasababishwa na ukaaji wa mgeni kwenye nyumba au kushiriki kwenye tukio katika muda wa nafasi iliyowekwa yanaweza kushughulikiwa na Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji wa China na Bima ya Ulinzi ya Tukio la China (kuanzia tarehe 1 Agosti, 2021).

Wenyeji wa nyumba na matukio huwasilishaje madai ya bima?
 1. Fanya madai dhidi ya mgeni wako kupitia tovuti au [andikisha madai] (/ bima/unda-madai?reservation_locale=cn) na PICC haraka iwezekanavyo baada ya ajali. Tafadhali mkumbushe mgeni wako au mshiriki wa tukio azungumze nawe haraka na kutoa maoni kuhusu jambo lililotukia.
 2. Ikiwa sehemu ya ndani ya nyumba yako imeharibiwa, acha ikaguliwe kwenye sehemu hiyo haraka.
 3. Ni muhimu kwamba ukusanye mara moja ushahidi mwingi iwezekanavyo, kama vile picha au video, au vyeti vya uchunguzi wa polisi, ili uweze kuwasilisha taarifa za kutosha za kuthibitisha wakati wa kuandiksha madai yako.
 4. Chukua hatua za vitendo baada ya ajali: piga simu kwenye nambari 110, 120, au 119 kwa msaada wa haraka.
Ni jinsi gani ya kupata ushauri wa masuala yanayohusiana na madai ya bima?

Unaweza kuwasiliana na timu ya huduma ya madai ya Marsh kwa taarifa zaidi kuhusu bima kupitia barua pepe [CN.Airbnb@marsh.com] (mailto:CN.Airbnb@marsh.com) au piga simu 400 622 8012, saa za huduma ni saa 3:30 asubuhi hadi saa 11:30 alasiri siku za kazi. Ikiwa inaweza kuwekewa bima itaamuliwa kiweledi na PICC kulingana na visa mahususi. Anwani ya barua pepe ya PICC ni [airbnbclaim@piccsh.com] (mailto:airbnbclaim@piccsh.com), SIMU ni 021-95518 (Kwa watumiaji ambao si wakazi wa Shanghai, unapaswa kupiga msimbo 021 kwanza; tafadhali wajulishe wafanyakazi wa huduma kwamba wewe ni mwenyeji au mgeni wa Airbnb), na nambari ya huduma ni saa 24 kwa siku; Kwenye sikukuu, rekodi ya huduma ya wateja itatumwa kwenye timu maalumu ya kisa ili ishughulikiwe nao watajibu moja kwa moja.

PICC ni kampuni ya aina gani ya bima?

Kama mshirika wa "Mpango wa Bima ya Mwenyeji wa China", PICC ni kampuni ya bima ya nyumba inayomilikiwa na serikali na ambayo imekuwepo kwa muda mrefu; nayo ina nguvu ya bima nchini China. Inaendesha kampuni kubwa za biashara zenye kiwango cha juu zilizo kwenye mstari wa mbele wa soko la bima ya nyumba kimataifa.