Unda wasifu wa mwenyeji mwenza unaovutia

Tangaza ujuzi wako na upige picha ya ubora wa juu.
Na Airbnb tarehe 16 Okt 2024
Imesasishwa tarehe 3 Mac 2025

Wasifu wako wa mwenyeji mwenza ni fursa ya kujitangaza. Mtandao wa Wenyeji Wenza hutumia algorithimu mahususi ili kuonyesha wasifu wa wenyeji wenza husika kwa mtu yeyote anayetafuta msaada.

Kujaza wasifu wako wa mwenyeji mwenza

Kamilisha wasifu wako wa mwenyeji mwenza ili uonekane katika matokeo ya utafutaji. Taarifa katika wasifu wako inapatikana kwa umma.

  • Jina: Wasifu wako wa mwenyeji mwenza hutumia kiotomatiki jina lako la kwanza na la mwisho kutoka kwenye akaunti yako ya Airbnb, isipokuwa uchague kuonyesha jina lako la kwanza pekee katika mipangilio yako ya wasifu wa mwenyeji mwenza. Ili kuonekana kwenye Mtandao wa Wenyeji Wenza, jina lako linaloonyeshwa, iwe ni jina rasmi kisheria au unalopendelea, lazima liwe jina lako binafsi, si jina la biashara.*
  • Utangulizi wa wasifu: Andika maelezo mafupi kuhusu uzoefu wako wa kukaribisha wageni ambayo yanaelezea kile kinachokufanya uwe wa kipekee. Kwa mfano, "Nilianza kwa kukaribisha wageni kwenye chumba cha ziada. Sasa, ninawasaidia wenyeji wengine wapate tathmini nzuri na kupata mapato wanayoyatazamia." Utangulizi wako utaonekana katika matokeo ya utafutaji na kwenye sehemu ya juu ya wasifu wako.
  • Huduma: Chagua kati ya aina 10, kama vile kuandaa tangazo na ujumbe wa wageni na ueleze kwa ufupi jinsi mbinu yako ya kukaribisha wageni ilivyo ya kipekee. Kwa mfano, "Nimefanya kazi na wafanya usafi wangu kwa zaidi ya miaka mitano na tunafanya ukaguzi wa kawaida wa ubora kabla na baada ya mgeni wa kwanza kukaa."
  • Bei: Wajulishe wenyeji unachotoza kwa kila nafasi iliyowekwa kwa ajili ya usaidizi unaoendelea (inahitajika) na kwa kila tangazo kwa ajili ya kuandaa (hiari).
  • Eneo la huduma ya mahali husika: Weka eneo ambapo unaweza kutoa huduma za kukaribisha wageni ana kwa ana ndani ya takribani kilomita 100.
  • Maelezo zaidi kukuhusu: Unaweza kushiriki maelezo kuhusu safari yako ya kukaribisha wageni, kama vile kile kilichokuingiza kwenye huduma ya ukarimu na wakati unaojivunia zaidi.

Wasifu wako wa mwenyeji mwenza pia unajumuisha taarifa hii.

  • Takwimu muhimu: Wenyeji huona idadi ya matangazo unayokaribisha wageni au unayoshirikiana kukaribisha wageni, idadi ya miaka ambayo umekuwa ukikaribisha wageni na ukadiriaji wa jumla wa wageni kwenye matangazo yote ambayo umekaribisha wageni au umeshirikiana kukaribisha wageni.
  • Vidokezi: Wenyeji wanaona utambuzi kwamba wewe au matangazo unayokaribisha wageni au kushirikiana kukaribisha wageni, umepokea kwenye Airbnb, kama vile "Mwenyeji Bingwa kwa miaka 8" au "Ukadiriaji bora kutoka kwa wageni wa hivi karibuni."
  • Tathmini za wageni: Wenyeji huona tathmini za matangazo unayokaribisha wageni au unayoshirikiana kukaribisha wageni, kuanzia na za hivi karibuni zaidi. Wanaweza pia kuchuja kulingana na ukadiriaji wa juu au wa chini zaidi na kutafuta kulingana na maneno muhimu.
  • Matangazo yako: Wenyeji huona matangazo yote unayosaidia na muda ambao umekaribisha wageni au umeshirikiana kukaribisha wageni kila moja.

Kupiga picha nzuri ya wasifu

Wasifu wako wa mwenyeji mwenza huvuta kiotomatiki picha ya wasifu kutoka kwenye akaunti yako ya Airbnb. Picha lazima iwe na uangavu wa hali ya juu na ukubwa wa faili uwe hadi MB 100 na isiwe na ukungu. Picha lazima ionyeshe wazi uso wako.*

Fuata miongozo hii:

  • Tumia mandharinyuma sahili na mwanga wa asili.
  • Piga picha ya wima na uache nafasi ya kuikata.
  • Epuka picha za kujipiga, mwako, mwanga wa nyuma, nembo na vielelezo.
  • Usijumuishe wanyama vipenzi na watu wengine.

*Ikiwa unakaribisha wageni kama biashara nchini Australia, Eneo la Kiuchumi la Ulaya au Uingereza, takwa hili halitumiki.

Pata maelezo kuhusu algorithimu ya utafutaji kwenye Kituo cha Msaada.

Mtandao wa Wenyeji Wenza unapatikana nchini Ufaransa, Uhispania, Italia, Ujerumani, Uingereza, Australia, Meksiko (unaendeshwa na Airbnb Global Services Limited), Kanada, Marekani (unaendeshwa na Airbnb Living LLC) na Brazili (unaendeshwa na Airbnb Plataforma Digital Ltda).

Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Airbnb
16 Okt 2024
Ilikuwa na manufaa?