Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Utaratibu wa msingi wa kukaribisha wageni kwenye Airbnb

  Je, una sehemu ya kukodisha? Pata pesa kama Mwenyeji wa Airbnb. Hii hapa ni jinsi ya kuanza.
  Na Airbnb tarehe 20 Nov 2019
  Inachukua dakika 2 kusoma
  Imesasishwa tarehe 2 Sep 2021

  Vidokezi

  • Watu hukaribisha wageni kwenye Airbnb kwa sababu nyingi, kama vile kupata pesa za ziada au kuweka akiba kwa ajili ya kustaafu

  • Weka bei yako, ni usiku upi unakaribisha wageni na unalipwa vipi

  • Unda tangazo lenye maelezo ya kweli—na utoe sehemu safi yenye vistawishi vya msingi

  • Wasiliana na wageni haraka na kwa njia dhahiri

  Wenyeji wengine hutumia mapato yao ya Airbnb ili kulipia kustaafu. Wengine huyatumia kufadhili miradi waipendayo. "Nimeweza kutengeneza nguo kwa miaka mitatu katika Chuo cha Sanaa cha Morley," anasema mwenyeji Tessa kutoka London. "Nimeweza kusafiri na kukaribisha wageni kumenisaidia kulipia jiko jipya." Haijalishi malengo yako ya kifedha ni yapi, kukaribisha wageni kwenye Airbnb kunaweza kuwa njia nzuri ya kupata mapato ya ziada. Jifunze jinsi ya kuanza, kuanzia kuunda tangazo lako hadi kulipwa.

  Unaweza kuwa mwenyeji

  Kwa hivyo nini kinahitajika ili kuwa mwenyeji wa Airbnb? Kwanza, unahitaji kuwa na sehemu inayopatikana ya kushiriki na wasafiri. Iwe ni nyumba nzima, chumba cha ziada, au kitanda cha kustarehesha cha sofa, kuna uwezekano wa kuwa na mgeni ambaye atafurahia sehemu yako—cha muhimu ni kuunda tangazo la Airbnb ambalo, kwa uaminifu na kwa usahihi, linawaonyesha wasafiri nini cha kutarajia. Na unahitaji kuwa tayari kuwapa wageni wako ukarimu wenye uchangamfu, ambao kwa ujumla unamaanisha:

  1. Wasiliana kwa haraka na kwa uwazi
  2. Toa sehemu safi yenye vistawishi vya msingi vinavyohitajika kwa ajili ya ukaaji mzuri
  3. Weka vitu vyovyote vya ziada ambavyo unafikiri vitafanya sehemu yako kuwa maalumu

  Unachotoza ni juu yako

  Kwa kukaribisha wageni kwenye Airbnb, unaweza kutangaza nyumba yako kwa wasafiri bila masharti yoyote—hakuna ada za kujisajili au ada za uanachama. Na unaamua mwenyewe bei yako ya kila usiku. Unaweza kuweka bei maalumu kwa ajili ya misimu, wikendi na usiku mwingine wowote ambapo unataka kudhibiti kile unachotoza. Unaweza kuweka ada mwanzoni kwa ajili ya vitu kama vile wageni wa ziada au kufanya usafi wa nyumba*. Ikiwa unataka msaada wa kuamua ni kiasi gani cha kutoza, Airbnb ina nyenzo zinazolinganisha bei zako na mahitaji na zinapendekeza bei ya ushindani kwa kila usiku.

  Anza kuwekewa nafasi

  Mara baada ya kutangaza sehemu yako kwenye Airbnb, utaanza kupata maulizo na kuwekewa nafasi na wageni. Airbnb inamtoza kila mgeni kabla ya kuwasili ili kuhakikisha kuwa kila mara utalipwa kwa wakati unapokaribisha wageni. Huhitaji kushughulikia pesa moja kwa moja.

  Lipwa baada ya kuingia

  Unaweza pia kuchagua jinsi unavyolipwa, kwa kutumia njia kama vile amana ya moja kwa moja ya benki au PayPal. Airbnb kwa kawaida hutoa malipo yako takribani saa 24 baada ya saa iliyoratibiwa ya mgeni wako kuwasili. Inaweza kuchukua siku kadhaa ili pesa hizo kuingia kwenye akaunti yako. Malipo yako yatakuwa ni bei yako ya kila usiku ukiondoa ada ndogo ya huduma. Airbnb haitozi ada zozote za kuchakata kadi za benki, kwa hivyo inafanya iwe rahisi kwa wageni kuweka nafasi kama ilivyo kwa wenyeji kulipwa.

  *Ukiondoa Wenyeji wanaotoa malazi nchini China Bara.Pata maelezo zaidi Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Vidokezi

  • Watu hukaribisha wageni kwenye Airbnb kwa sababu nyingi, kama vile kupata pesa za ziada au kuweka akiba kwa ajili ya kustaafu

  • Weka bei yako, ni usiku upi unakaribisha wageni na unalipwa vipi

  • Unda tangazo lenye maelezo ya kweli—na utoe sehemu safi yenye vistawishi vya msingi

  • Wasiliana na wageni haraka na kwa njia dhahiri

  Airbnb
  20 Nov 2019
  Ilikuwa na manufaa?