Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

    Jinsi ya kuunda kisa chako

    Wenyeji Bingwa Tereasa na David wanashiriki mikakati yao ya kusimulia kisa.
    Na Airbnb tarehe 22 Ago 2023
    Inachukua dakika 7 kusoma
    Imesasishwa tarehe 22 Ago 2023

    Vidokezi

    • Kutafuta, kuunda na kushiriki kisa chako ni njia ya kuungana na wageni

    • Fikiria kuhusu matukio katika nyumba yako au eneo ambayo wageni hawawezi kuyapata mahali pengine popote

    • Kuza mazingira ya nyumba yako kupatikana kwenye mitandao ya kijamii

    • Kichukulie kila kikwazo kama fursa ya kujifunza na kukua

    • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni

    Wenyeji Bingwa Tereasa na David wanajua mambo kadhaa kuhusu usimulizi wa kisa. Kama wazazi, wahifadhi wa mazingira, wakurugenzi wa ubunifu, waandishi waliochapishwa na wamiliki wa Camp Wandawega huko Elkhorn, Wisconsin, wamejifunza jinsi kusimulia kisa kunavyoweza kuwaleta watu pamoja. "Tulipoanza kugundua na kuchapisha maelezo ya historia ya kambi hiyo—kama sehemu ya klabu cha pombe cha miaka ya 1920, mahali pa majambazi kukutania, danguro, kambi ya majira ya joto kwa ajili ya jumuiya ya wakimbizi ya Kilatvia na vilevile uhusiano wetu na hiyo nyumba—tuligundua kwamba watu kweli waliipenda," anasema Tereasa.

    Hapa, wanashiriki maneno yenye busara kuhusu jinsi ya kupata na kutunga hadithi ya nyumba yako.

    1. Pata kivutio chako

    Tereasa: "Hata kama sehemu yako si jengo la klabu cha pombe la karne moja iliyopita, daima kuna kisa kusimulia. Ili kupata yako, anza kwa kuchimba:

    • Nini historia ya nyumba yako?
    • Ni matukio gani ambayo ni ya kipekee kwa mji wako ambayo wageni hawawezi kuyapata mahali pengine popote?
    • Je, ni vidokezi vipi vya kupendeza unavyoweza kuchukulia juujuu tu?

    Fanya utafiti na uviweke katika tangazo lako."

    David: "Kuna vitu vingi zaidi ambavyo unaweza kushiriki katika tangazo lako mbali na idadi ya vyumba vya kulala na mabafu. Watu wangependa kujua ni wapi wanaweza kunywa kikombe cha kahawa safi, wangependa kujua sehemu unazozipenda—kwa hivyo shiriki vitu vya kipekee kuhusu uzoefu unaoweza kutoa. Wageni wanatafuta uhusiano na sababu ya kushiriki kimihemko na visa vinatusaidia kuja pamoja."

    2. Usiwe mkamilifu

    David: "Tangu mapema sana, tulijifunza kwamba tunahitaji kudhibiti matarajio ya watu kabla ya wakati kwa sababu tusingependa kamwe kuwavunja moyo. Kwa hivyo tuliunda Ilani yetu ya Matarajio ya Chini. Ni njia ya ucheshi kwetu kuanzisha maisha ya kambi ya mashambani. Huwaambia watu nini cha kutarajia—kitu ambacho mara nyingi ni wadudu wanaoudhi, viumbe wa msituni na ukosefu kabisa wa viyoyozi—kwa hivyo ikiwa unahitaji mashuka ya Misri au anasa za kisasa, eneo hili huenda lisikufae."

    Tereasa: "Sisi hatujifanyi. Na kwa hivyo tunaegemea hapo kwa lugha tunayotumia kuelezea sehemu yetu. Tuliamua kuwaambia watu ukweli. Tulitumia mtindo wa sauti ambao ni wenye ucheshi lakini wa kweli. Utani huwa mwingi sana kwetu nao hutuletea ucheshi, hatua ambayo, kwa maoni yangu, hufanya tuwe wenye kufikika zaidi. Na si lazima uwe mwandishi wa matangazo ili uweze kufikika—unaweza kuelezea tu eneo lako kwa njia ya unyenyekevu."

