Nembo ya Airbnb 2022 Toleo la Novemba
Toleo la Novemba

Sasa ni rahisi zaidi kuweka nyumba yako kwenye Airbnb

Mwenyeji Bingwa anayetabasamu katika programu ya Airbnb. Maandishi yanatujulisha kwamba jina lake ni Myranda, ana uzoefu wa miaka mitatu akikaribisha wageni huko Little Rock na ukadiriaji wake wa Airbnb ni nyota 4.96 kati ya 5.

Anza Kutumia Airbnb: Njia mpya na rahisi ya kuanza

Mtu yeyote anaweza kuweka eneo lake kwenye Airbnb na kuanza kujipatia mapato, akiwa na mwongozo wa moja kwa moja wa bila malipo, katika kila hatua.
Simu inaonyesha kiibukizi kilichoandikwa: Pata mwongozo wa moja kwa moja kutoka kwa Mwenyeji Bingwa. Juu ya kichwa hiki tunaona Myranda ambaye ni Mwenyeji Bingwa, akizungukwa na miduara zaidi yenye Wenyeji Bingwa wanaotabasamu. 

Maandishi kwenye skrini yameandikwa: Tutakukutanisha na Mwenyeji mzoefu. Atakuongoza kupitia gumzo au video unapoweka eneo lako kwenye Airbnb. Unaweza pia kuanza kivyako kisha ukutanishwe baadaye.

Vitufe viwili vilivyo hapa chini vinakupa chaguo la kukutanishwa na Mwenyeji Bingwa au kuanza tu peke yako.

Mwongozo wa ana kwa ana kutoka kwa Mwenyeji Bingwa

Kutanishwa na Mwenyeji Bingwa wako mwenyewe, Mwenyeji mzoefu ambaye atakupa msaada wa moja kwa moja kuanzia swali lako la kwanza hadi mgeni wako wa kwanza. Wanapatikana kwa njia ya simu, video au gumzo katika nchi zaidi ya 80.
Simu inaonyesha kichwa kilichoandikwa: Chagua mtu wa kumkaribisha kwenye nafasi ya kwanza uliyowekewa. Wenyeji wanaweza kuchagua kumkaribisha mgeni yeyote wa Airbnb au wanaweza kuchagua kumkaribisha mgeni mzoefu. Kitufe cha mgeni mwenye uzoefu kimechaguliwa.

Mgeni mzoefu kwa nafasi ya kwanza unayowekewa

Ili kukusaidia uhisi umeridhika zaidi mara ya kwanza unapokaribisha wageni, sasa una chaguo la kumkaribisha mgeni mzoefu, ambaye amekaa angalau mara tatu na ana rekodi nzuri kwenye Airbnb.
Simu inaonyesha Kichupo cha Leo kwa ajili ya Wenyeji wa Airbnb, kikiwa na mipangilio mbalimbali ili waweze kusimamia tangazo lao, kama vile nyenzo ya kalenda. Katika nusu ya chini ya skrini kuna machaguo ya Wenyeji wapya kuzungumza na Mwenyeji Bingwa wao au kupata usaidizi maalumu kutoka Airbnb, kwa kubofya tu kitufe kwenye skrini yao.

Usaidizi maalumu kutoka Airbnb

Kwa kubofya mara moja tu, Wenyeji wapya wanaweza kuwasiliana na wahudumu wetu wa Usaidizi wa Jumuiya waliopata mafunzo mahususi kwa ajili ya msaada wa chochote kuanzia matatizo ya akaunti hadi kulipwa. Kwa sasa unapatikana katika lugha 42.
Nembo ya AirCover kwa ajili ya Wenyeji
Nembo ya AirCover kwa ajili ya Wenyeji

Tunakuletea ulinzi hata zaidi

Uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni

Mfumo wetu kamili wa uthibitishaji hukagua maelezo kama vile jina, anwani, kitambulisho cha serikali na kadhalika ili kuthibitisha utambulisho wa wageni wanaoweka nafasi kwenye Airbnb.

