Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Jinsi na wakati wa kuwasiliana na wageni

  Orodha kaguzi ya Mwenyeji wa Airbnb kwa ajili ya mawasiliano mazuri na wageni.
  Na Airbnb tarehe 8 Jan 2020
  Inachukua dakika 3 kusoma
  Imesasishwa tarehe 28 Jul 2021

  Vidokezi

  Mawasiliano mazuri yanaweka msingi bora kwa ajili ya uzoefu mzuri wa wageni. Kama Mwenyeji, unaweza kuwasaidia wageni kufurahia ukaaji mzuri (na kuchochea tathmini nzuri) kwa kuwasiliana waziwazi na mara moja kuanzia wakati ambapo wageni wanaonyesha kupendezwa na tangazo lako, hadi baada ya kutoka kwenye eneo lako.

  Vidokezi vya mawasiliano mazuri

  Uwe mnyofu: Mwenyeji Abhay kutoka San Francisco anasema yeye ni mnyofu kabisa kuhusu sehemu hii. Kwa mfano, anaeleza wazi kuwa anamiliki mbwa mkubwa ambaye anatoka manyoya na kwamba anapangisha vyumba viwili nyumbani kwake, kwa hivyo kunaweza kuwa na wageni wengine. "Wazo ni kuweka matarajio sahihi ili uweze kutoa uzoefu mzuri."

  Patikana: "Ninajitolea kujibu maswali mara moja," anasema Mwenyeji Chris kutoka Cleveland. "Ikiwa kitu chochote kinahitaji kurekebishwa, tunakishughulikia mara moja." Wenyeji wenye uzoefu hutumia majibu ya haraka na ujumbe ulioratibiwa ili kufanya mawasiliano na wageni yawe ya haraka na rahisi.

  Kuwa mwenye kujali: Matendo madogo ya fadhili yanaweza kufanya ukaaji kuwa uzoefu bora kwako na kwa wageni wako. "Kuna furaha unapokuwa mwenye fadhili kwa watu—kwa wageni ambao hujawahi kukutana nao—na kujaribu tu kushughulikia mahitaji yao," anasema Abhay. Tatizo likitokea, wageni mara nyingi husema kwamba cha muhimu kwao ni jinsi wenyeji wao wanavyojibu.

  Kuwa mjuzi: Kuwasiliana na wageni kwenye programu ya Airbnb husaidia kukulinda wewe, kwani mazungumzo yote hurekodiwa kwa makusudi ya kuyarejelea kwa ajili ya huduma kwa wateja. Pia inafanya iwe rahisi kupata taarifa muhimu za wageni.

  Nyakati muhimu za kuwasiliana na wageni

  Hatua ya maulizo: "Ninajaribu kuwapa wageni uzoefu ambao ningependa kupata ikiwa ningekuwa nasafiri," anasema Abhay. "Kwa hivyo ninajaribu kujibu mara moja."

  Kujibu maswali si muhimu tu kwa ajili ya kuwafurahisha wageni—ni mojawapo ya vigezo vya kuwa Mwenyeji Bingwa. Unaweza kutoa huduma yenye ukadiriaji wa nyota tano tangu mwanzo kwa kujibu maswali yote ya mgeni ndani ya saa 24, iwe ni kwa kukubali, kukataa au kutuma ujumbe. Unaweza pia kuokoa muda kwa kuweka majibu yako ya haraka, ambayo hufanya iwe rahisi kwako kujibu maswali yanayoulizwa sana na wageni.

  Ikiwa umechagua kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, hutapokea ujumbe wako wa kwanza kutoka kwa wageni hadi baada ya nafasi waliyoweka kuthibitishwa, isipokuwa uchague kufanya ujumbe wa kabla ya kuweka nafasi uhitajike kwenye mipangilio ya kipengele chako cha Kuweka Nafasi Papo Hapo.

  Wakati wa kuweka nafasi: Wageni wanafurahia wakati Wenyeji wanawatumia ujumbe wa "asante kwa kuweka nafasi". Ili kukurahisishia jambo hili, tumeunda ujumbe ulioratibiwa ambao unaweza kutuma moja kwa moja kwa wageni wakati wa kuweka nafasi. Hii pia ni fursa yako kuuliza maswali ya ziada kama vile kusudi la safari yao na ni nani ataandamana nao.

  Wazo ni kuweka matarajio sahihi ili uweze kutoa uzoefu mzuri.
  Abhay,
  San Francisco

  Kabla ya kuwasili: Jambo gumu zaidi katika usafiri mara nyingi huwa ni kufika mahali uendako, kwa hivyo maelezo dhahiri ya kuingia ni muhimu ili kuwasaidia wageni wako wasikabili usumbufu wakati wa kuwasili. Mara baada ya kuweka maelekezo yako ya kuingia kwenye sehemu ya "taarifa kwa ajili ya wageni" ya kichupo cha Matangazo, yatapatikana kiotomatiki kwa wageni katika kichupo chao cha Safari siku tatu kabla ya kuwasili. Yatajumuishwa pia katika Mwongozo wao wa Kuwasili saa 48 kabla ya kuingia, pamoja na maelekezo ya kwenda kwenye sehemu yako na taarifa ya Wi-Fi.

  Wakati wa kuingia: Ikiwa hutakuwepo ili kuwaonyesha wageni eneo lako, hakikisha wanaweza kupata mwongozo wa nyumba ambao unajumuisha taarifa mahususi kwa sehemu yako—kwa mfano, jinsi ya kutumia mfumo wa burudani, kiyoyozi, meko, Wi-Fi au kitu kingine chochote ambacho kitawasaidia kufurahia ukaaji wao.

  Baada ya ukaaji wa usiku wa kwanza: Wenyeji wengi wanasema wanapenda kuwasiliana na wageni wakati wa ukaaji wao. Inasaidia kuwa makini na kuuliza ikiwa kila kitu kiko sawa.

  Kabla ya kutoka: Ni muhimu kuwakumbusha wageni ni wakati gani wanahitaji kutoka, mahali pa kuacha ufunguo na chochote wanachohitaji kufanya katika sehemu hiyo kabla ya kuondoka, kama vile kuondoa taka.

  Baada ya kuondoka: Baadhi ya Wenyeji wanapenda kutuma ujume mfupi wa kuwashukuru wageni kwa ajili ya ukaaji wao. Ni wazo zuri kuwatathmini wageni wako mara moja vile vile—hii inawachochea kukuandikia tathmini pia, wakati wangali wanakumbuka maelezo kuhusu kile kilichofanya ukaaji wao kuwa mzuri.

  Vidokezi

  Airbnb
  8 Jan 2020
  Ilikuwa na manufaa?