Kughairi wakati wa ukaaji wako
Iwapo jambo lolote lisilotarajiwa litatokea wakati wa ukaaji wako, tunapendekeza umtumie Mwenyeji wako ujumbe ili mjadiliane kuhusu suluhisho kwanza. Kuna uwezekano kwamba atakusaidia kulirekebisha mara moja. Ikiwa ungependa kuomba kurejeshewa fedha au kughairi nafasi uliyoweka, tunaweza kukusaidia kutuma ombi kwa Mwenyeji wako.
Mtumie Mwenyeji wako ujumbe
Kwa ujumla, ni wazo zuri kujaribu kuzungumza na Mwenyeji wako kwanza. Unaweza kumtumia Mwenyeji wako ujumbe moja kwa moja kutoka kwenye kikasha chako ili kujadili suluhisho. Mkikubaliana na Mwenyeji wako kuhusu suluhisho, kuna uwezekano mkubwa kwamba ombi lako litaidhinishwa. Iwapo tatizo lako tayari limetatuliwa na Mwenyeji wako na unaweza kuendelea na ukaaji wako, basi ruka hatua zifuatazo.
Tuma ombi ndani ya saa 24
Iwapo bado unahitaji kughairi nafasi uliyoweka wakati wa ukaaji wako, tunaweza kukusaidia kutuma ombi la kutatua tatizo hilo kwa Mwenyeji wako. Unapofanya hivi, unaweza kuchagua kumwomba Mwenyeji wako atatue tatizo, uombe kurejeshewa sehemu ya fedha au uombe kughairi nafasi uliyoweka ili urejeshewe fedha zote. Akikubali ombi lako, fedha unazorejeshewa zitatumwa kwenye njia ya malipo uliyotumia ulipoweka nafasi. Ikiwa Mwenyeji wako atakataa au hatajibu, unaweza kuiomba Airbnb iingilie kati ili kukusaidia.
- Kusanya ushahidi: Ikiwezekana, piga picha au video ili uweke kumbukumbu ya matatizo kama vile kistawishi kinachokosekana au kilichovunjika.
- Wasilisha ombi kwa Mwenyeji wako: utaelezea tatizo hilo, utatoa picha ukiweza na kumjulisha Mwenyeji jinsi ungependa kulitatua. Ni muhimu kupata msaada ndani ya saa 24 baada ya kugundua tatizo hilo. Vinginevyo, kiasi cha fedha unazorejeshewa kinaweza kuathirika.
- Subiri jibu lake: Akikataa au asipojibu ndani ya saa 1, unaweza kuiomba Airbnb iingilie kati ili kukusaidia. Airbnb itarejelea Sera ya Kurejesha Fedha ya Mgeni ili kukusaidia kutatua tatizo hilo.
Makala yanayohusiana
Kuomba kurejeshewa fedha
Je, unahitaji kurejeshewa fedha? Hatua yako ya kwanza ni kutuma ujumbe kwa Mwenyeji wako ili kulirekebisha. Ikiwa hawezi kulirekebisha, anaw…- Mgeni
Sera ya Kuweka Nafasi Tena na Kurejeshewa Fedha
Tafadhali kagua Sera yetu ya Kuweka Nafasi Tena na Kurejeshewa Fedha. - Mgeni
Omba kurejeshewa fedha
Maombi ya kurejeshewa fedha ya kiasi chochote yanapaswa kushughulikiwa kupitia Kituo chetu cha Usuluhishi.