Ukaguzi wa nafasi iliyowekwa

Teknolojia tunayomiliki inachambua mamia ya mambo katika kila nafasi iliyowekwa na inazuia baadhi ya nafasi zilizowekwa ambazo zinaonyesha hatari kubwa ya sherehe zenye kuvuruga na uharibifu wa mali.

Ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3

Airbnb inakufidia kutokana na uharibifu uliosababishwa na wageni kwenye nyumba na mali yako na inajumuisha ulinzi huu maalumu:

Vitu vya sanaa na vya thamani

Airbnb itarejesha, itabadilisha au kukulipa kutokana na vitu vya sanaa au vya thamani vilivyoharibiwa.

Magari na boti

Tunalinda magari, boti na vyombo vingine vya kwenye maji ambavyo unaegesha au kuhifadhi nyumbani kwako.

Uharibifu uliosababishwa na mnyama kipenzi

Tutalipa ili kurekebisha uharibifu uliosababishwa na mnyama kipenzi wa mgeni.

Kupoteza mapato

Ikiwa utalazimika kughairi nafasi zilizowekwa za Airbnb kwa sababu ya uharibifu wa mgeni, utalipwa fidia kwa ajili ya mapato yaliyopotea.

Kufanya usafi wa kina

Tutakufidia kwa ajili ya huduma za kufanya usafi wa ziada zinazohitajika baada ya ukaaji wa mgeni, kwa mfano, usafishaji wa kitaalamu wa zulia.

Bima ya dhima ya USD Milioni 1

Unalindwa katika tukio nadra ambapo mgeni anajeruhiwa au mali yake kuharibiwa au kuibwa.

Mawasiliano ya usalama saa 24

Endapo utahofia usalama wako, programu yetu itakupa ufikiaji wa kubofya mara moja kwa maafisa wa usalama waliopata mafunzo mahususi, mchana au usiku.

Pata maelezo kamili kuhusu jinsi AirCover kwa ajili ya Wenyeji inavyokulinda na vighairi vyovyote vinavyotumika.

Ni Airbnb pekee inayokupa AirCover

AirbnbWashindani
Uthibitishaji wa utambulisho wa mgeni
Ukaguzi wa nafasi iliyowekwa
Ulinzi dhidi ya uharibifu wa USD milioni 3
Vitu vya sanaa na vya thamani
Magari na boti
Uharibifu uliosababishwa na mnyama kipenzi
Kupoteza mapato
Kufanya usafi wa kina
Bima ya dhima ya USD Milioni 1
Mawasiliano ya usalama saa 24

Ulinganisho unategemea taarifa ya umma na matoleo ya bila malipo ya washindani wakuu kufikia mwezi Oktoba mwaka 2022.

