Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Jinsi ya kuweka tangazo bora

  Boresha tangazo lako kwa picha bora, bei ya ushindani, na zaidi.
  Na Airbnb tarehe 18 Nov 2020
  Inachukua dakika 6 kusoma
  Imesasishwa tarehe 1 Jul 2021

  Vidokezi

  • Andika maelezo ya tangazo ambayo ni ya kina na sahihi

   • Hakikisha kalenda yako na mipangilio ya kuweka nafasi imesasishwa

    • Sasisha tangazo lako
    • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili wa kuweka tangazo lenye mafanikio

    Tangazo lako ni muhimu — kwa kweli, ndiyo fursa yako ya kwanza ya kuvuta umakini wa wageni kwa picha nzuri, vistawishi maarufu na maelezo ya kina kuhusu nafasi yako. Pia ni muhimu kuweka kalenda na bei yako kwa uangalifu, jambo linalosaidia kuhakikisha kuwa unapata tu uwekaji nafasi unaotaka, unapotaka, na kwa bei sahihi.

    Sasisha ni wakati gani na jinsi ambavyo wanaweka nafasi

    Kama mwenyeji, una udhibiti kuhusu wakati gani na jinsi gani wageni wanaweka nafasi. Hapa kuna vipengele kadhaa vya kuzingatia:

    • Mipangilio ya kalenda: Weka kiwango cha chini na cha juu cha usiku ambacho mgeni anaweza kuweka nafasi, epuka maombi ya siku hiyo hiyo, na zaidi — yote ndani ya mipangilio yako ya kalenda. Usisahau kusasisha kalenda yako kwa kuzuia tarehe wakati utakapokuwa mbali au huwezi kukaribisha wageni.
    • Maombi ya kuweka nafasi: Kipengele hiki hukuruhusu kukagua ombi la kuweka nafasi kabla ya kulikubali. Hakikisha tu unamjibu mgeni ndani ya saa 24.
    • Kuweka Nafasi Papo Hapo: Wageni mara nyingi hutafuta tangazo lenye kipengele chaKuweka Nafasi Papo Hapo.

    Fanya tangazo lako liwe sahihi kwa maelezo muhimu

    Vidokezo hivi vinaweza kusaidia kulitofautisha tangazo lako kwa wageni watarajiwa katika matokeo ya utafutaji.

    • Andika maelezo ya kina. Hakikisha kichwa na maelezo yanaonyesha kitu chochote ambacho wageni wanapaswa kujua kuhusu sehemu yako, kama vile ukaribu na vivutio vya eneo husika. Kwa mfano, mwenyeji mmoja ambaye ana sehemu nzuri karibu na bahari anaandika, "Tembea kwenda ufukweni kutoka kwenye eneo lenye faragha."
    • Orodhesha vistawishi vyako. Kulingana na utafiti wa Airbnb*, vistawishi maarufu ni pamoja na Wi-Fi, huduma ya kuingia mwenyewe, meza ya kufanyia kazi kwa kompyuta mpakato, maegesho ya bila malipo na sehemu inayofaa wanyama, kwa hivyo hakikisha unaorodhesha kistawishi chochote unachotoa.
    • Jizatiti kwenye usafi. Ili kusaidia kuhakikisha usalama wa jumuiya yetu wakati wa COVID-19, tunahitaji wenyeji wote wanaotoa huduma ya malazi ** wajizatiti kwenye mchakato wa hatua tano za Airbnb za itifaki ya kufanya usafi wa kina.
    • Sheria za nyumba: Sheria za nyumba huweka matarajio kwa wageni na kuwapa kionjo cha mtindo wako wa kukaribisha wageni. Tumia sheria zako za nyumba kushiriki maelezo muhimu — kama vile sera ya kutovuta sigara — na wageni watarajiwa.

    Tumia picha maridadi ili kuvutia wageni

    Picha bora zinasaidia kuonyesha utu na mtindo wako, kwa hivyo ni busara kusasisha picha zako mara nyingi na kumbuka kuonyesha maelezo fulani.

