Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

Jinsi ya kukaribisha wageni kwa masharti yako

Karibisha wageni kwenye sehemu yako kwa kurekebisha mipangilio na sheria za nyumba.
Na Airbnb tarehe 10 Nov 2020
Inachukua dakika 5 kusoma
Imesasishwa tarehe 16 Nov 2022

Vidokezi

  • Tangazo lako linakuwezesha kuweka idadi ya wageni unaowakaribisha na vistawishi wanavyoweza kufikia

  • Sheria za nyumba hukusaidia kuweka matarajio na kuwaonyesha wageni mtindo wako wa kukaribisha wageni

  • Mipangilio yako ya kuweka nafasi huamua wakati wageni wanaweza kuweka nafasi kwenye eneo lako

Kuwakaribisha watu ambao hujawahi kukutana nao kwenye sehemu yako kunaweza kuwa jambo jipya kwako. Ili kukusaidia ujisikie huru zaidi kukaribisha wageni, Airbnb ina mipangilio na vipengele vinavyokuwezesha kudhibiti jinsi na wakati wa kukaribisha wageni.

Kuanzia sehemu katika eneo lako zinazopatikana kwa wageni hadi idadi ya wageni wanaoweza kukaa, unaweza kurekebisha mipangilio yako ya kuweka nafasi kulingana na mahitaji, upatikanaji na mapendeleo yako.

Ikiwa huna uhakika kuhusu jinsi ya kuchagua mipangilio yako ya kuweka nafasi au kuunda sheria za nyumba yako, usiwe na wasiwasi. Tutakuongoza kupitia machaguo tofauti na kukupa mifano michache ya njia unazoweza kukaribisha wageni kwa masharti yako.

Unda tangazo dhahiri na lenye maelezo ya kina

Tangazo lako huwapa wageni fursa ya kuchunguza sehemu yako na kuwasaidia kupata ufahamu bora wa jinsi unavyoishi na bei kabla ya kuweka nafasi. Unapounda tangazo lako, fikiria:

  • Bei na ada za kila usiku unazotaka kutoza: Unapokaribisha wageni kwenye Airbnb, unaweka bei ya kila usiku unayowatoza wageni wako. Bei zako zinaweza kubadilishwa wakati wowote kabla ya kukubali nafasi iliyowekwa na zinaweza kutofautiana kutoka usiku mmoja hadi mwingine na msimu mmoja hadi mwingine. Unaweza pia kuchagua kujumuisha ada za ziada za kufanya usafi, wageni wa ziada na kadhalika. Vidokezi vyetu vya bei vinaweza kukusaidia kuweka bei yenye ushindani.
  • Idadi ya wageni unaoweza kukaribisha kwenye sehemu yako: Katika tangazo lako, onyesha idadi ya juu zaidi ya wageni ambao uko tayari kukaribisha kwa wakati mmoja. Wageni wanaweza tu kuweka nafasi kwenye eneo lako ikiwa idadi ya jumla ya watu katika kundi lao ni sawa au chini ya ile uliyoweka katika vigezo vyako vya kuweka nafasi.
  • Vistawishi vinavyopatikana kwa wageni: Kwa sababu tu una jiko la kuchomea nyama au mashine ya kuosha na kukausha haimaanishi kwamba unahitaji kuzifanya zipatikane. Unaweza kuonyesha vistawishi katika nyumba yako ambavyo wageni wanaweza kutumia, vile ambavyo hawawezi kutumia na vyovyote ambavyo vimezuiwa. Kwa mfano, Brian, Mwenyeji huko Newport, Rhode Island, anaandika katika maelezo ya tangazo lake, "Wageni wanaweza kutumia mashine yangu ya kuosha na kukausha wanapoomba."

Weka sheria za nyumba yako

Sheria za nyumba hukusaidia kuwa wazi kuhusu mtindo wako wa kukaribisha wageni na kuweka matarajio na wageni. Pia huwasaidia wageni kuamua mapema ikiwa nyumba yako inawafaa.

Sheria za nyumba yako sasa zinaangaziwa katika maeneo manne: kwenye ukurasa wa tangazo lako, wakati wageni wanaweka nafasi kwenye sehemu yako na kwenye barua pepe ya Pakia Mizigo Yako pamoja na Mwongozo wa Kuwasili ambao wageni hupokea kabla ya safari yao. Ukiwa na sheria za msingi, chochote unachojumuisha katika sheria za kawaida za nyumba yako kinaweza kutekelezwa.

Unaweza kuchagua sheria za kawaida za nyumba yako kutoka kwa seti ya machaguo yasiyobadilika katika maeneo yafuatayo:

  • Wanyama vipenzi
  • Matukio
  • Uvutaji sigara, uvutaji wa mvuke wa sigara za kielektroniki na sigara za kielektroniki
  • Saa za utulivu
  • Nyakati za kuingia na kutoka
  • Idadi ya juu ya wageni
  • Kupiga picha na kurekodi video za kibiashara

Kama kawaida, unaweza pia kuongeza seti iliyoandikwa ya sheria za ziada ili kuambatana na sheria za kawaida za nyumba yako. Sheria zako za ziada zinapaswa kubainisha kitu chochote ambacho wageni hawaruhusiwi kufanya, kama vile kuingia kwenye roshani ya kujitegemea au kabati la kuweka vitu vya mtu binafsi. Unaweza pia kujumuisha sheria zinazohusiana na desturi za eneo lako na za kikanda (kama vile kukaa kimya wakati wa usingizi wa mchana) na matakwa ambayo hayajajumuishwa katika sheria za kawaida za nyumba (kama vile kutovaa viatu ndani ya nyumba).