Aina za Airbnb: Aina zaidi za kipekee

Leo tunakuletea aina sita mpya na kuboresha jinsi ya kuzifanya ziwe mahususi.
Mpya
Sehemu nzuri zilizowekwa kwenye Airbnb ndani ya wiki 10 zilizopita.
Vilele vya dunia
Nyumba zilizo karibu futi 10,000 juu ya usawa wa bahari, mara nyingi huwa na mandhari ya kupendeza.
Zinazovuma
Nyumba zenye ukadiriaji wa juu hutazamwa sana kwenye Airbnb.
Zinazofikika
Imethibitishwa kwa ajili ya vijia visivyo na ngazi vya kuingia kwenye nyumba, bafu na chumba cha kulala.
Michezo ya Watoto
Maeneo yenye vyumba vya michezo, mitelezo ya maji na kadhalika.
Hanok
Nyumba za jadi za Kikorea zilizojengwa kwa vifaa vya asili.
Kompyuta mpakato na simu zinaonyesha ukurasa wa mwanzo wa Airbnb ulio na safu mbili za nyumba kutoka kwenye aina mpya ya Toleo la Novemba la Airbnb inayoitwa Mpya, ambayo inajumuisha nyumba zilizowekwa kwenye Airbnb ndani ya wiki 10 zilizopita.Kompyuta mpakato na simu zinaonyesha ukurasa wa mwanzo wa Airbnb ulio na safu mbili za nyumba kutoka kwenye aina mpya ya Airbnb Toleo la Novemba inayoitwa Vilele vya Dunia, ambayo inajumuisha nyumba zilizo kwenye mwinuko wa juu, karibu futi 10,000 juu ya usawa wa bahari.Kompyuta mpakato na simu inaonyesha ukurasa wa mwanzo wa Airbnb ulio na safu mbili za nyumba kutoka kwenye aina mpya ya Airbnb Toleo la Novemba inayoitwa Zinazovuma, inayojumuisha nyumba ambazo zimetazamwa sana hivi karibuni.Kompyuta mpakato na simu inaonyesha ukurasa wa mwanzo wa Airbnb ulio na safu mbili za nyumba kutoka kwenye aina mpya ya Airbnb Toleo la Novemba inayoitwa Zinazofikika, ambayo inajumuisha nyumba zinazoweza kufikiwa kwa kutumia kiti cha magurudumu ambazo zimethibitisha njia zisizo na ngazi katika vyumba vya kulala na mabafu.Kompyuta mpakato na simu inaonyesha ukurasa wa mwanzo wa Airbnb ulio na safu mbili za nyumba kutoka kwenye aina mpya ya Airbnb Toleo la Novemba inayoitwa Michezo ya Watoto, ambayo inajumuisha nyumba zilizo na shughuli za kufurahisha kama vile vyumba vya michezo, mitelezo ya maji, viwanja vya mpira wa kikapu na kadhalika.Kompyuta mpakato na simu zinaonyesha ukurasa wa mwanzo wa Airbnb ulio na safu mbili za nyumba kutoka kwenye aina mpya ya Toleo la Novemba la Airbnb inayoitwa Hanok, ambayo inajumuisha nyumba za jadi za karne ya 14 za Korea Kusini zilizojengwa kwa vifaa vya asili.
Mpya
Mchakato wa kuzifanya ziwe mahususi umeboreshwa
Tunafanya aina tunazokuonyesha zikufae zaidi, kwa mfano, ikiwa umevinjari nyumba huko Napa tutakuonyesha Mashamba ya Mizabibu kwanza wakati mwingine utakapofungua programu.
Maelezo yaliyowekwa
Utapata pia maelezo zaidi kuhusu kila nyumba unapovinjari. Kwa mfano, nyumba katika Aina ya Hifadhi za Taifa zitaonyesha umbali wa lango la hifadhi ya taifa.

Maboresho ya ziada kwa ajili ya Wenyeji

Mchakato rahisi wa madai ya AirCover kwa ajili ya Wenyeji

Wenyeji sasa wanaweza kuwasilisha ombi la kufidiwa kwa hatua chache rahisi na kufuatilia hali yake kwenye Kichupo cha Leo.

Tunakuletea Malipo ya Haraka

Wenyeji sasa wanaweza kuchagua kupokea malipo kwenye kadi yao ya benki ndani ya dakika 30 au chini (inapatikana nchini Marekani pekee).

Tathmini za kina zaidi

Wageni na Wenyeji sasa wanaweza kuweka viambatisho kwenye tathmini zao ili kutoa maelezo mahususi zaidi kuhusu ukaaji.

Ulinzi dhidi ya tathmini za kulipiza kisasi

Tumepanua sababu ambazo tathmini inaweza kupingwa na tunawaruhusu Wenyeji waombe kuondolewa kwa tathmini zozote za kulipiza kisasi katika historia yao.

Sheria za msingi kwa ajili ya wageni

Sheria rahisi za msingi, zikisaidiwa na sera imara za uwajibikaji, husaidia kuhakikisha kwamba wageni wanaitendea kila nyumba kwa uangalifu na heshima.

Vidhibiti vya aina mpya

Kuanzia mwanzoni mwa mwaka 2023, Wenyeji wataweza kuona aina ya nyumba yao na kuweka maelezo mahususi kwa aina hiyo kwenye tangazo lao.