Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Jinsi ya kuweka ukurasa wa tangazo unaovutia

  Onyesha picha bora, bei yenye ushindani na kadhalika.
  Na Airbnb tarehe 18 Nov 2020
  Inachukua dakika 6 kusoma
  Imesasishwa tarehe 4 Okt 2022

  Vidokezi

  • Andika maelezo sahihi na jumuishi ya tangazo

   • Hakikisha kalenda yako na mipangilio ya kuweka nafasi imesasishwa

    • Fahamu jinsi ya kudumisha ushindani wa bei yako ya kila usiku

    Fursa yako ya kwanza ya kuwavutia wageni ni ukurasa wako wa tangazo, ambao unajumuisha kichwa, maelezo, picha, vistawishi na kadhalika. Unapoweka tangazo lako, ni muhimu uchague kwa uangalifu kalenda na mipangilio yako ya bei, jambo linalosaidia kuhakikisha kwamba unapata tu nafasi zinazowekwa unazotaka, unapozitaka na kwa bei sahihi.

    Dhibiti lini na jinsi gani wageni wanaweza kuweka nafasi

    Ukiwa Mwenyeji, unaweza kuamua lini na jinsi gani wageni wataweka nafasi kwenye eneo lako. Vipengele kadhaa vya kuzingatia:

    • Mipangilio ya kalenda: Weka idadi ya chini na ya juu ya usiku ambao mgeni anaweza kuweka nafasi, epuka maombi ya siku hiyohiyo na kadhalika, hayo yote ndani ya mipangilio ya kalenda yako. Usisahau kusasisha kalenda yako kwa kuzuia tarehe wakati utakapokuwa mbali au huwezi kukaribisha wageni.
    • Ombi la kuweka nafasi: Kipengele hiki hukuruhusu kukagua ombi la kuweka nafasi kabla ya kulikubali. Hakikisha tu unamjibu mgeni ndani ya saa 24.
    • Kuweka Nafasi Papo Hapo: Wageni mara nyingi hutafuta tangazo lenye kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo, ambacho kinawaruhusu wageni kuweka nafasi kwenye tangazo lako bila idhini ya awali. Hii pia inaashiria kwamba uko tayari kumkaribisha mtu yeyote anayekidhi vigezo vyako vya kuweka nafasi, sehemu muhimu sana ya kuwa Mwenyeji jumuishi.

    Fanya tangazo lako liwe sahihi kwa maelezo muhimu

    Vidokezi hivi vinaweza kusaidia kulitofautisha tangazo lako kwa wageni watarajiwa katika matokeo ya utafutaji ya Airbnb.

    • Andika maelezo ya kina.Hakikisha kwamba kichwa na maelezo yanaonyesha kitu chochote ambacho wageni wanapaswa kujua kuhusu sehemu yako, kama vile kuwa karibu na vivutio vya nje katika eneo lako. Kwa mfano, Mwenyeji ambaye ana sehemu yenye starehe karibu na bahari anaweza kuandika "Likizo ya ufukweni yenye starehe" kama kichwa cha tangazo lake.
    • Tumia lugha jumuishi. Onyesha wazi katika maelezo ya tangazo lako kwamba unakaribisha watu wa aina zote.
    • Orodhesha vistawishi vyako.Vistawishi maarufu vinajumuisha Wi-Fi, huduma ya kuingia mwenyewe, meza ya kufanyia kazi kwa kompyuta mpakato, maegesho ya bila malipo na sehemu inayofaa wanyama vipenzi, kwa hivyo hakikisha kwamba unaorodhesha kistawishi chochote unachotoa.
    • Shiriki sheria za nyumba yako. Hizi huweka matarajio kwa wageni na kuwapa kionjo cha mtindo wako wa kukaribisha wageni. Tumia sheria za nyumba yako ili kushiriki taarifa muhimu kama vile sera ya kutovuta sigara na wageni watarajiwa.

    Tumia picha maridadi ili kuvutia wageni

    Picha zinazovutia husaidia kuonyesha haiba na mtindo wako, kwa hivyo ni jambo la busara kusasisha picha zako mara kwa mara na kukumbuka kuonyesha maelezo fulani.

