Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Kuandika maelezo yenye ufanisi kuhusu eneo lako

  Wasaidie wageni wajione wakiwa katika sehemu yako kwa kutumia maelezo dhahiri na sahihi.
  Na Airbnb tarehe 18 Nov 2020
  Inachukua dakika 8 kusoma
  Imesasishwa tarehe 11 Okt 2022

  Vidokezi

  • Zingatia kile kinachofanya sehemu yako iwe ya kipekee

  • Kuwa mkweli kuhusu eneo lako ili uweke matarajio mapema

  • Sasisha maelezo ya tangazo lako

  Tumejifunza kutoka kwa Wenyeji Bingwa kwamba si lazima eneo lako liwe kamilifu ili liwe maarufu, lakini unahitaji kuwajulisha wageni hasa kile watakachopata watakapowasili.

  Kuandika maelezo mazuri kuhusu eneo lako ni mojawapo ya njia bora za kuweka matarajio na kuwekewa nafasi. Hivi ndivyo unavyoweza kuwafanya wasafiri wafurahie kukaa katika sehemu yako.

  Andika kichwa cha kuvutia

  Kichwa cha tangazo lako ndilo jambo la kwanza ambalo wageni husoma, pamoja na picha ya jalada lako, huwafanya wachunguze ukurasa wa tangazo lako. Kitumie kuelekeza uangalifu kwenye vipengee vikuu vya sehemu yako.

  Hii ni mifano michache ya vichwa bora:

  • Nyumba ya mbao yenye starehe iliyo na jiko la mpishi
  • Studio inayofaa mbwa karibu na LAX
  • Vila ya ufukweni iliyo na kayaki

  Una herufi 32, ikiwa ni pamoja na nafasi, ili kuchochea hamu ya wageni ya kupata maelezo zaidi kuhusu eneo lako. Kwa nini ni chache sana? Vichwa vifupi hufaa zaidi kwenye simu mahiri na kompyuta kibao, ambazo hutumiwa katika asilimia 75 ya utafutaji wote kwenye Airbnb.

  Epuka kutumia emoji au alama na utumie herufi kubwa mwanzoni mwa majina maalumu pekee (kama vile "Yellowstone") na vifupisho vya kawaida (kama vile "LAX").

  Soma miongozo yetu ya kuandika vichwa

  Zingatia vipengele maalumu

  Kuna mamilioni ya sehemu za kukaa kwenye Airbnb. Ili kuonyesha kile ambacho ni cha kipekee kuhusu tangazo lako, tumia dakika chache kufikiria kuhusu vipengele vinavyofanya tangazo lako liwe tofauti, kama vile eneo lake au vistawishi vyake.

  Kulingana na hali yako, unaweza kutambua:

  • "Tuko umbali wa kutembea kwa dakika 10 kutoka kwenye viwanda viwili bora vya kutengeneza pombe mjini."
  • "Njia maarufu za baiskeli za mlimani za eneo hili zipo umbali wa dakika 15 tu za kuendesha baiskeli au dakika tano za kuendesha gari."

  Ili uhamasishwe, jaribu kusoma maelezo ya tangazo yaliyoandikwa na Wenyeji wengine na uangalie tathmini zao. Utaweza kupata maelezo kuhusu aina za taarifa na vistawishi ambavyo watu wanathamini sana katika tangazo.

  Simulia kuhusu sehemu yako

  Maelezo yako ni pale ambapo unaitangaza sehemu yako, usimulizi ni sehemu muhimu ya uuzaji wenye ufanisi. Si lazima uwe mwandishi mzuri ili uweze kuandika maelezo yanayovutia lakini ni lazima utumie lugha inayoeleweka na inayovutia.

  Ikiwa hujui jinsi ya kuanza, zungumza na rafiki na umweleze jinsi ilivyo kukaa kwenye eneo lako. Maelezo muhimu zaidi yanaweza kutoka mara moja, kwa njia ya mazungumzo ambayo hufanya maelezo ya tangazo yawe ya kina.

