Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Sheria

Miongozo ya Alama ya Biashara

Airbnb inahisi jukumu kubwa katika kuhudumia jumuiya yake, ikiwemo Wenyeji, wageni, washirika na wengine wanaotumia au kukutana na tovuti na huduma zetu. Sehemu ya kuhudumia jumuiya yetu inajumuisha kulinda alama zetu za biashara na chapa. Hatutaki jumuiya yetu au mtu mwingine yeyote achanganyikiwe endapo kitu fulani kinaidhinishwa, kinadhibitiwa au kinasimamiwa na sisi. Miongozo hii imebuniwa ili kulinda chapa yetu na pia kukusaidia kushiriki habari kuhusu Airbnb kwa kuwajibika.

Miongozo hii ni sehemu ya Masharti yetu ya Huduma. Kwa kutumia huduma yoyote ya Airbnb, unakubaliana na Miongozo hii, Masharti yetu ya Huduma na sera zetu nyingine.

1. Alama za Biashara za Airbnb

Alama za biashara za Airbnb zinajumuisha jina la Airbnb, nembo ya Airbnb, nembo ya Bélo, beji ya Mwenyeji Bingwa na Aircover, pamoja na maneno yote, kauli mbiu, aikoni, nembo, michoro, ubunifu na viashiria vingine vinavyotambulisha Airbnb, mashirika yake yanayohusika au huduma au bidhaa zake. Tumeweka juhudi nyingi katika kuhakikisha kwamba kila kitu tunachokupa ni chenye ubora wa juu na chapa zetu zinawakilisha juhudi hizo. Hii ndiyo sababu tunalinda bidhaa zetu kabisa kwa kusajili alama zetu za biashara na mwonekano wa bidhaa nchini Marekani na ulimwenguni kote.

Huruhusiwi kutumia nembo ya Airbnb, nembo ya Bélo au alama zozote za biashara, nembo, au aikoni za Airbnb isipokuwa uwe na ruhusa rasmi iliyoandikwa kutoka kwenye biashara inayohusika au timu za kisheria katika Airbnb, Inc. Isipokuwa tu kwa matumizi machache ya "Airbnb" yaliyoelezewa katika Sehemu ya 2 hapa chini.

Epuka kuchanganyikiwa na Alama za Biashara za Airbnb

Fanya

 • Kubali na utumie jina, nembo na utambulisho wa chapa, ikiwemo rangi, fonti au aina ya maandishi, ambayo ni tofauti na alama za biashara na vipengele vya chapa vya Airbnb.

USI...

 • Usitumie nembo ya Bélo katika muundo wowote, ikiwemo kivyake au kwa kuchanganya na jina lolote la biashara, alama ya biashara, jina la akaunti ya mitandao ya kijamii au neno la kawaida.
 • Usitumie "Airbnb," "Air," "bnb," "b&b" au maneno kama hayo, katika jina la tovuti yako, jina la biashara, jina la bidhaa, alama ya biashara, usajili wa kikoa, akaunti ya mitandao ya kijamii, nyenzo za chapa, nk.
 • Usionyeshe rangi ya kipekee ya Airbnb ya Rausch katika maudhui yako, ikiwemo katika alama zako za biashara, nembo, ubunifu au vipengele vingine vya chapa.
 • Usitumie "Airbnb" kuwa inamaanisha "upangishaji wa muda mfupi" au maneno kama hayo.

Mifano

Safi!

Hapana...

Nyumba ya Kupangisha ya Kisiwani ya Bob’s Best

Airbnbike

Kufanya Usafi Katika Nyumba ya Kupangisha ya Red

Sunbnb au Sun Bnb

Likizo kwenye Kisiwa cha Anna

BNB Mwalimu

rentmyskihaus.com

Bikebandb au Bikeb&b

Nyumba za Kupangisha za Bike and Stay

nicebnb.com

STR Management Co

airmansion

2. Kutumia jina letu, "Airbnb"

Unaweza kuzungumza kuhusu Airbnb (kampuni) au kutumia "Airbnb" kuelezea kwa ukweli huduma unayotoa. Ikiwa haya yanakuhusu, tafadhali fuata miongozo ifuatayo kila wakati:

Iweke iwe ya kweli, sahihi na yenye maelezo

Fanya

 • Unaweza kutaja "Airbnb", lakini kwa njia pekee ambayo inaelezea kwa uaminifu na kwa usahihi uhusiano wako na Airbnb kampuni na/au bidhaa zinazotoka au zilizoidhinishwa na Airbnb, kama vile "Mwenyeji wa Airbnb," "Tangazo la Airbnb," "Programu ya Airbnb," na zaidi.
 • Tumia "Airbnb" kwenye kiini cha maandishi tu (si, kwa mfano, katika vichwa na vichwa vya habari) kwa ukubwa, aina, rangi na mtindo unaofanana na kiini cha maandishi yaliyosalia pekee.

