Omba kurejeshewa fedha
Ikiwa ungependa kuomba urejeshewe fedha kabla au baada ya safari yako, maombi ya kurejeshewa fedha za kiasi chochote yanaweza kushughulikiwa kupitia Kituo chetu cha Usuluhishi.
Tunapendekeza ujadili kiasi chochote cha fedha za kurejeshewa na Mwenyeji wako kupitia uzi wako wa ujumbe wa Airbnb kabla ya kuwasilisha ombi katika Kituo cha Usuluhishi. Hata hivyo, ikiwa wewe na Mwenyeji wako mmeshindwa kukubaliana ndani ya saa 72, utakuwa na chaguo la kuiomba Airbnb iwasaidie kupata suluhisho.
Kumbuka: Una hadi siku 60 baada ya tarehe ya kutoka ya nafasi uliyoweka kuwasilisha ombi kwenye Kituo cha Usuluhishi.
Iwapo unakumbana na tatizo wakati wa ukaaji wako, tutakusaidia kumwomba Mwenyeji wako alirekebishe, kuomba urejeshewe fedha au kuomba kughairi ili urejeshewe fedha zote. Ni muhimu kuwasilisha ombi ndani ya saa 24 baada ya kugundua tatizo hilo la usafiri. Mwenyeji wako atakuwa na saa 1 ya kujibu. Akikataa au asipojibu, unaweza kuiomba Airbnb iingilie kati ili kukusaidia.