  Kisa unachosimulia kinaweza kuwa kuhusu huduma unayowapa wageni. Je, una fleti kwenye ghorofa ya juu ambayo imezungukwa na miti yenye kivuli? "Utahisi kama uko kwenye nyumba ya kwenye mti!" Chumba cha kawaida katika sehemu ya biashara ya jiji kinaweza kuwa “sehemu inayofaa kwa ajili ya kuvinjari jiji.”

  Tereasa na David, Wenyeji Bingwa huko Elkhorn, Wisconsin, wanasema kwamba kushiriki historia ya nyumba yao "kumewavutia" wageni wao. Wanapendekeza ujue jumuiya yako na ujue ni nini kinachovutia kuhusu nyumba yako au mji wako unapotunga simulizi lako.

  Usitumie maneno mengi

  Wageni wanaotafuta sehemu ya kukaa mara nyingi huchanganua maelezo ya tangazo kwa ajili ya vipengele muhimu bila kusoma kila neno. Fupisha maelezo ya tangazo lako, huku ukiweka taarifa muhimu mwanzoni, ili wageni wako watarajiwa wasitumie wakati mwingi kuitafuta.

  Kwa njia hiyo, jaribu kutorudia maelezo ambayo umeshiriki tayari. Kwa mfano, unaweza kutumia orodha kaguzi ya vistawishi ili kujumuisha vipengele vyote vinavyotolewa na sehemu yako, kama vile Wi-Fi, maegesho na kiyoyozi. Hii inaweka maelezo yako kuwa mafupi na pia inahakikisha kwamba tangazo lako litaonekana wakati wageni wanachuja kwa ajili ya vistawishi hivyo katika utafutaji wao.

  Kuwa mkweli na mwaminifu

  Kusifia mno au kutia chumvi kwenye maelezo kuhusu eneo lako kunaweza kusababisha maudhi na tathmini mbaya. Kueleza mambo kihalisi huwasaidia wageni kuamua iwapo sehemu yako inakidhi mahitaji yao kabla ya kuweka nafasi.

  "Kwenye tangazo lako, hakikisha kwamba unajumuisha maelezo ya vipengee vya kipekee kwenye nyumba yako," anasema Nikki, Mwenyeji Bingwa huko San Francisco. “Vieleze kwa namna ambayo ni ya kweli na wazi, bila kukatisha tamaa. Unahitaji kuonyesha uwazi wa kutosha ili kuwasaidia wageni wako wachague nyumba wanayoitaka.”

  Ni muhimu sana kuweka vipengele vya ufikiaji kisha kuangazia vipengele vya nyumba yako ambavyo vinaweza kuleta changamoto kwa baadhi ya wageni, ikiwemo wale walio na matatizo ya kutembea, watoto wadogo au wanyama vipenzi. Sehemu za "Maelezo mengine ya kuzingatia" na "Sehemu" za maelezo ya tangazo lako ni sehemu mbili ambazo unaweza kuweka taarifa hii.

  Tumia maelezo mafupi ya picha kikamilifu

  Picha zako zinazingatiwa sana katika uamuzi wa mgeni kuhusu iwapo atawekea nafasi sehemu yako na maelezo mafupi yanatoa fursa ya kuunganisha picha na huduma ambayo wageni watapata. Ukijikuta umechanganyikiwa kuhusu jinsi ya kuweka maelezo mafupi kwenye picha, fikiria kuhusu kile unachoweza kuongeza ambacho huenda kamera haijanasa.

  Ikiwa unaonyesha chumba cha kulala, waambie wageni wako ukubwa wa kitanda na utaje aina ya godoro, ikiwa inafaa. Je, una picha ya pembe yenye starehe dirishani? Unaweza kusema kwamba ni mahali pazuri pa kujikunja ukisoma kitabu jua linapotua.

  Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu wa kuweka tangazo lenye mafanikio

  Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Vidokezi

  • Zingatia kile kinachofanya sehemu yako iwe ya kipekee

  • Kuwa mkweli kuhusu eneo lako ili uweke matarajio mapema

  • Sasisha maelezo ya tangazo lako
  Airbnb
  18 Nov 2020
  Ilikuwa na manufaa?