Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kuweka ada zako za usafi

  Kurekebisha ada yako kwa muda tofauti wa kukaa kunaweza kukusaidia kuwa na ushindani.
  Na Airbnb tarehe 9 Nov 2021
  Inachukua dakika 2 kusoma
  Imesasishwa tarehe 10 Jun 2022

  Vidokezi

  Tunaelewa kwamba kuweka bei yako ni mojawapo ya sehemu ngumu zaidi za kukaribisha wageni. Kuifanya ipasavyo kunaweza kuwa tofauti kati ya kuwekewa nafasi au la. Bei yako ya kila usiku na ada zozote za ziada, zinapaswa kuleta usawa kati ya kulipia gharama zako za kukaribisha wageni na kutoa thamani bora zaidi kwa wageni wako.

  Ili kukusaidia kupata usawa huo, je, unajua kwamba unaweza kurekebisha ada zako za usafi kulingana na muda wa ukaaji wa mgeni?

  Kuweka ada za usafi kwenye tangazo lako

  Ada zako za usafi kwa kawaida hugharamia kufanya usafi ambayo ungetarajia kufanya baada ya kukaribisha mgeni yeyote, kama vile kutandika vitanda kwa mashuka yaliyosafishwa, kufuta kaunta na sehemu nyingine mbalimbali na kusugua masinki na vyoo. Ada za usafi zinaweza kukusaidia kulipia huduma ya kitaalamu ya utunzaji wa nyumba na vifaa vya kufanyia usafi.

  Kulingana na jinsi utakavyochagua kuweka ada yako ya usafi, unaweza kuchagua kufanya yoyote (au kutofanya chochote) kati ya yafuatayo:

  • Weka ada moja ya usafi isiyobadilika kwa wageni wote, bila kujali muda wao wa kukaa
  • Weka ada ya chini ya usafi kwa ukaaji wa usiku 1 au 2 pekee na udumishe ada yako isiyobadilika kwa ukaaji mwingine wote.
  • Weka ada ya mnyama kipenzi ili kulipia gharama za ziada za kufanya usafi unapokaribisha wageni walio na wanyama vipenzi

  Ada za usafi hazipatikani kwa Wenyeji wanaotoa malazi huko China Bara..

  Kujitayarisha kwa mafanikio

  Ni muhimu kusimamia matarajio kuhusu kilichojumuishwa kwenye ada zako za usafi na kile (ikiwa kuna chochote) unachowaomba wageni wafanye. Ungependa wageni wapakie vyombo vichafu kwenye mashine ya kuosha vyombo au kuondoa mashuka kitandani kabla ya kutoka? Ikiwa ndivyo, zingatia kutoza ada ndogo sana ya usafi—au kutotoza ada yoyote.

  Kukiwa ada ya juu, wageni wanaweza kutarajia kuondoka kwenye sehemu yako wakati wa kutoka kama vile wangefanya kwenye chumba cha hoteli.

  Katika tukio la nadra ambapo eneo au mali yako imeharibiwa na mgeni wakati wa ukaaji, AirCover kwa ajili ya Wenyeji inawapa Wenyeji USD milioni 1 za ulinzi dhidi ya uharibifu, ikijumuisha gharama ya kufanya usafi bila kutarajia. Unaweza kuomba kulipwa kupitia Kituo chetu cha Usuluhishi.

  Baadhi ya mazoea bora ya kukumbuka wakati wa kuweka ada ya usafi:

  • Nuia kutumia ada ya usafi kugharamia kufanya usafi—si kujipatia pesa za ziada.
  • Ikiwa wewe ni mpya kwenye huduma ya kukaribisha wageni, fikiria kusubiri kabla ya kuweka ada ya usafi hadi utakapokuwa na tathmini nzuri kadhaa ili kuvutia kuwekewa nafasi zaidi

  Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji si sera ya bima. Haiwalindi Wenyeji wanaotoa huduma ya sehemu za kukaa kupitia Airbnb Travel, LLC au Wenyeji nchini China Bara au Japani. Kumbuka kwamba vikomo vyote vya ulinzi vinaonyeshwa katika USD na kwamba kuna vigezo, masharti na vighairi vingine.

  Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Vidokezi

  Airbnb
  9 Nov 2021
  Ilikuwa na manufaa?