Kurejelea usafiri kwa usalama
Pata vidokezi vya hivi karibuni kuhusu usafiri wakati wa
janga la COVID-19 na baadaye.
Usalama ni jukumu la kila mtu
Tunaiomba jumuiya ya Airbnb ifuate mazoea yetu ya afya na usalama ya COVID-19.
Kuvaa barakoa
Kuepuka mikusanyiko
Usafi wa kina
Viwango vya juu kwa ajili ya kila sehemu ya kukaa
Mchakato wetu wa kufanya usafi wa kina wa hatua tano, ambao unaungwa mkono na wataalamu, unatimiza zaidi ya kufanya usafi wa kawaida na ni hatua muhimu ambayo Wenyeji wanaweza kuchukua ili kusaidia kuhakikisha usalama wa jumuiya yetu.
Sehemu ya kujitegemea, mbali na umati wa watu
Nyumba za kujitegemea. Kuingia bila kukutana ana kwa ana. Sehemu pana za nje. Chumba chenye nafasi ya kutosha kupumua. Tafuta sehemu za kukaa zilizo na vistawishi ambavyo ni muhimu sana kwako.
Majibu kwa maswali yako
Wenyeji wote wanatakiwa kufuata mazoea yetu ya usalama na kufanya usafi ya COVID-19. Pata maelezo zaidi kuhusu Kufanya Usafi wa Kina wa Airbnb.
Inapohitajika na sheria au miongozo ya eneo husika, Wenyeji na wageni wote lazima wakubali kuvaa barakoa au kitambaa cha kufunika uso wakati wanaingiliana ana kwa ana na wadumishe umbali wa futi 6 (mita 2) kati yao. Na bila shaka tunapendekeza usikaribishe wageni au kusafiri ikiwa umekaribiana na mtu aliyeambukizwa COVID-19 au ikiwa una dalili za ugonjwa huo. Tathmini matakwa yetu ya afya na usalama kwa ajili ya sehemu za kukaa.
Wakati wowote unaweza kuwasiliana na Mwenyeji ukiwa na maswali mahususi kuhusu mazoea yake ya afya na usalama katika programu ya Airbnb.
Ikiwa unahitaji kubadilisha au kughairi nafasi uliyoweka, tembelea sehemu yaSafari ya tovuti au programu ya Airbnb kwa maelezo zaidi kuhusu machaguo yako ya sasa ya kughairi. Tumetengeneza nyenzo hii ili kuwasaidia wageni wapitie michakato na sera za kughairi.
Aidha, wageni ambao hawawezi kusafiri kwa sababu wanaugua COVID-19 wanaweza kustahiki kughairi nafasi waliyoweka na kurejeshewa fedha zote kwa kuwasiliana na usaidizi kwa wateja. Pata maelezo zaidi kuhusu sera yetu ya sababu zisizozuilika.
Matukio ya Airbnb yamefunguliwa tena katika nchi ambazo sheria husika za serikali zinaruhusu. Wageni na Wenyeji wanatarajiwa kufuata mazoea mahususi ya usalama kwa ajili ya Matukio ya ana kwa ana, ikiwemo kuepuka mikusanyiko na kuvaa barakoa wanapohitajika kufanya hivyo na sheria au miongozo ya eneo husika. Na bila shaka, kaa nyumbani ikiwa umekuwa katika hali ya kuweza kuambukizwa COVID-19 au unajisikia mgonjwa. Pata maelezo zaidi kuhusu Miongozo yetu ya afya na usalama wa Matukio.
Ikiwa ungependelea kufanya Tukio na kundi lako pekee, unaweza kuzingatia kuweka nafasi binafsi. Ikiwa hujihisi huru kukusanyika katika makundi au ikiwa Matukio ya ana kwa ana bado hayajafunguliwa tena katika soko lako, angalia Matukio yetu ya mtandaoni.
Sera za kughairi huwekwa na Wenyeji na hutofautiana kati ya matangazo. Unaweza kupata maelezo kuhusu sera ya kughairi ya kila sehemu ya kukaa kwenye ukurasa mkuu wa kila tangazo. Tumeweka kichujio kipya cha utafutaji ili iwe rahisi kwako kupata maeneo yenye sera za kughairi zinazoweza kubadilika. Pata maelezo zaidi kuhusu kichujio hicho kipya.