    David: "Wakati ninavinjari Airbnb, mimi hupenda jinsi utu wa mtu unavyojitokeza kwa namna anayvoelezea eneo lake. Hasa ikiwa tutashiriki sehemu, ningependa kujua wewe ni mcheshi na ni mtu ambaye ningependa kushinda naye. Usijaribu kunilaghai. Usijaribu kujifanya kuwa mtu bora zaidi ulimwenguni. Kuwa mkweli tu na mwaminifu na mwenye kufurahisha kwa sababu watu wanataka kujihisi starehe wanapokuja kukaa katika eneo lako.”

    3. Fanya mambo kijamii

    Tereasa: "Ili kuongeza mvuto na uwekaji nafasi, iweke nyumba yako kwenye mitandao ya kijamii. Watu wengi hutupata kwenye mitandao ya kijamii kwanza. Wanaziona picha zetu au kupitia taarifa ya Instagram—ni njia nzuri sana ya kuongeza hadhira na kuwaalika katika kufurahia fursa wanazoweza kupata kwenye kambi. Vidokezi kadhaa:

      • Jaribu kushiriki wasaa wa maisha ambao watu wanataka kuushiriki. Ungependa kuwa na kitabu kando ya kitanda na kikombe cha kahawa moto huku ukiona mandhari nje ya dirisha—yote.
      • Mtindo mzuri na picha nzuri ni kipengele muhimu kwa masimulizi ya picha. Ifanye iwe ya kuvutia na nzuri!"

      David: "Watu wanapotembelea Wandawega, siwezi kukumbuka ni mara ngapi watu wameniambia kwamba wameona picha kwenye Instagram na wanataka kupiga mbio kwenda hapo ili kuunda upya wasaa huo kwa ajili yao wenyewe. Instagram inakuwa chombo cha orodha ya wasaa—na hakiki ya mtandaoni ya sehemu yako kwa ajili ya hadhira yako. Mara nyingi hiyo inaweza kuwa sababu ya sehemu yako kuwekewa nafasi."

      Usijaribu kujifanya kuwa mtu bora zaidi ulimwenguni. Kuwa mkweli tu na mwaminifu na mwenye kufurahisha.
      David,
      Elkhorn, Wisconsin

      4. Endelea "kukabiliana na mapungufu"

      David: "Hapo mwanzoni, tulifanya makosa mengi. Lakini tumejifunza kukumbatia kile tunachokiita kutaja mapungufu mapema—na shida za maisha. Kwa mfano, kupitia usimulizi wa kisa, tulijifunza kwamba kuna kitu kinachoitwa kushiriki kupita kiasi. Ingawa watu hupenda visa vya kahaba kwenye danguro, mafia na mauaji—haimaanishi kwamba lazima wanapenda kujua wapi ilitokea—hasa ikiwa lazima walale huko. Baada ya muda, utagundua kile kinachofanya kazi, kisichofanya kazi na kile ambacho hadhira yako inapenda.”

      Tereasa: "Kutaja mapungufu mapema, kwa maoni yetu, ni kikiona kila kikwazo kama fursa ya kukua. Ndivyo unavyojifunza."

      5. Shiriki safari

      Tereasa: "Tulipoanza safari hii mara ya kwanza, nilikuwa na hofu kubwa ya kushiriki picha zetu za 'zamani'. Nilidhani hakuna mtu ambaye angekubali kuja kukaa nasi kwa sababu ya jinsi mambo yalivyoonekana yenye kutisha. Lakini kwa kweli tumepata uhusiano mzuri zaidi kwa kutumia picha za 'zamani na za hivi karibuni'.

      David: "Watu hupenda uaminifu. Wanataka kuona mchakato. Kwa kurudia tena, wanatafuta uhusiano binafsi—kwa hivyo usiogope kushiriki sehemu za safari ya maisha yako. Uwe mkweli na usimulie kisa chako kipekee."

      Vidokezi

      • Kutafuta, kuunda na kushiriki kisa chako ni njia ya kuungana na wageni

      • Fikiria kuhusu matukio katika nyumba yako au eneo ambayo wageni hawawezi kuyapata mahali pengine popote

      • Kuza mazingira ya nyumba yako kupatikana kwenye mitandao ya kijamii

      • Kichukulie kila kikwazo kama fursa ya kujifunza na kukua

      • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili ili kuboresha huduma yako ya kukaribisha wageni
      Airbnb
      22 Ago 2023
      Ilikuwa na manufaa?