Ikiwa unaamini kwamba mgeni anakiuka sheria zako, iwe ni zile ulizochagua au zile ulizoandika, wasiliana na Usaidizi wa Jumuiya. Tutakusaidia ikiwa utahitaji kughairi nafasi iliyowekwa.

Kumbuka: Sheria zote za nyumba lazima zipatane na sera na masharti ya Airbnb, ikiwemo masharti yetu ya huduma na sera ya kutobagua.

Jinsi ya kuhariri sheria za nyumba yako

Chagua mipangilio yako ya kuweka nafasi

Tumia mipangilio ya kalenda yako na ya kuweka nafasi ili uweke upatikanaji wako na utambue aina za nafasi unazotaka uwekewe. Unapoamua mipangilio yako ya kuweka nafasi, fikiria:

  • Upatikanaji wako: Wewe ndiye unayeamua wakati ambapo ungependa kufanya eneo lako lipatikane kwa wageni. Ikiwa utakuwa nje ya mjini, unakaribisha marafiki au familia au huwezi kukaribisha wageni katika nyakati fulani, unaweza kuzuia kalenda yako kwa tarehe mahususi. Ikiwa ungependa kuwa na muda zaidi wa kufanya usafi au kupumzika baada ya mgeni kuondoka na kabla ya mwingine kuingia, unaweza pia kuweka muda wa kawaida wa maandalizi kabla ya kila nafasi iliyowekwa ili kuunda kizuizi baada ya kila mgeni kuondoka na kabla ya mwingine kuingia.
  • Jinsi wageni wanavyoweza kuweka nafasi: Kama Mwenyeji, unaweza kuchagua jinsi wageni wanavyoweka nafasi kwenye sehemu yako: iwe ni kwa kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo au kwa kutuma ombi la kuweka nafasi. Kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo huwaruhusu watu ambao wanakidhi mahitaji yako yote ya mgeni na kukubali sheria za nyumba yako kuweka nafasi ya sehemu yako papo hapo kwa tarehe zozote zinazopatikana. Ukiwa na maombi ya kuweka nafasi, unatathmini na kukubali kila ombi kivyake.
  • Muda ambao unataka wageni wakae: Unaweza kuchagua muda wa chini na wa juu wa kukaa katika eneo lako, kwa kuzingatia sheria za eneo lako. Baadhi ya Wenyeji hurekebisha matakwa yao kulingana na uhitaji wa kimsimu, wakihitaji muda wa chini wa usiku mbili au hata wiki moja wakati wa vipindi vya wageni wengi.
  • Ilani ya mapema: Je, huna uhakika lini utapatikana ili kukaribisha wageni katika siku zijazo? Usiwe na shaka. Tumia mipangilio yako ili udhibiti muda wa mapema unaotaka kukubali nafasi zinazowekwa. Kwa kufanya hivyo, wageni hawawezi kuweka nafasi kwa tarehe ambazo hauko tayari kuwakaribisha. Unaweza pia kuweka kiasi cha ilani unayohitaji kabla ya wageni kuwasili, kwa mfano, unaweza kutumia mipangilio yako ili kuepuka nafasi zinazowekwa za siku hiyo hiyo au siku inayofuata ikiwa ungependelea kuwa na ilani zaidi kabla ya mgeni kuwasili.
  • Wakati wa kuwasili na kuondoka kwa wageni: Kuchelewa kutoka na kuwasili mapema kunaweza kuingiliana na nafasi nyingine zilizowekwa, hasa ikiwa una nafasi zilizowekwa ambazo zinafuatana. Unaweza kutumia mipangilio yako kuweka wakati wa kuwasili na kuondoka kwa wageni na kuhariri tangazo lako ili kuelezea kwa nini ni muhimu kwa wageni kuzingatia nyakati hizi (kwa mfano: "Msafishaji atawasili saa 5 asubuhi").

Kumbuka, mipangilio yako ya kuweka nafasi inaweza kurekebishwa wakati wowote. Inaweza pia kuwa muhimu kutathmini mipangilio yako ya kuweka nafasi mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba inalingana na upatikanaji wako wa sasa na mapendeleo ya kukaribisha wageni.

Karibisha wageni ukiwa na uhakika

Wenyeji hufurahia wageni ambao huchukulia eneo lao kana kwamba ni lao wenyewe. Katika Airbnb, tumetekeleza sera na ulinzi kadhaa ili kukusaidia kuvutia wageni ambao wataweza kufaa sehemu yako.

Mbali na ulinzi huu, maelezo ya wazi ya tangazo, sheria za kina za nyumba na mipangilio ya hivi karibuni ya kuweka nafasi inaweza kusaidia kuhakikisha kwamba eneo lako linaheshimiwa, kukupa uhakika zaidi na kukusaidia kuwapa wageni wako huduma bora.

Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

Vidokezi

  • Tangazo lako linakuwezesha kuweka idadi ya wageni unaowakaribisha na vistawishi wanavyoweza kufikia

  • Sheria za nyumba hukusaidia kuweka matarajio na kuwaonyesha wageni mtindo wako wa kukaribisha wageni

  • Mipangilio yako ya kuweka nafasi huamua wakati wageni wanaweza kuweka nafasi kwenye eneo lako

Airbnb
10 Nov 2020
Ilikuwa na manufaa?