Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Maudhui haya hayapatikani katika lugha uliyochagua, kwa hivyo tumeifanya ipatikane kwa lugha iliyo karibu zaidi inayopatikana kwa sasa.

  Sera na ulinzi ili kukusaidia ukaribishe wageni kwa kujiamini

  Pata maelezo kuhusu vidhibiti vya Mwenyeji, sheria za nyumba, viwango vya wageni na zaidi.
  Na Airbnb tarehe 20 Okt 2020
  Inachukua dakika 5 kusoma
  Imesasishwa tarehe 9 Nov 2021

  Vidokezi

  • Tunatoa nyenzo nyingi za kukusaidia kudhibiti ni wakati gani na jinsi gani unakaribisha wageni

  • Sheria za nyumba ni njia bora ya kuweka matarajio na tunakusaidia kuangazia katika mchakato mzima wa kuweka nafasi

  • Pia tunatekeleza viwango vya mgeni na kuwawajibisha wageni kwa sera zetu za jumuiya, kama vile sera yetu ya kutobagua

  Airbnb imechukua hatua kadhaa ili kukusaidia kuwavutia wageni ambao watafaa kwenye sehemu yako—na kukutendea wewe na mali zako kwa heshima.

  Kwa kuzingatia mahitaji yanayobadilika kila mara ya jumuiya yetu, tunasaidia kuboresha uzoefu wako na wageni kwa kukupa udhibiti zaidi juu ya nafasi zako zilizowekwa na hivyo kukupa taarifa zaidi kuhusu wageni na kukusaidia kulinda mali zako.

  Amua kinachokufaa

  Kuanzia na idadi ya watu wanaoweza kukaa na sehemu wanazoweza kufikia, unawafahamisha wageni kinachokufaa.

  Baadhi ya mipangilio utakayoamua ni pamoja na:

  • Jinsi wageni wanavyoweka nafasi: Unachagua jinsi wageni watakavyoweka nafasi kwenye eneo lako—kwa kutumia kipengele cha Kuweka Nafasi Papo Hapo au kwa kufanya maombi ya kuweka nafasi mwenyewe.
  • Utambulisho: Wageni lazima watoe jina lao kamili, tarehe ya kuzaliwa, nambari ya simu, anwani ya barua pepe na taarifa ya malipo kwa Airbnb kabla ya kuweka nafasi. Pia una chaguo la kuwataka wageni kuipa Airbnb kitambulisho cha serikali kabla ya kuweza kuweka nafasi. Pata maelezo kuhusu jinsi ya kuomba wageni wathibitishwe
  • Kipindi cha kuweka nafasi: Unaweza kudhibiti muda wa kabla wa kukubali nafasi zinazowekwa. Kwa mfano, unaweza kuchagua kuzuia tarehe miezi 3, 6 au 12 kuanzia leo.
  • Ilani ya mapema: Unachagua urefu wa ilani unayohitaji ili kujiandaa kupokea wageni—kwa mfano, kuepuka nafasi zinazowekwa siku hiyo hiyo au siku inayofuatia.
  • Urefu wa safari: Unaweza kuweka muda wa chini na wa juu zaidi wa ukaaji kwa ajili ya wageni wako kwa kuzingatia sheria za eneo husika.

  Pata maelezo zaidi kuhusu kuchagua mipangilio ya kuweka nafasi

  Weka matarajio na sheria za nyumba

  Wasaidie wageni kutathmini iwapo sehemu yako inawafaa kabla ya kuiwekea nafasi kwa kushiriki matarajio yako—kama vile ikiwa sehemu fulani za sehemu yako zimezuiliwa au ikiwa wageni hawaruhusiwi. Kuwapa wageni kionjo cha mambo ya kutarajia kunaweza kuleta uzoefu mzuri na tathmni nzuri zaidi.

  Kwa sababu ya umuhimu wa sheria za nyumba, tutazifanya zionekane hata zaidi na wageni ifikapo mwezi Novemba mwaka 2020:

  • Sheria kuu za nyumbani—kama vile kutoruhusu kuvuta sigara au wanyama vipenzi—zitaonekana kwenye sehemu ya juu ya ukurasa wa tangazo lako ili ziwe dhahiri zaidi wageni wanapotafuta.
  • Sheria zote za nyumba ambazo umetangaza, pamoja na ufichuzi wa usalama, zitaonekana katika maelezo ya ukurasa wa tangazo lako.
  • Sheria za nyumba zitaonyeshwa tena kwenye ukurasa wa uthibitishaji wa nafasi iliyowekwa ili kusaidia kuhakikisha kuwa wageni wanazielewa na kuzikubali kabla ya kukamilisha kuweka nafasi.
  • Pia zitajumuishwa katika barua pepe ya uthibitishaji wa nafasi iliyowekwa ili kuwakumbusha wageni kuhusu matarajio yako kabla ya kuwasili.

  Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia vyema zaidi sheria za nyumba

  Unaweza pia kuweka taarifa muhimu za usalama kwenye tangazo lako kwa kujibu maswali machache kuhusu vipengele vya usalama na vistawishi, kama vile ikiwa una kamera za usalama au unahitaji kupanda ngazi mbili za kuelekea kwenye mlango. Hii inaweza kusaidia kuzuia mambo yasiyotarajiwa wakati wa kuingia na kusaidia wageni wako wawe na huduma bora kwa ujumla.

  Kumbuka: Sheria zote za nyumba lazima zipatane na sera na masharti ya Airbnb—pamoja na masharti yetu ya huduma na sera ya kutobagua.