    • Weka umakini kwenye picha yako ya kwanza. Pamoja na kichwa cha tangazo lako, hili ndilo jambo la kwanza ambalo wageni wataona katika matokeo ya utafutaji. “Ninapotafuta kwenye Airbnb, huwa ninaenda moja kwa moja kwenye picha. Kwa hivyo fikiria kuhusu kile ambacho kinatofautisha eneo lako na maeneo mengine,” anasema Candida, Mwenyeji huko Joshua Tree, California.
    • Tumia picha za sehemu yako yote. Kuweka kama picha tatu za kila chumba kutoka pembe tofauti huwapa wageni ziara ya mtandaoni ya sehemu yako.
    • Andika maelezo mafupi yenye ufafanuzi. Maelezo yako mafupi ni mahali pazuri pa kuwaambia wageni wako kuhusu maelezo muhimu. Kwa mfano, usisahau kuelezea meza ya kuchezea mchezo wa pool au bafu ya kuoga kwa kujiloweka.
    • Onyesha vipengele vya ufikiaji.Wageni wengi hutafuta vipengele vya ufikiaji, kwa hivyo ni muhimu kuweka hivi kwenye maelezo na picha za tangazo lako.
    Angalia mafunzo yetu ya upigaji picha ili upate vidokezi zaidi

    Weka bei yako iwe ya ushindani

    Kiasi unachotoza kwa ajli ya tangazo lako ni juu yako kabisa. Haya ni baadhi ya mambo ya kuzingatia:

    • Wageni mara nyingi huweka kipaumbele kwenye bei wanapotafuta sehemu, kwa hivyo ni muhimu uhakikishe kwamba sehemu yako inatoa thamani nzuri kwa eneo na vistawishi unavyotoa. Ili kujua thamani ya eneo lako, unaweza kujaribu zana yetu.
    • Unapoweka bei yako ya kila usiku, ni muhimu ufikirie ada za ziada, kama vile ada za usafi, ada za mgeni wa ziada, ada za huduma na kodi za eneo husika na jinsi zitakavyoathiri bei ya jumla ambayo wageni wako watailipa.
    • Kama Mwenyeji mpya, unaweza kutaka kuanza kwa bei ya kila usiku ya utangulizi hadi utakapoandikiwa tathmini moja au mbili nzuri.
    • Kipengele cha Upangaji Bei Kiotomatiki kinakusaidia kuweka bei yenye ushindani kwa kurekebisha bei yako kiotomatiki kulingana na uhitaji wa matangazo yanayofanana na lako.

    Orodha kaguzi kwa ajili ya tangazo lenye mafanikio

    Uko tayari kunufaika zaidi na tangazo lako? Hapa kuna orodha kaguzi fupi ya kukusaidia kuanza:

    • Je, mipangilio yako ya kalenda imesasishwa?
    • Je, umewasha kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo?
    • Je, maelezo na kichwa yanaeleweka vizuri na yanavutia?
    • Je, ni wazi katika maelezo yako kwamba unakaribisha watu wa aina zote?
    • Je, umeweka vistawishi vyako vyote?
    • Je, una picha kadhaa zenye ubora wa hali ya juu pamoja na maelezo ya picha?
    • Je, uliweka bei ya ushindani ya kila usiku?

    Mara baada ya kuanza kukaribisha wageni na kupokea maoni kutoka kwa wageni, ni wazo zuri kusasisha tangazo lako mara kwa mara, ukihakikisha kwamba maelezo yako na picha zinaonyesha kweli kile kilicho cha kipekee kuhusu sehemu yako.

    Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu wa kuweka tangazo lenye mafanikio

    Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

    Vidokezi

    • Andika maelezo sahihi na jumuishi ya tangazo

     • Hakikisha kalenda yako na mipangilio ya kuweka nafasi imesasishwa

      • Fahamu jinsi ya kudumisha ushindani wa bei yako ya kila usiku

      Airbnb
      18 Nov 2020
      Ilikuwa na manufaa?