Ruka kwenda kwenye maudhui
  Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Je, nitaandaaje tukio la mtandaoni?

  Kwanza, wasilisha wazo lako kwa ajili ya tukio la mtandaoni. Katika mchakato wa kuwasilisha, tia alama kwenye kisanduku ukionyesha kwamba linafanyika mtandaoni unapoweka eneo lako.

  Matukio ya mtandaoni yanafanyika kwenye Zoom.Zoom ni tovuti ya wahusika wengine inayotoa huduma ya mikutano kwa njia ya video na inaweza kutumiwa kwenye kompyuta, tabuleti na vifaa vya mkononi.

  Uwasilishaji na tathmini ya Airbnb

  Ruhusu wiki 2-4 zipite baada ya kuwasilisha kwa ajili ya tathmini na idhini.Kila tukio la mtandaoni hutathminiwa ili kuhakikisha kuwa linakidhiviwango vyetu vya ubora, ikiwemo mahitaji ya ziada kwa ajili ya matukio ya mtandaoni.Ikiwa tukio lako halikufuzu tathmini, utapokea barua pepe na unakaribishwa kuwasilisha wazo jipya.

  Jinsi ya kuunda akaunti ya Zoom

  Baada ya tukio lako kuwasilishwa na kukubaliwa ili kuchapishwa, utapewa akaunti ya Zoom bila malipo ili uitumie tu kwenye tukio lako la mtandaoni kwenye Airbnb.

  Utapewa kidokezi cha kuanzisha akaunti yako ya Zoom katika mipangilio ya tukio lako. Utapokea barua pepe ambayo itakupitisha kwenye hatua chache za kuunda akaunti yako ya Zoom na mwaliko wa kujiunga na mkutano wa majaribio. Mara utakapokamilisha mchakato, akaunti yako ya Zoom itawezeshwa.

  Kumbuka inaweza kuchukua hadi dakika 30 baada ya kukamilisha hatua zote kabla ya hali ya uwezeshaji wa Zoom kusasishwa.

  Kupata kiunganishi chako cha Zoom na nenosiri

  Unaweza kupata kiunganishi mahususi kwa kila kisa cha tukio lako kwenye kalenda, katika barua pepe ya uthibitisho inayotumwa kila wakati mgeni anapoweka nafasi na katika barua pepe ya kumbusho iliyotumwa kabla ya tukio lako kuanza.

  Kutatua matatizo ya Zoom

  Ikiwa una tatizo linalohusiana na Zoom, tafadhali wasiliana na timu ya usaidizi ya Zoom.Unaweza pia kupata taarifa katika Kituo cha Msaada cha Zoom.

  Jinsi wageni wanavyoweka nafasi

  Wageni wataweka nafasi ya tukio lako la mtandaoni kwenye Airbnb kwa kufuata njia ileile kama kwenye Matukio ya Airbnb ya ana kwa ana. Kutumia kipengele cha "chumba cha wanaosubiri" kilichopo kwenye Zoom hukuwezesha kudhibiti wale wanaojiunga na tukio lako.Ikiwa mgeni anashiriki kiunganishi cha Zoom na mgeni mwingine ambaye hakujumuishwa katika nafasi yake aliyoweka, si lazima umwalike ajiunge.

  Jinsi upangaji bei unavyofanya kazi

  Kiasi cha malipo ni uamuzi wako mwenyewe.Tunashauri uanze na bei ya chini, kisha ukipata mazoezi ya kutosha na tathmini za nyota 5, unaweza kuongeza kiasi unacholipisha.Kama tu matukio ya ana kwa ana, Airbnb itamtoza mwenyeji ada ya huduma, isipokuwa kama tukio hilo ni Wajibu kwa Jamii.

  Matukio ya mtandaoni huwekewa bei chaguo-msingi kwa kila mtu. Ikiwa nafasi iliwekewa mgeni mmoja lakini unatambua kuna wageni 2, unaweza kumwomba amlipie yule mtu wa ziada katika Kituo cha Usuluhishi.Hata hivyo, ikiwa unaruhusu wageni kadhaa kujiunga kwa kutumia kifaa kimoja, unaweza kuwajulisha wageni kuwa wanahitaji tu kuweka nafasi moja kwenye ukurasa wako wa tukio chini ya Utakachofanya na Jinsi ya Kushiriki.

  Makala yanayohusiana
  Ulipata msaada uliohitaji?