  Ulinzi wa Mwenyeji

  Ingawa ni nadra, ajali wakati mwingine hutokea. Lakini unaweza kuwa na uhakika kujua kwambaAirCover inajumuisha ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji na bima ya dhima ya Mwenyeji.

  Ili kusaidia kuweka jumuiya yetu salama, tunajaribu pia kugundua sherehe kwa niaba ya Wenyeji inapowezekana. Hivi ndivyo tunavyofanya ili kukulinda:

  Arifa za kughairi: Hivi karibuni, tutashiriki arifa katika kikasha chako ikiwa tutaghairi au kuzuia nafasi zilizowekwa ambazo zinaweza kuwa zimeongoza kwenye sherehe, kulingana na tathmini za awali za wageni ambazo zinataja sherehe na vigezo vingine. Tunajua linaweza kuwa jambo linalofadhaisha wakati nafasi zilizowekwa zinaghairiwa bila kutarajia, kwa hivyo tunataka kukupa muktadha zaidi kuanzia sasa na kuendelea.

  Kughairi kunakodhibitiwa na Mwenyeji: Kufikia mwisho wa mwezi Oktoba mwaka 2020, utaweza kughairi mara moja nafasi iliyowekwa ambayo una sababu halali ya kuamini kwamba itaongoza kwenye sherehe—kulingana na nyuzi za ujumbe au tathmini za awali za mgeni ambazo zinataja sherehe—bila kuwasiliana na kitengo cha usaidizi. Maadamu sababu yako imeidhinishwa na timu yetu ya tathmini, hutapokea adhabu za kifedha wala hadhi yako ya Mwenyeji Bingwa haitaathiriwa.

  Timu yetu inapotathmini kughairi, itatafuta ushahidi wa uwezekano wa sherehe kutoka kwenye tathmini za awali za mgeni au nyuzi za ujumbe. Ingawa mchakato huu utaruhusu Wenyeji kughairi wanaposhuku kutakuwa na sherehe, hatua zote za kughairi lazima zifuate sera ya kutobagua ya Airbnb.

  Kukiwa na ulinzi huu uliowekwa pamoja na baadhi yahatua za kimsingi za usalama kwa upande wako, unaweza kukaribisha wageni ukiwa na uhakika zaidi. Kwa maelezo zaidi kuhusu njia muhimu ambazo Airbnb hutumia kuwaweka Wenyeji na wageni salama, tembelea ukurasa wa Airbnb wa Uaminifu na Usalama.

  Mwongozo wa jumuiya

  Airbnb pia inachukulia kwa uzito suala la kudumisha Mwongozo wa Jumuiya, ambao huzingatia kusaidia kuhakikisha usalama na hali ya kujisikia nyumbani katika jumuiya yetu ya kimataifa. Hapa chini kuna baadhi ya njia tunazohimiza ahadi hii inayoshirikiwa na Wenyeji na wageni.

  • Viwango vya wageni: Viwango vyetu vya kutegemeka kwa mgeni vinafafanua kile ambacho Airbnb inatarajia kutoka kwa wageni, kwa lengo la kuhakikisha kwamba Wenyeji wanaweza kupata mara kwa mara uzoefu mzuri. Mgeni anaporipotiwa kwa kutokidhi mojawapo ya viwango vilivyoainishwa katika sera, tabia hiyo inazingatiwa pamoja na ukiukaji wa awali, ambao huongoza maamuzi ya utekelezaji yanayofanywa na Airbnb. Iwapo itabainika kwamba mgeni amekiuka viwango hivi, tutatoa taarifa kuhusu sera hiyo na maonyo. Wageni wanaokiuka viwango hivi mara kwa mara au kwa njia kubwa wanaweza kusimamishwa au kuondolewa.
  • Ahadi ya Jumuiya: Tunawaomba wageni na Wenyeji wakubali kumtendea kila mtu katika jumuiya ya Airbnb kwa heshima na bila kuhukumu au kubagua. Tunachukulia ripoti za ubaguzi kwa uzito sana nasi huchunguza ripoti zote tunazopokea. Timu yetu ya usaidizi wa jumuiya pia huchukua hatua za kurekebisha mambo tunapopata ukiukaji wa sera yetu ya kutobagua.

  Tunatarajia kwamba, baada ya muda, mabadiliko haya yataboresha tabia ya wageni na uzoefu wako kama Mwenyeji. Bado kuna kazi nyingi ya kufanywa na tunakushukuru kwa maoni unayoendelea kutupatia. Kama kawaida, asante kwa kuwa Mwenyeji.

  Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji na bima ya dhima ya Mwenyeji haziwalindi Wenyeji wanaotoa sehemu za kukaa kupitia Airbnb Travel, LLC au Wenyeji nchini China bara na Japani, ambapo Mpango wa Ulinzi wa Mwenyeji wa China na Bima ya Mwenyeji wa Japani hutumika. Ulinzi dhidi ya uharibifu kwa Mwenyeji hauhusiani na bima ya dhima ya Mwenyeji.

  Kumbuka kwamba vikomo vyote vya malipo vinaonyeshwa katika USD na kwamba kuna vigezo, masharti na vighairi vingine.

  Taarifa zilizomo kwenye makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.  Vidokezi

  • Tunatoa nyenzo nyingi za kukusaidia kudhibiti ni wakati gani na jinsi gani unakaribisha wageni

  • Sheria za nyumba ni njia bora ya kuweka matarajio na tunakusaidia kuangazia katika mchakato mzima wa kuweka nafasi

  • Pia tunatekeleza viwango vya mgeni na kuwawajibisha wageni kwa sera zetu za jumuiya, kama vile sera yetu ya kutobagua
  Airbnb
  20 Okt 2020
  Ilikuwa na manufaa?