Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kuandika sheria za nyumba zinazofaa

  Saidia kulinda nyumba yako na kuunda uzoefu bora kwa wageni.
  Na Airbnb tarehe 1 Des 2020
  Inachukua dakika 3 kusoma
  Imesasishwa tarehe 13 Mei 2021

  Vidokezi

  • Sheria za nyumba hukusaidia kuonyesha vikumbusho vya usalama na kuweka matarajio ya wageni

  • Sasisha sheria za nyumba yako
  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili wa kuanzisha tangazo lenye mafanikio

  Sheria za nyumba yako zina maana zaidi ya orodha tu ya mambo ya kufanya na kutofanya. Zinaweka maratajio kwa wageni na kuwadokeza mtindo wako wa kukaribisha wageni. Pia huwasaidia wageni watathmini iwapo sehemu yako inawafaa kabla hawajaweka nafasi, jambo ambalo linaweza kuleta uzoefu bora. Kwa sababu ya umuhimu wa sheria za nyumba, tumezifanya zionekane kwa wageni wakati wanaweka nafasi.

  Je, unahitaji msaada wa kuandika zako? Fuata vidokezi hivi kutoka kwa Wenyeji kama wewe.

  Fanya iwe rahisi

  Tumia lugha ya wazi ambayo ni rahisi kueleweka. "Sheria za nyumba hazipaswi kuwa kama maandishi ya kisheria. Ikiwa zitaandikwa hivyo, hakuna mtu ambaye atazisoma au wageni watarajiwa wanaweza kwenda kwenye tangazo jingine ambalo lina sheria za nyumba ambazo ni rahisi," anasema J Renata, Mwenyeji huko Rio de Janeiro.

  Njia bora ya kufanya mambo yawe rahisi ni ipi? Fikiri kuhusu namna ambavyo ungependa mgeni akae kwenye sehemu yako na jinsi ambavyo ungeelezea kana kwamba unazungumza naye ana kwa ana, basi andika jinsi hiyo.

  Pia usingependa kuwachosha wageni na sheria nyingi kupita kiasi. Weka mkazo kwenye yale yanayopaswa kuwepo na yaache yale ambayo ni vizuri yawepo kwa ajili ya kuyashiriki kwingineko.

  "Siweki maombi ya hisani au vidokezo, kama vile wapi pa kuweka taulo na jinsi ya kutumia sehemu ya kufulia, kwenye sheria zangu za nyumba," anasema mwenyeji Annette kutoka Prescott, Arizona. "Maelezo haya ninayatoa ninapokutana ana kwa ana na wageni wakati ninawaelekeza kwenye fleti, au ninaacha ujumbe wa kirafiki." Njia nyingine inaweza kuwa kutangeneza mwongozo wa nyumba kwa maelezo muhimu ambayo si lazima yawe kwenye sheria za nyumba yako.

  Sheria za nyumba hazipaswi kuwa kama maandishi ya kisheria; ikiwa zitakuwa hivyo, hakuna atakayezisoma.
  J Renata,
  Rio de Janeiro

  Vikumbusho vya usalama

  Usidhani kwamba wageni wanajitahidi kuzingatia usalama na ulinzi kama unavyofanya wewe. Ni wazo zuri kushiriki aina hii ya taarifa kwenye sheria zako za nyumba. Hivi ndivyo baadhi ya wenyeji walivyofanya:

  • "Tafadhali funga na bana kwa kufuli madirisha na milango yote unapokuwa unaondoka chumbani." —Dave na Deb, Edmonton, Kanada
  • “Hakuna mishumaa. Hakuna. Badala yake, tunakupa mishumaa isiyokuwa na mwali wa moto, inayotumia betri.” —Heather, Ithaca, New York

  Ni muhimu pia kusisitiza matakwa ya afya na usalama kuhusiana na COVID-19. Tumia sheria za nyumba yako kuwakumbusha wageni juu ya mazoea ya lazima kuhusu barakoa na kuepuka mikusanyiko na udokeze miongozo yoyote ya ziada kwa ajili ya sehemu za pamoja ikiwa ni lazima.

  Tumia fursa hiyo kuwaelimisha wageni

  Ikiwa wageni wako wanatokea mbali, huenda wasijue masuala mahususi kwa eneo au utamaduni wako. Sheria za nyumba yako zinaweza kuwa fursa ya kushiriki taarifa muhimu sana. Hivi ndivyo ambavyo baadhi ya wenyeji wamejumuisha maarifa ya eneo husika:

  • "Tunaomba uwe kimya na mwenye busara, hasa usiku au wakati wa kupumzika." —Beatriz Elena, Medellin, Kolombia
  • “Usiingie ndani na viatu. Hili ni jambo la kawaida nchini Thailand.” —Nutth, Chiang Mai, Thailand
  • “Upakuaji haramu umekatazwa. Ikiwa utakutwa na hatia, faini za serikali zinaweza kufikia hadi Euro 1,700 kwa kila filamu.” —Branka na Silvia, Zagreb, Kroatia

  Onyesha utu wako

  Sheria zako zinadokeza mtindo wako wa kukaribisha wageni. Ni njia mojawapo kwa wageni kuamua iwapo sehemu yako inawafaa, kwa hivyo jibainishe.

  Ikiwa mbinu yako ya kukaribisha wageni ni ya kustarehe na kupenda ucheshi, basi acha ucheshi kidogo uangaze. Je, unapenda vitu viwe kwenye mpangilio zaidi? Hakikisha hiyo inaelezewa waziwazi.

  Mwenyeji Amy kutoka Nashville anapenda kuingiza ucheshi kidogo kwenye sheria za nyumba:

  "Natarajia wageni wafanye mambo kama watu wazima:
  • Usichome nyumba
  • Usimpige teke mbwa wangu
  • Usile chakula kinachomwagika mezani
  • Kuna ndoo kadhaa za uchafu kwenye nyumba: choo si moja wapo”

  Sheria za nyumba husaidia kukulinda

  Katika tukio nadra ambapo kuna tatizo na mgeni, sheria za nyumba pia zinaweza kukusaidia kutatua mgogoro. Ikiwa mgeni atakiuka sheria ya nyumba, hatua yako ya kwanza inapaswa kuwa kuwasiliana na mgeni kisha ujaribu kutatua tatizo hilo moja kwa moja. Ikiwa mtashindwa kupata suluhisho, wasiliana na kitengo cha huduma kwa mteja cha Airbnb ili kupata usaidizi.

  Kumbuka: Sheria zote za nyumba lazima zikubaliane na sera na masharti ya Airbnb—ikiwa ni pamoja na masharti yetu ya huduma na sera ya kutobagua. Pata maelezo zaidi

  Taarifa zilizo ndani ya makala hii zinaweza kuwa zimebadilika tangu zilipochapishwa.

  Vidokezi

  • Sheria za nyumba hukusaidia kuonyesha vikumbusho vya usalama na kuweka matarajio ya wageni

  • Sasisha sheria za nyumba yako
  • Gundua mengi zaidi kwenye mwongozo wetu kamili wa kuanzisha tangazo lenye mafanikio
  Airbnb
  1 Des 2020
  Ilikuwa na manufaa?