    • Zingatia sana picha ya kwanza unayojumuisha. Pamoja na kichwa cha tangazo lako, hili ndilo jambo la kwanza wageni wataona katika matokeo ya utafutaji. “Ninapotafuta kwenye Airbnb, huwa ninaenda moja kwa moja kwenye picha. Kwa hivyo fikiria ni kipi kinachoitofautisha sehemu yako na nyingine, ”anasema mwenyeji Candida.
    • Jumuisha picha za tangazo lako lote. Kuongeza kama picha tatu za kila chumba kutoka pembe tofauti huwapa wageni ziara ya mtandaoni ya sehemu yako.
    • Andika maelezo yanayojieleza. Hakikisha maelezo ya picha zako yanawaambia wageni wako juu ya maelezo muhimu. Kwa mfano, usisahau kuelezea meza ya kuchezea mchezo wa pool au bafu ya kuoga kwa kujiloweka.
    • Angazia vipengele vya ufikiaji. Wageni wengi hutafuta vipengele vya ufikiaji , kwa hivyo ni muhimu kuongeza hivi kwenye maelezo na picha za tangazo lako.

    Angalia mafunzo yetu ya upigaji picha kwa vidokezo zaidi juu ya kupiga picha nzuri za tangazo

    Weka bei yako iwe ya ushindani

    Kiasi unachotoza kwenye tangazo lako ni juu yako. Haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia:

    • Wageni mara nyingi huweka kipaumbele kwenye bei wanapotafuta sehemu, kwa hivyo ni muhimu kuhakikisha kuwa sehemu yako inatoa thamani nzuri kwa pesa kwa eneo na vistawishi unavyotoa. “Tafuta mtandaoni na uangalie matangazo mengine, hoteli, na nyumba zinazokodishwa kwa muda mfupi katika eneo la karibu. Je, ni vitu gani vinapatikana? Wanatoza kiasi gani cha pesa?” anapendekeza Mwenyeji Bingwa Nick. Pata maelezo zaidi
    • Unapoweka bei yako ya kila usiku, inasaidia kuzingatia ada za ziada—kama vile ada za usafi**, ada za wageni wa ziada, ada za huduma na kodi—na jinsi zitakavyoathiri bei ya jumla ambayo wageni wako watalipa.
    • Ukiwa mwenyeji mpya, unaweza kuchagua kuanza na bei ya kila usiku ya chini kuliko wastani mpaka utakapokuwa na tathmini moja au mbili nzuri.
    • Kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki kinakusaidia kuweka bei ya ushindani kwa kurekebisha kiotomatiki bei yako kulingana na mahitaji ya matangazo kama lako.

    Pata maelezo zaidi kuhusu ada ya huduma

    Orodha kaguzi kwa ajili ya tangazo lenye mafanikio

    Uko tayari kunufaika zaidi na tangazo lako? Hapa kuna orodha kaguzi fupi ya kukusaidia kuanza:

    • Je, mipangilio yako ya kalenda imesasishwa?
    • Umejaribu Kuweka Nafasi Papo Hapo?
    • Je, maelezo ya tangazo lako na kichwa yanaeleweka vizuri na yanavutia?
    • Je, umeweka vistawishi vyako vyote?
    • Je, una picha kadhaa zenye ubora wa hali ya juu pamoja na maelezo ya picha?
    • Je, uliweka bei ya ushindani ya kila usiku?

    Mara tu unapoanza kukaribisha na kupokea maoni kutoka kwa wageni, ni wazo zuri kusasisha tangazo lako mara kwa mara, ukihakikisha muhtasari wako na picha zinaonyesha kile ambacho ni cha kipekee kweli kuhusu sehemu yako.

    *Ulifanywa na Timu ya Utafiti ya Airbnb mwezi Mei 2020, utafiti ulijumuisha wageni 2,660 wa Airbnb nchini Marekani, Uingereza, Kanada na Australia

    **Ukiondoa Wenyeji wanaotoa huduma ya malazi huko China Bara. Pata maelezo zaidi

    Taarifa zilizomo kwenye makala haya zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

    Vidokezi

    • Andika maelezo ya tangazo ambayo ni ya kina na sahihi

     • Hakikisha kalenda yako na mipangilio ya kuweka nafasi imesasishwa

      • Sasisha tangazo lako
      • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili wa kuweka tangazo lenye mafanikio
      Airbnb
      18 Nov 2020
      Ilikuwa na manufaa?