USI...

 • Usitumie "Airbnb" kwa njia ambayo inadokezea ushirikiano, udhamini au kuidhinishwa, ikiwa ni pamoja na kama sehemu ya jina lako la biashara na/au kama neno lenye chapa (mfano "Usimamizi wa Nyumba wa Airbnb").
 • Usitumie neno "Airbnb" zaidi ya inavyohitajika ili kuelezea kwa ukweli uhusiano wako na Airbnb. Ikiwa usemi au sentensi ina maana sawa bila kutumia "Airbnb," iondoe.
 • Usitumie kamwe "Airbnb" kuelezea upangishaji wa muda mfupi, malazi ya muda mfupi, au usimamizi wa upangishaji kwa ujumla.

Itumie kwa usahihi

Fanya

 • Iandike "Airbnb" — neno moja, herufi kubwa "A." Si "AirBNB", "AirBnB" au "AirBnb", na haipaswi kamwe kuvunjwa kama "Air BNB" au "Air B&B".

USI...

 • Usibadilishe, kuongeza, au kuondoa chochote kwenye "Airbnb" — "Abb," "Airbnb-ish," "Airbnb-er" hazikubaliki.
 • Usitumie "Airbnb" kama kitenzi.
 • Tena, kwa sababu tunasisitiza hili kwa uzito, kamwe usitumie "Airbnb" kuelezea upangishaji wa muda mfupi, malazi ya muda mfupi, au usimamizi wa upangishaji kwa ujumla.

Mifano

Sahihi: Ya Kweli na yenye Maelezo

Si sahihi: Inachanganya, inapotosha

Sisi ni Kampuni ya Usimamizi wa Nyumba inayojishughulisha na matangazo ya Airbnb

Sisi ni Kampuni ya Usimamizi ya Airbnb

Tunatoa huduma za kufanya usafi wa kitaalamu kwenye nyumba za kwenye Airbnb

Huduma za kufanya usafi wa kitaalamu kwenye Airbnb

Vidokezi vyangu kuhusu Kuwa Mwenyeji kwenye Airbnb

Mpango wa Mafunzo wa Airbnb

Ninashauku sana ya kuwa Mwenyeji wa Airbnb

Tunaweka nyumba yetu kwenye Airbnb

Niliomba kazi kwenye Airbnb

Tuliweka nyumba hii nzuri kwenye Airbnb

Kikundi cha Mitandao ya Kijamii cha Wenyeji wa Airbnb

Kikundi cha Wenyeji wa Airbnb wa [Jiji/Nchi]

Kwa Kampuni za Usimamizi wa Nyumba

Ikiwa ungependa kutangaza kampuni yako ya usimamizi wa upangishaji wa muda mfupi, miongozo iliyo hapo juu inakuhusu pia. Tafadhali kumbuka pia kutojiita "Kampuni ya Usimamizi ya Airbnb," au kudai "uhusiano wa kipekee" na Airbnb ambao unaweza kuwachanganya watumiaji kuamini kwamba una uhusiano na Airbnb. Unaweza kutaja kwamba unasimamia au kuhudumia nyumba zilizotangazwa kwenye Airbnb, lakini Airbnb haipaswi kuwa kitovu cha tovuti yako au nyenzo nyingine za matangazo.

Ikiwa una tovuti, lazima ujumuishe tamko la wazi la jumla kwenye tovuti yako kama ifuatavyo, "[jina la kampuni yako] ni kampuni nyingine huru inayojitegemea na haijaidhinishwa au kuhusishwa na Airbnb, Inc. au washirika wake". Ikiwa una kikokotoo cha mapato, fomu ya mawasiliano, au unasaji mwingine wowote wa data ya mtumiaji kwenye tovuti yako, tafadhali onyesha kanusho hilo kwa uwazi chini ya kitufe cha CTA.

Kwa Washirika

Washirika lazima wawe na ruhusa ya maandishi ili watumie alama zetu za biashara. Ikiwa una ruhusa ya kutumia alama zetu za biashara, unahitajika kufuata miongozo ya hivi karibuni ya chapa iliyotolewa na mtu unayewasiliana naye wa Airbnb ambaye anaweza kujibu maswali yoyote kuhusu miongozo hii au ya ziada.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili