Iwe unasimamia maeneo mengi au unapendelea kuwa mbali zaidi, kukaribisha wageni na kundi ni njia nzuri ya kushiriki kazi na kuweka matangazo yako vizuri.
Timu ya kukaribisha wageni inaweza kuwa biashara au kundi la watu ambalo linasimamia upangishaji wa muda mfupi au wa muda mrefu kwa niaba ya mmiliki au mpangaji. Wanaweza kushughulikia idadi yoyote ya kazi, kuanzia kuweka nafasi na kuingiliana na wageni hadi kufanya usafi na matengenezo. Mtu yeyote aliye na tangazo kwenye Airbnb anaweza kualika huduma yake iliyopo ya usimamizi wa upangishaji ili ufikie na kusimamia matangazo yake kwa niaba yake. Fahamu jinsi timu za kukaribisha wageni zinavyotofautiana na Wenyeji Wenza.
Kama mmiliki wa akaunti, una udhibiti juu ya nani anayeweza kufikia tangazo lako na taarifa, hata wakati unasimamia tangazo na timu au msimamizi wa nyumba. Pata maelezo kuhusu ruhusa za timu ya kukaribisha wageni.
Ikiwa una nyumba nchini Ufaransa, Uhispania, au Kanada, unaweza kuisimamia kwa Luckey, kampuni tanzu ya Airbnb.